Matibabu ya hiatal hernia na acid reflux

mangonifera indica

JF-Expert Member
Dec 2, 2017
845
1,462
Habari za wakati huu wakuu,

Naomba kujua matibabu ya henia ya kifua na gharama zake kwa ujumla. Na dawa nzuri ya kusaidia acid reflux tumboni...
 
Habari za wakati huu wakuu
Naomba kujua matibabu ya henia ya kifua na gharama zake kwa ujumla
Na dawa nzuri ya kusaidia acid reflux tumboni...
Nahisi kama nipo nyuma ya kamera vilee mm kwa ufahamu wangu mdogo henia ni ngili ambayo huwasumbua wanaume weengi ni huu ugonjwa hutokwa ktk korodan mara nyingi moja au zito husumvuliwa na mshipa Fulani ambao dawa yake ni upasuahi na hugonjwa huu husumbua sana wakati WA baridi hufanya mtu awe na maumidu makaliii ktk korodani hapo mm ndio uwelewa wangu ulipoishia
 
Mkuu nenda hospital kubwa za serikali hizi za wilaya... Dawa ya acid reflux ni Omprazol... Na kupunguza vyakula vyenye uchachu uchachu na gesi ikiwezekana katika mboga yako usitumie nyanya kabisaa iwe chukuchuku hadi hali itakavyokaa sawa... Mimi nilipataga acid reflux kali sanaa... Ilinibidi niwe nakula vyakula chukuchuku tu huku nikisindikiza na omprazol
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Lakini nayo imegawanyika katika namna nyingi, kama ifautavyo:

Sliding type; Hiyo ni aina ya ngiri inayotokea wakati sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa esophagus hiatus kama matokeo ya ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo na hurudi katika hali yake ya kawaida wakati presha inapopungua.

Fixing type; Inatajwa kuwa Ngiri Kifua, ambayo hutokea wakati sehemu ya juu ya utumbo Sukuma kwenda kwenye diaphgram and kukaa hapo na hupelekea matatizo ya mzunguko wa damu tumboni.

DALILI ZAKE

Kwa kawaida, aina hiyo haijionyeshi dalili zozote, hadi mpaka pale ugonjwa umeshajijenga sana. Baadhi ya dalili zake inapokuwa imekomaa sana, ni pamoja na maumivu kifuani, vichomi vikali wakati wa kuinama au kulalia mgongo. (Heartburn, Regurgitation of food or liquids into the mouth, Backflow of stomach acid into the esophagus (acid reflux), Difficulty swallowing, Chest or abdominal pain, Shortness of breath, Vomiting of blood or passing of black stools, which may indicate gastrointestinal bleeding)

MATIBABU

Vipimo vyake ni Barium X-ray na Endoscopy hivi vipimo husadia daktari kujua ngiri imeathiri kiasi gani kwa upande wa utmbo na diaphragm.

Matibabu ya ngiri ni kupasuliwa, haishauriwi kufungia sarafu kwani inaweza kukosewa na kusababisha sehemu ya utumbo kubanwa au kuleta maambukizi ya ngozi kwenye kitovu. Kwa mtoto huisha yenyewe taratibu na ikibidi hupasuliwa baada ya umri wa miaka mitatu.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa.

Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni).

Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

DAWA ZA MATIBABU

Maji ya vuguvugu asubuhi; Mtu anatakiwa kunywa maji ya vuguvugu ama glasi moja au mbili, mara baada ya kuamka na kisha asimame na kufanya mazoezi ya kunyanyua mikono juu na kuirudisha chini mpaka maeneo ya kifua kwa dakika 10 hivi na uendelee na shughuli zako.

Ni litendo kitakachouwezesha utumbo wa mhusika ushindwe kupanda juu ya kifua kuleta ngiri. Mtu akikosa maji ya vuguvugu, anaweza kutumia maji ya joto la kawaida, bali yasiwe baridi.

Jambo hilo linaweza kufanyika hata kama haumwi ngiri au ugonjwa wowote. Ni muhimu pia kuepuka vitu kama kahawa, chai ya rangi, juisi za dukani na maji ya baridi, wakati wote.

Siki ya tufaa (apple cider vinegar); Siki ya tufaa ina msaada mkubwa katika kupunguza dalili za kiungulia na asidi iliyozidi mwilini kama matokeo ya ngiri ya kifua. Ingawa siki ya tufaa kwa asili ni tindikali, inapokuwa ndani ya tumbo hubadilika na kuwa alkalini. Mtu aongeze kijiko kidogo kimoja au viwili vya siki ya tufaa katika glasi moja ya maji ya vuguvuguna akinywa kwa dakika 20 kabla ya chakula cha mchana na jioni. Afanye hivyo, kila anapojihisi ana kiungulia au tindikali iliyozidi mwilini.

Mdalasini; Hicho ni kiungo maarufu duniani na kinachosaidia kutuliza na kusafisha tumbo. Mdalasini inaweza kuondoa maumivu yasiyo ya kawaida tumboni, mara tu baada ya mlo. Ina kawaida ya kufanya kazi kama dawa ya asili, kuondoa tIndikali iliyozidi mwilini. Namna ya kutumia ni kuongeza kijiko kidogo kimoja cha unga wa mdalasini kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto.

Hatua inayofuata, ni kuuacha mchanganyiko huo kwa wastani wa ama dakika mbili au tatu na kisha ukorogwe kwa ajili ya kunywewa yote. Mtu anatakiwa kufanya hivyo kutwa mara mbili; asubuhi na jioni. Kwa kuongezea mtu anaweza kuchanganya mdalasini kwenye vyakula vingi unavyopika kama sehemu ya kinga.

Unga wa kuokea mikate; Ni ile kinamama wanaitumia wakati wanapika maandazi. Hujulikana pia, kama ‘bicarbonate of soda. ’Ni dawa ya asili ya kuondoa tindikali mwilini na inaweza kuondoa kiungulia na maumivu ya ngiri ya kifua kwa haraka.

Changanya nusu kijiko kidogo cha chai cha unga wa kuokea mikate kwenye glasi moja ya maji na unywe papo hapo, kisha ulirudie hilo kutwa mara tatu. Haishauriwi dawa hii kutumika kwa mtu mwenye shinikizo la juu la damu.

Aloevera (mshubiri); Aloevera au mshubiri ni moja ya dawa nzuri zaidi za asili kwa matatizo mbalimbali ya tumbo yanayosababishwa na ngiri ya kifua. Huzisafisha kuta za ndani ya tumbo na kuziwekea ulinzi, zikiondoa maumivu yote ya tumbo, zikidhibiti kiungulia kirahisi.

Namna ya kutumia, ni kunywa robo kikombe cha juisi ya aloevera dakika 20 kabla ya kula chakula cha mchana au jioni na unaweza kuchanganya na juisi ya embe au parachichi, kuifanya kikombe kizima. Hiyo inafanyika kupunguza ukali wa dawa, wakati unakunywa.

Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli (maji maji) ya aloevera unapoandaa hii juisi yako, la sivyo unaweza kupatwa na ugonjwa wa kuharisha.

Badili chakula unachokula: Wakati unaumwa ugonjwa wa ngiri ya kifua, ni mhimu kuwa makini na kile unachokula kila siku. Epuka vyakula vinavyoweza kulizidisha zaidi tatizo. Pia, kuna ushauri wa kudhibiti uzito wako, epuka vyakula kama chokleti, kahawa, chai ya rangi, kitunguu maji, kitunguu swaumu, vyakula vyenye viungo vingi (spicy), machungwa na limau.

Lingine unaloaswa kula mboga za majani na matunda, kula mafuta safi kama vile mafuta ya zeituni, kula sana mbegu mbegu kama mbegu za maboga na korosho. Kula vyakula ambavyo havijakobolewa.

Mambo muhimu ya kuzingatia, ni kula milo au chakula kidogo mara nyingi kila siku;

Kula chakula cha usiku kwa saa mbili au tatu, kabla ya kwenda kulala

Mambo yanayosababisha kuugua ngiri:

  • Uvutaji sigara.
  • Uzito uliopitiliza.
  • Matumizi ya dawa za kulevya.
  • Msongo wa mawazo.
  • Mtatizo ya kurithi.
  • Kunyanyua vitu vizito.
  • Kuinama kwa muda mrefu.
  • Kukohoa kwa muda mrefu
  • Ujauzito.
Habari za wakati huu wakuu
Naomba kujua matibabu ya henia ya kifua na gharama zake kwa ujumla
Na dawa nzuri ya kusaidia acid reflux tumboni...
 
Ahsanteni woote, nimeamua Jumatatu kwenda hospitali maana kiungulia kimekuwa kikali mno hasa nikilala... Pia chakula hakishuki tumboni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom