Matokeo ya kidato cha nne yanatoka lini ?

lobikoki loti

Member
Dec 5, 2014
70
95
Motokeo ya form 4 2014 lini?na pia wataripoti shule lini!? kwani kuna wanaotaka kusoma kozi ya kompyuta miezi mitatu ila sasa wanapata wasiwasi kama mda utaruhusu ,nawasilisha wakuu ;.
 

Mapya Yaja

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
560
500
Kuripoti shule ni mwezi wa saba mwakani, km ni computer akasome tu maana bado ana muda wa kutosha mtaani
 

Tobbo

Member
Jan 19, 2013
31
0
Wewe dogo umewahi kuona lini, mtihani umefanyika mwezi wa 11 halafu unaanza kuuliza matokeo mwezi wa 12? Tulia, subiri vipimo vya Dokta Msonde. Kama ni Komputa, nenda ukasome salama!
 

grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
Na utitiri wenu vishule vya kata kila siku bado mnataka wawasahihishie na kuwatangazia kwa muda uleule wa miaka ya sisi!! Hapo bado hamjawaumiza vichwa watu wa watu kwa mituhuma yenu ya udanganyifu kwenye vyumba vya mitihani.
Unadhani mpaka watangaze kumfutia mtu matokeo ni kazi ya siku moja?
Halafu mara nyingi wenye viherehere vya kutaka kujua passmark ni ngapi, mara mitaala hatupewi madarasani mara ooh matokeo yamecheleweshwa...huwa kichwani sifuri. Wenyewe waliopigilia misonge ya nguvu wapo kimyaa wanajiamini...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom