Hii story inaweza kuonekana ya kuhuzunisha sana, but mnaokumbuka hii imeshatoka kwenye magazeti siku nyingi kidogo. Nimepata kuongea na diplomat mmoja na alichosema ni kuwa kwa kawaida hawa ma-housegirls wanaotolewa bongo huwa inakuwa hivi: ili apate viza lazima awe na mkataba unaoeleweka,yaani unakidhi sheria za nchi unayoenda. Sasa kwa kuwa diplomats hawezi kumudu kuajiri housegirl huko ughaibuini, anatafuta mbongo na wanamtengenezea mkataba ili viza ipatikane. Sasa the tricky part ni kuwa wako wanawake wa mataifa ya west Africa na hata kenya, ambao 'huwafumbua macho' hao ma HG wa kibongo na kuwashawishi waende kushitaki...ukitazama hakuna HG hapa Bongo anayelipwa 900USD hata wanaofanya kwenye nyumba za madiplomata masaki, Obay nk..halafu ni jambo la kawaida kwa HG hapa bongo kufanya kazi zaidi ya masaa 12, wanaamka saa 12 asubuhi na kulala saa nne usiku. Sio kawaida HG kuwa anapewa likizo na day off; hii inaonyesha kile nilichoandika hapo juu kuwa mikataba hii purpose yake ni kupata viza. Huyo mwanamke kwa kuripoti suala hilo anajua anapata faida zifuatazo 1)Amnesty, hivyo ataishi marekani kimoja 2) Chance kubwa ya kuvuna kitita cha hela ya kufa mtu!. Kwa hiyo tunapojadili nadhani hoja sio kuteswa Marekani, Ma HG wote wanateseka popote pale tanzania humu humu! Hivyo labda tmjadala uwe je hakiza wafanyakazi kama hawa iko wapi???