Matukio haya yanalitia doa Jeshi la Polisi

Matukio haya yanalitia doa Jeshi la Polisi

katumbwalala

Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
27
Reaction score
20
JANA vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini viliandika kuhusu kukamatwa kwa askari wawili waliokuwa wakisafirisha magunia 18 ya bangi kwa kutumia gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha.
Habari hiyo iliongeza uchafu kwenye taswira mbaya ya jeshi hilo, ambalo katika siku za karibuni watumishi wake wanatuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.
Miongoni mwa kashfa zinazoliandama jeshi hilo ni askari wake kujihusisha na biashara za magendo kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Kulazimisha rushwa ya sh milioni 25 baada ya kumbambikia mfanyabiashara fuvu la mtu, kukimbia na sh milioni 150 walizoziokoa kutoka kwa watuhumiwa wa ujambazi eneo la Kariakoo, Dar es Salaam na kupoteza ushahidi wa bangi iliyokuwapo Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, hayo ni baadhi ya maovu yanayofanywa kila uchao na askari hao ambao huua raia kwa risasi zinazonunuliwa kwa kodi za wananchi wote.

Tunasikitishwa na matukio hayo, kwa kuwa askari polisi ndio wenye dhamana ya kulinda raia na mali zao, wanapokuwa madalali wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya tunapata ukakasi, nani atamfunga paka kengele?
Askari waliokuwa wakisafirisha magunia 18 ya bangi kwa lengo la kuipeleka nchini Kenya kupitia Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ni F. 1734 Koplo Edward na G. 2434 Konstebo George, wakiwa kwenye gari namba PT 2025.
Baada ya kukamatwa, askari hao walisema wanaipeleka bangi hiyo kwa mfanyabiashara kwa ajili ya kusafirishwa. Hii ni aibu, utovu wa nidhamu na matumizi mabaya ya mali za serikali.
Tanzania Daima tunajiuliza, ikiwa polisi waliopewa dhanama ya kutokomeza dawa za kulevya wapo kwenye biashara hiyo, nani atawakamata? Hawa wanashirikiana na viongozi wao.
Tunaamini kwamba maovu yanayofanywa na askari polisi yanaharibu dhana nzuri ya polisi jamii na kuwalazimu raia kukosa imani na jeshi hilo, ndiyo maana kasi ya wananchi kujichukulia sheria mikononi imeshamiri.
Hatupendi kuona wananchi wakivamia vituo vya polisi na kufanya chochote kibaya wanachoweza, lakini kwa uhalifu unaofanywa na askari polisi ni dhahiri kwamba amani ya nchi hii inaelekea nchani iwapo askari hao wataachwa.
Tunasema hivyo kwa kuwa upo usemi wa funika kombe mwana haramu apite, wenye mamlaka watasubiri Watanzania wasahau kwa vile nyuma ya askari hao wapo viongozi wakubwa.
Wakati umefika kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema, kusafisha jeshi lako na kuhakikisha askari wanaoharibu taswira ya jeshi hilo wanapewa adhabu kali ili kuwa mfano kwa wengine.
Said Mwema, vita ya dawa za kulevya ni moja ya changamoto kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, pambana na wote wanaoliharibu taifa kwa biashara hii, msaidie Rais Jakaya Kikwete katika hili la mihadarati.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Matukio haya yanalitia doa Jeshi la Polisi


ban_tahariri.jpg

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
amka2.gif
[/TD]
 
baadhi ya matatizo yanainjiniwa na chadema kwa ukaribu sana
 
Doa linaonekana kama limewekwa kwenye kitu kisafi!!! Hili jeshi lina uozo kibao hivyo kusema linatiwa doa ni kulionea aibu!!! SEMA JESHI LA POLISI NI CHAFU au LINAUOZO!!!!
 
Kama kawaida viongozi wa juu wa jeshi la polisi watakaa kimya kama vile hakuna kilichotokea.
 
kwani nani alizitoa hizi taarifa? ni polisi wenyewe au ni nyie? kama niwao polisi ndio walizitoa hizi taarifa watakaaje kimya tena? wangetaka kukaa kimya wasingetoa taarifa hizo kwenye media!!!
 
Back
Top Bottom