likemike
Senior Member
- Mar 10, 2016
- 115
- 56
Ni vigumu msanii aliyepotea kwenye game kurejea kwa kishindo kile kile. Hii ipo ata kwenye msemo wa kiingeereza – “Golden Chance Never Comes Twice,” – yaani bahati haijirudii mara mbili.
Hata hivyo, kuna wakati bahati inaweza kijirudia, kama ilivyokuwa kwa Jay Moe – Pesa Madafu, na sasa Jay Moe – Nisaidie Kushare au hata kwa Ray C – Unanimaliza.
Na hivyo basi, bahati kujirudia si kwa Jay Moe na Ray C pekee, Matonya emerejea tena kwenye game ya Bongo Flava. Na sasa, ni dhahiri Matonya is here to stay, atakuwepo kwa kipindi kirefu sana. Nyimbo yake ya sasa Matonya – Nifungulie ni kiashiria tosha.
Matonya alifanya vizuri sana kwenye Game ya Bongo Flava mwaka 2006 na Album ya Siamini iliyokuwa na nyimbo mashuhuri kama Vaileth, Dunia Mapito na Siamini. Matonya pia alifanya vema mwaka 2008 na Album yake – Safari ya Dunia aliyomshirikisha Prof. Jay, Joslin, Klyinn (Jackline Mengi), TID Mnyama na Lady Jay Dee commando. Nyimbo zilizofanya vizuri kwenye Album hiyo ni pamoja na Matonya x Lady Jay Dee – Anitha na Matonya x Lady Jay Dee – Taxi Bubu.
Hivi karibuni, Matonya ametoa nyimbo kadhaa kama Matonya – Hakijaeleweka aliyoitoa mapema mwezi January, 2017. Mwaka 2015 Matonya alitoa nyimbo iliyojipatia mashabiki karibu milioni moja Youtube. Katika nyimbo hiyo ya Matonya – Mule Mule alimshirikisha Rich Mavoko . Nyingine ni pamoja na Matonya – Sugua Bench iliyotoka wiki ya pili ya mwezi October, mwaka 2016.
Matonya anayeonekana kurejea kwa kasi, hasa baada ya nyimbo zake kuanza kutawala kwenye mitandao ya kijamii na vituo vya redio, bado ana kazi kubwa ya kuwaaminisha mashabiki wake atawapa kile wanachokitegemea kutoka kwake, na pengine zaidi.
Matonya kujipatia watazamaji elfu 76 kwa kipindi cha siku nne Youtube akishindana na Nikki wa Pili x G Nako – Quality Time kunapaswa kumuongezea ari Matonya kutengeneza nyimbo bora zaidi, kutengeneza mwili wa kisanii, kutengeneza video nzuri na kutoipoteza nafasi yake tena – Golden Chance Never Comes Thrice.
Chanzo; kibandaumiza.comhttp://www.kibandaumiza.com/matonya-amerudi/