Matokeo ya uchaguzi Igunga yaharakishwe hapa JF

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
974
Imekuwa ni kawaida ya watanzania wengi na hata humu JF kutaka matokeo yaliyojumlishwa na Tume. Inapokuwa hivyo basi hakuna kujishughulisha kujua kila kituo matokeo yalikuwa vipi kwa kila chama. Mwisho wake ni kuisubiri idadi ya jumla itakayotajwa na TUme na ndipo tunaoanza ama kushangilia ama kutupiana maneno na kejeli mbalimbali.

Hii inaashiria nini? Inaashiria kwamba kama hatupendi kuchanganua kituo kwa kituo basi hatustahili kuitwa Thinkers kwa sababu ya uvivu wetu wa kujumlisha wenyewe. Kwa nini mtu ukae mtandaoni ukisubiri Tume ikujumlishie wakati inawezekana kabisa kkupata idadi ya matokeo kwa kila kituo.

Kama vyama vitafanya tena kosa hili basi tusisumbuane kusema kimeibiwa wakati hatujui ni kituoa gani waliiba zaidi na wapi walishindwa kuiba.

Tuanze sasa hivi kuchanganua ikibidi kwenye thread hii, Je, Igunga ina vituo vingapi vya kupigia kura?. Tuvitaje vituo vyote. Nimeangalia website ya Tume nimeona kwamba uchaguzi ulipoita Rostam alipata kura 35,674 na Mahona wa CUF alipata kura 11,321. Hivyo walau jumla itakuwa karibu na hapo yaani 49,013 baada ya kuchanganya na kura 2,018 zilizoharibika.

Habari ya kusema chama fulani hakiwezi kutujulisha matokea mimi hainiingii akilini kwani ninajua kuwa pale kituoni matokeo yanaandikwa kwenye voucher moja na kila chama kinapewa kopi yake. Chama kama CHADEMA wanaweza kuamua kuwa mara tu wanapomaliza kupokea matokeo ya kituoni basi wakala awasiliane ama moja kwa moja na wadau wanaofikisha matokeo humu JF.

Kama tulishajiandaa na idadi yetu ya vituo basi kadiri tunavyopata matokeo basi tunakuwa tunajua kuwa ni kituo au vituo gani ambavyo bado hatujapata idadi ya kura.

Kwa wale ambao ni wavivu mimi sihangaiki nao. Binafsi nitawapa watoto wa dara la nne kama mtihani wa kunijumlishia idadi kulingana na kura zitakavyowasilishwa humu JF. S kwamba sijui hesabu. Na si kwamba sintajumlisha mwenyewe. Ninajua mathematics ya University level lakni nataka tu kuonyesa jambo hili la kujumlisha kura ni suala la kitoto tunapojikuta wote tunakaa kusubiri tujumlishiwe na tume kana kwamba hatukumaliza hata darasa la kindergaten.

Ikifanikiwa hivi. Basi safari hii tutajua nani mwongo na nani mkweli. Hatuwezi kuhubiriwa kuwa kura zinaibiwa wakati sisi tunachotaka ni idadi ya kura za vituoni na tuone ni jinsi gani sasa profesa wa kuiba kura anavyoweza kutudanganya wakati kila kituo tumeshapata idadi yake humuhumu JF na mitandao mingine.

Vituo hufungwa saa 10:00 au kidogo zaidi ya hapo. Musoma Mjini walimtangaza mbunge Vicent kwenye saa mbili usiku. Iweje Igunga ishindikane kuyajua matokeo ya vituo vyote saa nne usiku ya siku ya kupiga kura? Ni kijiji gani Igunga hakina network ya simu zote hapa nchini hadi tuchelewe kujua yanayojiri pale.

Hivyo, kazi kwetu. Kama tunaona hii ni upuuzi eti tuache tusikie tume itakavyotangaza basi utakuwa ni kurudia upuuzi kana kwamba hatukujifunza ya Octoba.

Japo nimetaja CHADEMA nina maana kwamba matokeo tunayoyataka humu JF ni yale waliyoya-sign mawakala pale kituoni ambayo sitarajii yawe tofauti.

Mimi sijali kama matokeo yatatangazwa kwenye kituo cha Poli au la. Cha msingi ni idadi ya kura za kituoni ambazo hata Tume ikishajua zimashafika mitandaoni kwa uhalisi wake basi kama kuna ujanja tutaona ni ujanja gani inabidi waufikirie.

Natumaini nimeeleweka na michango inayokuja itakuwa ni kuboresha na ya kueleweka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom