Matokeo ya uchaguzi yatangazwa Malawi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,677
2,000

Baadhi ya wagombea wa uchaguzi mkuu wa Malawi

Hatimaye Tume ya uchaguzi nchini Malawi imeanza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jumanne iliyopita.

Matokeo hayo ambayo ni asilimia 30 tu ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa yanaonyesha kuwa mgombea wa chama kikuu cha upinzani Democratic Progressive Party-DPP Profesa Peter Mutharika anaongoza kwa kura 683,621 akifuatiwa na Dr Joyce Banda wa Peoples Party kwa kura 372,101


Mgombea Urais wa chama kikongwe cha kisiasa nchini humo, Malawi Congress Party MCP Mchungaji Dr Lazarus Chakwera anashika nafasi ya tatu kwa kujipatia kura 289,145 huku Atupele Muluzi wa United Democratic Front- UDF akikusanya kura za wamalawi 269,250
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye anafuatilia uchaguzi huo nchini humo, amesema mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mackson Mbendera aliwaambia waandishi wa habari mjini Blantyre usiku wa kuamkia leo kuwa tume yake kwa pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa wamethibitisha matokeo hayo.


Udanganyifu
Katika mkutano huo Jaji Mbendera amesema tume yake imegundua kuwa kulikuwa na udanganyifu katika baadhi ya maeneo ambapo wamekuta idadi ya kura zilizopigwa ni zaidi ya watu walioandikishwa kupiga kura, na kwamba wamezuia matokeo hayo hadi watakapo pata ufumbuzi na ukweli wa hali ilivyokuwa.


Wakati huo huo Mahakama nchini humo imezuia uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la utangazaji la Malawi MBC kumlazimisha Mkurugenzi Mkuu Dr Benson Tembo kwenda likizo ya lazima na haraka.
Uamuzi huo umefuatia baadhi ya wanasheria kutoka kamisheni ya wanasheria wa Lilongwe kuweka zuwio mahakamani kupinga uamuzi wa bodi ya shirika hilo.


Itakumbukwa kuwa ijumaa asubuhi Dr Tembo alipewa barua ya kumtaka aende likizo ya lazima kutokana na madai kuwa ameshindwa kufuata maelekezo ya mwajiri wake ambaye ni serikali.


Miongoni mwa madai hayo ni pamoja na vyombo vya shirika hilo ikiwemo television na radio za taifa kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi ambayo hayajathibitishwa na Tume ya uchaguzi.


Pia MBC ilishindwa kurusha moja kwa moja matangazo ya mkutano wa Rais Joyce Banda na waandishi wa habari mjini Lilongwe siku ya alhamis, ambapo Dr Banda alikuwa akitoa maelekezo kwa tume ya uchaguzi kuanza kuhesabu kura kwa kutumia mikono na kuzuia kutoa matokeo kutokana na udanganyifu uliojitokeza.mia

Chanzo:BBC
 

RealMan

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,367
1,250
Huyu mama hachomoi

Na sijui sheria yao ya uchaguzi ikoj, is it 50% +1????????
 

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,316
2,000
Huyu mama hachomoi

Na sijui sheria yao ya uchaguzi ikoj, is it 50% +1????????

Hiyo sheria huko haipo kabisa. Ukishinda hata kwa kura moja unakuwa raisi wa nchi, ndo maana yule mama alihamasisha watu wengi kuingia katika kinyanganyiro kama wagombea ili kugawa kura za wapinzani lakini wapi?
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,146
1,250
Mmh, mbona kuna taarifa kwamba uchaguzi umefutwa? Hawa BBC nao wanajichanganya tu. Inasemekana kuwa Banda amefuta matokeo yote ya uchaguzi na ametangaza kwamba uchaguzi utarudiwa tena baada ya siku tisini
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Wamshukuru Mungu Malawi si nchi ya kikabila kama majirani zetu wengi....ingekuwa kuna ukabila kabila la huyu mama na la Professor wangeshaagiza mapanga China....

Ukabila mbaya sana...unafanya watu wawe blind....wanakuwa tayari kuongozwa hata na Ghost as long as ni kutoka kabila lao...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom