MATIBABU YA MWISHONI(Palliative Care)

MATIBABU YA MWISHONI(Palliative Care)

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
MATIBABU YA MWISHONI(PALLIATIVE CARE)

Ameandika rafiki yangu Dr. Justin Banyukwa.

Matibabu ya mwisho yaani palliative care, hii ni aina ya matibabu apewayo mgonjwa ambae ana ugonjwa wa mda mrefu yaani "chronic illiness" . Mfano magonjwa ya figo, kisukari, HIV/AIDS , saratani na magonjwa ya mfumo wa fahamu kama vile "stroke."

Matibabu haya hutolewa kwa malengo ya kumuondolea mgonjwa maumivu ya mwili, maumivu ya kisaikolojia na pia humpa mgonjwa msaada wa kiroho kutokana na imani yake ya kidini.

Lakini pia humuandaa mgonjwa kukabiliana na umauti utakaotokana na ugonjwa husika na hivyo humfanya mgonjwa afariki katika hali isiyo ya kuweweseka. Ni kipindi hiki mgonjwa huitaji vitu mbali mbali kama vile kuongozwa sala ya toba, au kuonana na watoto wake au jamaa na marafiki zake. Ni wajibu wa wahudumu wa afya kwa kushirikiana na ndugu wa mgonjwa kutimiza mambo hayo ili kumfariji katika safari yake ya mwisho hapa duniani.

Pia ni kipindi hiki ambapo ndugu na jamaa wa mgonjwa huandaliwa kisaikolojia kuwa matumaini ya mgonjwa wao kupona hayapo na hivyo kujiandaa na hali ya kuondokewa na ndugu yao.

kipindi hiki kwa ufupi huambatana na masuala ya kiimani na sala mbalimbali na kuwatia moyo ndugu wanao uguza na mgonjwa pia.

Naomba kusisitiza kuwa matibabu haya hutolewa kwa wagonjwa wale tu ambao ugonjwa wao umefikia mwishoni katika hatua isiyo tibika (End stage of disease)

Mwisho nitoe pole na niwaombee wote wanao pitia kipindi hiki mahospitalini.
 
Mungu atulinde na atuepushe na maradhi yote mabaya ila siyo kwa mapenzi yetu ila mapenzi yake yatimizwe.

Pia awahurumie na awapunguzie maumivu wale wote wanaoteseka kwa maradhi mabaya.umenikumbusha rafiki Hamis Milyomi ambaye ana wiki mbili figo zilimuuwa.

Dunia haina raha hata kidogo sisi tulio hai tunapata tabu sana tutubu kwa kwa Mungu imani zetu atuepushe na haya maafa.
 
Back
Top Bottom