Mto_Ngono
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 686
- 589
Mjini na tochi hazifai kabisa. Matrafiki najua mnatimiza wajibu wenu ni vizuri sana lakini pia ni vizuri kuangalia na mazingira ambayo mnafanyia kazi na msiyabebe kuwapendelea nyie tu bali angalieni na jamii inayowazunguka. Nachoamini lengo la uwepo wenu sio fine bali mazingira salama kwa watumiaji wote wa barabara. Naamini zaidi kuwa watu wengi wangependa kuona kila kitu kinafanyika kwa kufuata sheria na taratibu na sidhani kama watu wanapenda ajali ziendelee kutokea.
Katika kudhibiti mwendo katikati ya mji zipo alama zinazoonesha mwendo unaotakiwa kwenda. Alama hizo hata barabara za nje ya mji kuelekea mikoani zipo lakini huonesha zinapoanzia na kuishia kwa mfano unakuta alama inahitaji uende mwendo wa 50km/h na pia uendapo mbele unakuta alama inayoonesha ukomo wa mwendo huo. Kwa mjini iko tofauti kwa mfano. alama mitaa ya bondeni/kawe New bagamoyo Rd inaonesha alama inapoanzia lakini inapoishia hakuna kwa hiyo hujikuta bado upo ndani ya 50km kwa umbali mrefu bila kujua ukomo wa mwendo huo na maeneo hayo tochi zipo.
Uwepo wa tochi ni mzuri kudhibiti mwendo ndani ya mjini lakini tunawaomba mtusaidie kuweka alama za barabarani zionekane vizuri haswa kuweka ukomo wa mwendo pale kunapokuwa na alama ya awali ya kudhibiti mwendo, kuchora mistari ya barabarani vizuri (lane demarcation lines), na kuzifanyia maboresho alama zote za barabarani.
Zaidi nashauri uboreshwaji wa mfumo wa utatuaji malalamiko haswa pale dereva au mmiliki wa chombo anapoonewa kwa kuandikiwa kosa lisilosahihi. Itakuwa vizuri kama matrafiki watakuwa na vyombo vizuri na vya haraka vya kuchukua ushahidi wa kosa alilofanya dereva ili isilete utata na mzunguko mrefu wa kumuadhibu. Vyombo hivyo pamoja na kurahisisha ushughulikiaji wa makosa hayo itasaidia pia kuokoa muda wa askari na mmiliki wa chombo (muda ni mali haukusubiri).
Nadhani niliyoshauri yatazingatiwa.