Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 130
Habari zenu wannajamvi..naomba kuuliza juu ya hawa wakorea wenye kituo cha seragem..je? zile mashine zao zinasaidia?. Yoyote mwenye uthibitisho wa kuona aje hapa anihakikishie..
Nina binti yangu ana 1.8 year.. alipata homa ya uti wa mgongo kwahiyo ikimsababishia celebral palsy. so mpaka sasa hawezi kukaa, shingo haijakaza, hawezi kushika kitu chochote..huwa nampeleka kwenye physiotherapy muhimbili na CCBRT. Improvement ipo kwa mbali namimi sijakata tamaa bado naamini ata improve.
Sasa nimesikia kuwa hawa seragem wana mashine nzuri zinazotibu kupitia uti wa mgongo kwa hivyo mnijuze kwa wale mliowahi kuona kwa macho kwa jirani. ndugu, jamaa, rafiki ama wewe mwenyewe..
Nyingine imefunguliwa Ubungo, nyuma ya stand ta mkoa. Hata mie nina mashaka nayo. Ukihoji kuhusu ule umeme wanaochomewa unaambiwa ni miale ya jua na si mionzi. Nashindwa kuelewa kabisa.
Ukianza matibabu haya siku za mwanzo ni lazima uumwe sana. Unatakiwa kuchomwa kila siku mara tatu kwa mwezi mzima mfululizo, then unaweza ukawa unachomwa kila baada ya siku moja. Umeme, mashine, huduma vyote vinatolewa bureeeee!
Uliwahi kuuziwa karanga na wale wachuzi wa kikapu mkononi? Yani anachota kama punje tano hivi za karanga anakuonjesha, ukishanogewa tu lazima ununue, sasa ndio modus operandi ya Ceragem ukianza matibabu ni muonjo, baadae unauziwa mashine ukajitibie mwenyewe. Sawa Koku?Mmh! Kwa nini bure? Running cost anafaidi li nani?
Mwanahisa, si wangetanganza wanauza mashine? Safari za mwezi mzima kwa mtu aliyepooza ndio nini?Uliwahi kuuziwa karanga na wale wachuzi wa kikapu mkononi? Yani anachota kama punje tano hivi za karanga anakuonjesha, ukishanogewa tu lazima ununue, sasa ndio modus operandi ya Ceragem ukianza matibabu ni muonjo, baadae unauziwa mashine ukajitibie mwenyewe. Sawa Koku?
Nafikiri wanawafanyisha watu mazoezi yakuamka asubuhi na mapema bila wao kujua kua ile nafuu wanayopata inatokana na ule mchaka mchaka wa asubuhi. Ila mashine ndio core business hizi nyingine mbwe mbwe tu.Mwanahisa, si wangetanganza wanauza mashine? Safari za mwezi mzima kwa mtu aliyepooza ndio nini?
hebu fuata huu uzi mkuu Benice https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/190671-matibabu-ya-ceragem-tanzania.htmlJamani inamaana hakuna anaewajua hawa? Nilitegemea kupata majibu mazuri humu ndani