Matokeo ya kidato cha nne yanatisha

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,142
3,217
Wamefeli kweli kweli wenda kuliko mwaka jana, tembelea website ya necta au wizara.
 
Ajabu siku hizi mambo yako simple sana sio kama enzi zetu, tuition hazikuwepo, vitabu ndo usiseme!Siku hizi vitabu buku mbili mbili na watoto wanafeli namna hii, lol!
 
Wamefeli kweli kweli wenda kuliko mwaka jana, tembelea website ya necta au wizara.

Mkuu hawa vijana miaka ya hivi karibuni walizoea sana kuchakachua, hadi ikafikia waalimu wa tuition wanafundisha mitihani yenyewe. Mie naona pale baraza la mtihani wamebana kidogo na haya matokeo unayoona ndio viwango halisi vya elimu ya shule zetu. Hata wa miaka 2 hadi 3 iliyopita wangebanwa kidogo ungeyaona kama haya ya leo.

Sikumbuki kusikia paper yoyote kuvuja mwaka jana, labda tuwapongeze Baraza la Mtihani kwa kuongeza udhibiti na walimu wetu hawa wa Vodafasta wafanyekazi yao vizuri ndio viwango vitapanda.
 
Angalia shule ya feza girls alafu angalia aliyepata dv 4 peke yake ni mtoto wa nani
 
nimeangalia mkuu. anaitwa Mwana...JK. huenda ni majina tu. Kama kweli ni mwana wa mkuu wa nchi Nawapa Heko Necta na waliosahihisha. Hawakuangalia ni wa nani. Hata mkuu mwenyewe na familia yake nawapa heko hawakutoa Rushwa mtoto wao Apaishwe. Haki Bin Haki. NECTA wembe ni huo huo Pumba lazima zielee.
 
eti nani alaumiwe kwa kufeli huku....?
Wakati rais wetu anachukua uongozi hawa watoto walikuwa class five. Ni reflection ya utawala mbaya, uongozi mbaya wizarani sera duni na hafifu za chama tawala.

Miaka mitatu ijayo mtashangaa zaidi
 
Back
Top Bottom