Matokeo ya CVO Madagascar

Matokeo ya CVO Madagascar

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Posts
2,904
Reaction score
1,363
Nimeshangazwa na habari kuwa Madagascar inaoma msaada wa kupambana na corona wakati wana dawa. Nikafuatilia dawa yao iliyoletwa Tanzania kujua utafiti ulionyesha nini juu ya dawa hiyo - sikupata jibu

Ebu fuatilia habari hiyo Madagascar yaomba msaada wa kukabiliana na corona - BBC News Swahili

===

Wizara ya afya nchini Madagascar imetuma ombi la msaada wa dharura kwa mashirika na taaisi za Afya huku wagonjwa wa corona wakiongezeka.

Wizara ya Afya imesema kwamba ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni umesambaa kwa kiwango cha juu nchini Madagascar huku maeneo kadhaa yakirekodi milipuko hususan mji mkuu wa Antananrivo, kulingana na mtandao wa Actu Orange.

Kumekuwa na ripoti kwamba hospitali za umma nchini Madagascar zimejaa na zimekuwa zikiwalaza wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi.

Katika hospitali moja mjini Antananarivo, mkurugenzi anasema kwamba tayari wanatibu wagonjwa 46 na kwamba wana nafasi ya wagonja wanne zaidi.

Maafisa katika baadhi ya hospitali katika mji mkuu wa Antananarivo, wanadai kwamba hospitali zimejaa kutokana na kuongezeka maradufu kwa wagonjwa wa corona.

Mwakilishi wa WHO nchini Madagascar ameonya kwamba hospitali zimejaa hata kabla ya mlipuko huo kufikia kilele chake nchini humo.

Taifa hilo kwa sasa lina takriban wagonjwa 7000 wa Covid-19.

Rais Andry Rajaolina mapema mwezi huu aliweka masharti ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo kufuatia kuongezeka kwa maradhi hayo.

Mnamo mwezi Aprili, alizindua dawa ya mitishamba ya maradhi ya Covid-19 ambayo ilisambazwa nchini humo.

Mizigo kadhaa ya dawa hiyo ya Covid Organic pia ilitumwa kwa makumi ya mataifa barani Afrika.

Hatahivyo uwezo wa kinywaji hicho umepuuziliwa mbali na wataalam wa Afya nchin NIgeria na DR Congo mataifa ambayo yalifanyia majaribio dawa hiyo.

Katikati ya mwezi Julai rais wa taifa hilo alitangaza kwamba wabunge wawili wamefariki kutokana na virusi vya corona huku wabunge wengine 25 wakiambukizwa virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kilipothibitishwa katika kisiwa hicho mnamo mwezi Machi.

Rajoleina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo ambayo ilizinduliwa mwezi Aprili, licha ya onyo kutoka kwa shirika la Afya duniani kwamba haijaidhinishwa kutumika.

Ni kweli kwamba nimewasiliana na walioambukizwa . Nimeingia katika mahospitali yanayowatibu wagonjwa wa corona. Niko salama'', alisema.

Sina virusi vya corona hata kidogo. Sina dalili. Namshukuru Mungu. Nafuata maagizo niliojiwekea, lakini zaidi ya yote mimi na wapenzi wangu mke wangu na watoto wangu, tunakunywa na kufuata maagizo ya dawa yetu ya mitishamba''
 
Back
Top Bottom