Matokeo Kidato cha Nne 2016 yatoka, Feza Boys yaongoza!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,786
23,041
MATOKEO KIDATO CHA 4

Baraza la Mitihani nchini(NECTA) latangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2016. Wavulana wafaulu kwa 73.26% na Wasichana 67%.

- Feza, St. Francis na Kaizerege zaendelea kutamba kileleni, Dar yaburuza mkia.

Wanafunzi 277,283 (asilimia 70.09) waliofanya mtihani 2016 wafaulu.


7263769a-6c94-4751-8803-b0ea306abf17.jpg

Shule za Dar zaongoza washika mkia matokeo ya kidato cha Nne.

692f61dc-1bad-422f-b8cf-ef69706a7b01.jpg

Matokeo yote yapo hapa >> http://41.188.136.77:8080/matokeo/2016/csee/index.html
=====

Mada hii ilisomwa kwenye Jamii Leo ya JamiiForums; Kuona mada nyingine zilizosomwa angalia video hii hapa chini:-

 
Kwa sasa suala la Elimu ya Msingi na ile ya Upili imekuwa ni jukumu la sekta binafsi
Sekta binafsi ndio inajenga mazingira bora ya elimu na watoto kufanya vizuri kuliko serikali.

Lakini "Social Contract" kati ya wananchi na serikali kila baada ya miaka mitano ya kuomba kura huwa ni malipo ya elimu bora,afya bora na huduma bora za maji na maisha.

Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kutokufuata masharti haya ya "Social Contract" kati yake na wapiga kura.Kuwepo na ukosefu wa shule za serikali ktk kumi bora,ni moja ya uvunjwaji mkubwa wa "mkataba wa kijamii" kati ya serikali na wananchi.Na hapa Serikali inapswa kuadhibiwa.

Unawekaje kipimo sawa kati ya mwanafunzi anayesoma kwa kibatari na chemli kule Iselamagazi Tabora na yule anafanya study Tour Uturuki huku akiwa na mazingira bora ya kusoma?

Na hili kudhihirisha hivyo,kwa sasa huwezi kukuta viongozi wa serikali wakipeleka watoto wao ktk shule za serikali kwa maana na wao hawaamini ktk ubora wa elimu inayotolewa na shule za umma.

Ilboru,Tabora Boys,Mzumbe,Kibaha,Weruweru,Tabora Girls,Kilakala,Msalato na Korogwe Girls zimebaki magofu ya historia ya elimu bora ya Tanzania.Majengo ni toka ya mkoloni.Hakuna jitihada za kimkakati za kurudisha ubora.

Elimu imekuwa biashara badala ya Huduma.Na hao watunga sera wanaopaswa kuirudisha elimu ktk mstari mnyoofu ndio wafanyabishara wa elimu.Waziri anamiliki shule,mbunge anayeisimamia serikali naye anamiliki shule au kuwa na hisa ktk biashara ya elimu.

Katika nchi zilizoendelea,Elimu ya msingi na upili sio biashara,bali ni huduma.Ni huduma kwa sbb ni haki ya kimsingi ya kila mtu kupata elimu ya msingi na ya upili.Ndio maana nchi kama Sweden ni fahari kuwa sehemu ya shule ya serikali kuliko binafsi.

Mazingira ya kielimu ya mtoto aliyeko Kwa Msisi Handeni,ambapo zaidi ya kuwaza masomo,anawaza wapi atapata maji ya kuoga na kunywa si sawa na Marian Girls,ambapo mpaka pedi mtoto anaikutq kati vyoo vya shule,hawa hawawezi kuwa sawa kieleimu na kimtazamo.

Hii ni sawa na kuwaweka ulingoni Dula Mbabe anyecheza ngumi za amacha na Myweather
Its like feather weight boxer vs heavyweight boxer!!Kwa hili tujitathmini upya
 
Back
Top Bottom