nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
KITAIFA
Posted Alhamisi,Decemba25 2014 saa 7:4 AM
KWA UFUPI
Akisoma matokeo hayo jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tamisemi, Khalist Luanda alisema matokeo hayo yamekamilika kwa asilimia 99 kutokana na baadhi ya maeneo kutofanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wagombea kufungua kesi mahakamani na baadhi ya wagombea kufariki dunia kabla ya uchaguzi.
Dodoma/Dar. Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), imetangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14 na 21 yakionyesha kuwa uungwaji mkono wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo ya mijini umeporomoka kwa kasi.
Katika uchaguzi huo, chama kipya cha ACT-Tanzania kimechomoza na kuviacha baadhi yavyama vikongwe ambavyo havikupata hata nafasi ya ujumbe.

Jumla ya vyama 15 vilishiriki uchaguzi huo vikiwamo CCM, Chadema, CUF, NCCR - Mageuzi, TLP, NLD, ACT, UDP na APPT- Maendeleo. Vingine ni Chauma, NRA, UMD na vitatu ambavyo havikuambulia kiti hata kimoja vya DP, Tadea na ADC.
Matokeo
Pamoja na CCM kuendelea kuongoza kwa ujumla, chama hicho kimeonekana kupoteza viti mijini na vijijini na kimeporomoka zaidi mijini.
Katika maeneo ya vijiji na vitongoji, chama hicho kimepata ushindi wa asilimia 79.81 (vijiji) na 79.83 katika vitongoji, wakati kwenye mitaa ambayo ipo sehemu za mijini kimeshuka zaidi na kupata asilimia 66.66.
Matokeo hayo yakilinganishwa na yale ya mwaka 1999, chama hicho kimepata asilimia 89.2 katika mitaa, asilimia 91 katika vitongoji na asilimia 91.6 katika vijiji.
Matokeo ya vijiji
Idadi ya vijiji vyote Tanzania Bara vilivyotarajiwa kufanya uchaguzi ni 12,443 lakini umefanyika katika vijiji 11,750.
Matokeo ya vyama pamoja na asilimia katika mabano ni CCM 9,378 (79.8), Chadema 1,754 (14.9), CUF 516 (4.4), NCCR Mageuzi 67 (0.6) na TLP 10 (0.09).
Vingine ni UDP 14, ACT 8 (0.07), NLD 2 (0.02), (0.12) na NRA 1 (0.0001).
Uchaguzi wa vitongoji
Jumla ya vitongoji vilivyotarajiwa ni 64,616 lakini vilivyopiga kura 60,688 huku CCM ikiendelea kuongoza kwa kupata vitongoji 48,447 (79.8), Chadema 9,145 (15.1), CUF 2,561(4.2), NCCR Mageuzi 339 (0. 6), ACT 72 (0.12, TLP 55 (0.1), UDP 54 (0.1), NLD 2 (0.02).
Matokeo ya Mitaa
Mitaa yote 3,875 nchini ilifanya uchaguzi na kukamilika kwa asilimia 100 huku CCM ikipata asilimia 66.66 baada ya kupata mitaa 2,583, ikifuatiwa na Chadema iliyopata mitaa 980 (25.3), CUF 266 (6.9), NCCR Mageuzi 28 (0.7), TLP 1 (0.03), ACT 12 (0.31), UDP 3 (0.08), NRA 1 (0.03) na UMD 1(0.03).
Ukawa yachanua
Kwa matokeo hayo, inaonyesha kuwa vyama vinavyounda Ukawa vimeongeza nguvu katika maeneo mengi hasa mijini ambako kwa pamoja vimepata wenyeviti 1,275 ikiwa ni sawa na asilimia 32.18 ya mitaa yote.
Katika maeneo ya vijiji Ukawa wamepata jumla ya vijiji 2,339 ambayo ni asilimia 19.91 wakati kwenye vitongoji waliambulia 12,047 sawa na asilimia 19.87.
Wajumbe viti Maalumu
Kwa upande wa wajumbe wa viti maalumu ambao safari hii wamepigiwa kura badala ya kutokana na uwiano wa kura, CCM ilipata asilimia 80.24, Chadema (14.8), CUF asilimia (4.31), NCCR asilimia (0.48), ACT (0.08) huku APPT Maendeleo, Chauma na NRA vyote vikipata mjumbe mmoja kila kimoja sawa na asilimia 0.0001.
Waliopata sifuri walonga
Akizungumzia matokeo hayo, Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alisema, "hivi ni vitu vidogo na mara nyingi vinakosa uhalali wa kisheria. Ni vigumu sana kushinda uchaguzi Tanzania kwa mazingira yaliyojitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa."
Alisema ili chama kishinde lazima kitumie ubabe na mbinu chafu na katika uchaguzi wa aina mbalimbali nchini kunakosekana msingi wa demokrasia na haki ya kweli.
Katibu Mkuu wa AFP, Rashid Rai alisema "Uchaguzi ulikuwa na changamoto nyingi zilizosababishwa na Ukawa na CCM. Mvutano ulioibuka kati yao umeviathiri kwa kiasi kikubwa vyama vidogo."
Hata hivyo, Rai alisema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kitakachofanyika Januari 14, watajadili sababu za chama hicho kushindwa katika uchaguzi huo na namna ya kujipanga katika uchaguzi ujao.
Mwenyekiti wa Tadea, Lifa Chipaka alisema, "Sasa unaniuliza mimi matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, watafute Tamisemi watakupa matokeo."
Baadaye Chipaka alipiga simu katika chumba cha habari cha gazeti hili na kusisitiza kuwa Tadea kilisimamisha wagombea wengi mkoani Shinyanga, Tabora na Kigoma na kuibuka na ushindi.
Alipotakiwa kueleza idadi ya viti walivyoshinda katika mikoa hiyo alisisitiza kuwa wameshinda na alipobanwa zaidi alikata simu.
Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa ADC, Doni Myamani alipingana na matokeo ya Tamisemi akidai kuwa uchaguzi huo wameshinda vitongoji 19 na vijiji saba.
Doni alisema katika nafasi ya uenyekiti walishinda katika vitongoji vinane na vijiji viwili mkoani Dodoma; Mkoa wa Mara wamepata vitongoji tisa na vijiji vitatu; Mkoa wa Kigoma nafasi moja eneo la Mwandiga na katika Mkoa wa Lindi Wilaya ya Nachingwea kiti kimoja.
Doni alisema sehemu nyingine za Mtwara, Mara, Tanga, Simiyu na Kigoma na Kijiji cha Busega walishinda katika nafasi za wajumbe.
Imeandikwa na Habel Chidawali na Rachel Chibwete Dodoma na Fidelisi Butahe Dar es Salaam.