Matokeo ya rufaa kidato cha nne 2012 yametoka tupeni tathmini kwa walioyaona jamani

Matokeo hayajabadilika kwa asilimia 99.9. Wanafunzi watatu (4) ndio waliobadilishiwa. Walikataa rufaa kwa masomo ya Chemistry, History, Biology, na Hesabu. Masomo yote awali walipata F, sasa wote wamepata D. Japo nimepia kurasa zote 93 za CSEE; za awamu ya kwanza ila naweza kuwa nimekosa umakini kidogo, nimekosea katika uchambuzi wangu uniwie radhi.
Je Bujugo (Mkurugenzi wa Green Acress S. S) hajatoa kauli? Nasubiri, kama kuna, awamu ya pili.
 
Matokeo hayajabadilika kwa
asilimia 99.9. Wanafunzi watatu (3) ndio waliobadilishiwa. Walikataa
rufaa kwa masomo ya Chemistry, History, na Biology. Masomo yote awali
walipata F, sasa wote wamepata D. Japo nimepia kurasa zote 93 za CSEE;
za awamu ya kwanza ila naweza kuwa nimekosa umakini kidogo, nimekosea
katika uchambuzi wangu uniwie radhi.
Je Bujugo (Mkurugenzi wa Green Acress S. S) hajatoa kauli? Nasubiri,
kama kuna, awamu ya pili.

asante sana bado tunakalibisha tathmini zaidi ila necta dah bado wizi mtupuuuuuu
 
Matokeo ya QT ni mabaya asilimia 100.
Ila muda ya kujisajili kama mtahiniwa binafsi (Private Candidate) na QT umeongezwa mpaka tarehe 31 Machi 2013 bila ya faini. Kisha mwisho itakuwa tarehe 01 April 2013 kwa faini. Labda kwa kuwa ya rufaa hazikukamika kabla ya tarehe 28 Februari 2013.
Naona Dr J. Ndalichako amekomaa, yaani, liwalo na liwe (hata kuondolewa kwenye kiti).
 
we umeshayaona? Kwa sababu sina adobe pdf reader siwez kuyasoma

Namaanisha rufaa zingekuwa na maana sana kama kungekuwa na chombo kingine huru aambacho kingekuwa kinazishughulikia. Kwa akili ya haraka haraka sidhani kama kukiwa na tofauti kubwa ya matokeo hawa jamaa watakubali ionekane, kwa sababu implication yake ni kuwa hawakufanya kazi vizuri hapo awali. Hivyo kwa mantiki hiyo serikali ilitakiwa ilione hili ili kuwatendea haki wananchi wake.

Haya ni maoni yangu binafsi na wala sio kielelezo kwamba matokeo ya rufaa si sahihi ila huwa sina imani nayo kwa asilimia kadhaa. Ila kama kungekuwa na chombo huru cha kuyashughulikia imani yangu ingekuwepo. Ni ushauri tuu, Kwa sababu Kawambwa anapita hapa anaweza kuufanyika kazi huu ushauri.
 
Matokeo hayajabadilika kwa asilimia 99.9. Wanafunzi watatu (4) ndio waliobadilishiwa. Walikataa rufaa kwa masomo ya Chemistry, History, Biology, na Hesabu. Masomo yote awali walipata F, sasa wote wamepata D. Japo nimepia kurasa zote 93 za CSEE; za awamu ya kwanza ila naweza kuwa nimekosa umakini kidogo, nimekosea katika uchambuzi wangu uniwie radhi.
Je Bujugo (Mkurugenzi wa Green Acress S. S) hajatoa kauli? Nasubiri, kama kuna, awamu ya pili.

Gazeti la Nipashe linaonesha mabadiliko makubwa ya rufaa kwamba wengi wamefeli zaidi. Sasa ukweli ni upo wakuu maana hapa ni kwa GT lazima tujadili mambo yenye uhakika. Naomba tuwekane sawa Wakuu
 
nimepitia kurasa zote 93 za awamu ya kwanza, nimeona katika maoni kuwa hakuna mabadiriko katika matokeo ya awali. Je waliofeli zaidi Nipashe iliyatoa wapi.

rukaaragata
 
nimepitia kurasa zote 93 za awamu ya kwanza, nimeona katika maoni kuwa hakuna mabadiriko katika matokeo ya awali. Je waliofeli zaidi Nipashe iliyatoa wapi.

rukaaragata

Uko sahii mkuu.
Baada ya kupitia news nikakutana na habari hii kuwa waliokata rufaa ya matokeo yao ya kidato cha nne, hali imekuwa mbaya zaidi. Nikaona si vibaya kujiridhisha. Baada ya kupita kwenye web ya Necta nikagundua kuwa waandishi wamekoleza maneno yao. Hayajabadilika kama kwa asilimia 99 na point kadhaa. Hii imenifanya nitafakari aina ya waandishi wa habari tulio nao. Kumbe labda ndo maana Mzee Mkapa halikuwa hawakubali waandishi wa Bongo. Nimepitia kurasa zote 93, sehemu kubwa ya comment ni "Haijabalilia" hata wale wachache walio badiishiwa wengi wao wamepanda. Hii ni kinyume na maelezo ya kwenye magazeti. Shame kwa waandishi wetu. Au kuna watu walitaka kuwatisha!!!
 
Duuuuuu, hawa jamaa kama wameweza kuandika habari ya kupika namna hiyo ndiyo maana wanajiita NIPASHE. Jina lao tu limekaa kimajungu yaani mtu yeyote akiwaasha kwao inakuwa habari. Ni aibu sana kwa gazeti hilo maana suala la rufaa lilianza kujadiliwa JF tangu Jmosi ina maana hakuna mtu wa Nipashe anayetembelea humu?

Shame on them
 
Kwa nini hao Nipashe wasifungiwe. Hivi Mwanahalisi walikuwa wanaandika uongo kiasi hicho? Nimeshangaa sana taarifa iko kwenye mtandao wao wanatoa habari ya uongo mtupu.
Uhakiki wa vyeti uanzie kwa hao waandishi walioandika habari hiyo Thobias Mwanakatwe na Samson Fridiolin. Lazima elimu yao ina walakini
 
NIPASHE wamepotosha umma. Namkumbuka Roma "Siamini magazeti, waandishi wengi kanjanja". Hii habari ya NIPASHE ni ya kupikwa, huyu mwandishi amekaa chini ya mti na kujiandikia ndoto zake alizoota usiku.
 
Back
Top Bottom