Maticha wana wakati mgumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maticha wana wakati mgumu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Scofield, Jan 18, 2012.

 1. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Walimu wazidi kusotea Mishahara ya Desemba [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Hamisi Mwesi, Dodoma
  WALIMU ambao majina yao hayakuonekana katika uhakiki wa watumishi Manispaa ya Dodoma, wametakiwa kupeleka vielelezo vyao ofisi ya utumishi kwenye manispaa hiyo ili vihakikiwe kwa ajili ya kulipwa mshahara wao wa Desemba mwaka jana.

  Hatua hiyo inatokana na usumbufu na unyanyasaji waliopata walimu hao wakifuatilia mishahara yao baada ya kuzuiwa na manispaa hiyo kufuatia uhakiki unaoendelea nchini, kubaini watumishi hewa na majina ya baadhi ya walimu hayakuonekana.

  Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Nicolaus Buretta, alisema walimu wote ambao hawakupata mishahara wapeleke vielelezo vinavyoonyesha utumishi wao ili waweze kulipwa mishahara yao.

  Buretta alisema iwapo kama walihama kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali, wapeleke vielelezo vyote mpaka vya uhamisho vihakikiwe kwa ajili ya kupitisha mishahara yao kwa sababu fedha zao zipo.

  “Iwapo mwalimu ana vielelezo vyote alete ofisi ya utumishi ya manispaa ili vihakikiwe, tayari kwa kupitisha mishahara yao hakuna tatizo,” alisema Buretta.

  Alisema hadi sasa hawajajua majina ya watumishi hewa na kwamba, uhakiki huo unaendelea mpaka utakapomalizika.
  Pia, Buretta alisema wanatarajia kufanya uhakiki mwingine wa hesabu kuanzia Februari mwaka huu kwa watumishi waliohakikiwa awamu ya kwanza.

  Kuhusu usumbufu wanaopata walimu hao kufuatilia mishahara yao, Buretta alisema amesikitishwa na kitendo hicho kwani siyo uungwana na kwamba, kama walimu hao wangetoa taarifa kwake na kutaja wahusika angechukua hatua za kisheria.

  “Nasikitika kusikia mtumishi anayefuatilia haki yake anapewa maneno machafu, iwapo huyo mwalimu aliyefanyiwa hivyo angetoa ushirikiano na kumtaja mfanyakazi huyo wa manispaa aliyefanya hivyo, ningemchukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo,” alisema Buretta.
  Mwananchi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Hivi tujiulize hii serikali kwa nini inawanyanyasa waalimu kiasi hiki, wanataka waishi maisha gani?
  Hivi mwalim akiwa darasani atafundisha kwa morali kweli ili hali hajalipwa mshahara wake


  TAFAKARI, CHUKUA, HATUA.
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Walimu na wao nadhani bado hawajajitambua kwani wangekuwa wamejitambua wasimgekuwa wakiomba haki zao bali wangezitafuta kwa means yoyote mfano mzuri wajifunze kwa wenzao kenya kwa umoja waliokuwa nao ambao kwa pamoja waliamua kugoma, kama na wao siku zote wanatangaza kugoma na kuahairisha ungekuta matatizo yao yashatatuliwa siku nyingi labda niwakumbushe tu kwa methali ama nahau walizotufundisha kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kwahiyo inaonyesha wao hawana umoja ndo maana tatizo lao limezidi kuwa endelevu
   
 3. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni viongozi wao ndio wanawayumbisha hawana msimamo JK kashawanunua.
   
Loading...