Mateso haya mpaka lini?

Yapaswe

JF-Expert Member
Oct 19, 2016
322
240
Wanabodi nawasalimu kila mmoja kutokana na umri wake,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 nilizaliwa nikiwa mzima bila ulemavu wowote mpaka naingia kidato cha nne ndipo nikapata tatizo la kutosikia vizuri,tatizo hili limenitesa sana mpaka leo nimeishi maisha ya chuo kwa shida sana hasa kipindi cha darasani mpaka nikae mbele ndo nasikia,lakini kwa uaminifu wa Mungu nilimaliza chuo bila tatizo wala suprimentary yoyote ile! Nimetumia dawa za kila aina hasa dawa asili,nimetibiwa hospital ya rufaa morogoro mpaka na ear syringe bila mafanikio yoyote yale,Wameniandikia rufaa kwenda Muhimbili ili nikapewe kitu kinaitwa earphone lakini kuna doctor ameniambia kuwa pia hicho kifaa kinamadhara,!
Kuhusu ulemevu ni kwamba nasikia mda wote vitu vinaunguruma maskioni hivyo mtu akiongea nashindwa kuyanasa Maneno husika!
Ndugu kaka na dada ningependa kupata msaada wa mawazo kutoka kwenu na Mungu awabariki!
 
What is Tinnitus?
Tinnitus is described as any sensation of sound in the absence of any external stimulation. It is often described as a ringing, buzzing or pulsing sensation in the ears. Tinnitus is thought to be caused by damage to the outer, middle or inner ear or the hearing nerve in the brain. The damage to the hearing system can result from a number of different sources, such as; noise exposure, age-related changes in the inner ear, certain medications, head injuries, wax, etc. If you experience ongoing tinnitus contact our clinic to schedule an appointment for a complete audiological assessment. Be sure to indicate that you are booking the test because of your tinnitus.
 
Daah aisee pole sana mkuu....Fanya utaratibu wa kwenda India kama itawezekana
 
What is Tinnitus?
Tinnitus is described as any sensation of sound in the absence of any external stimulation. It is often described as a ringing, buzzing or pulsing sensation in the ears. Tinnitus is thought to be caused by damage to the outer, middle or inner ear or the hearing nerve in the brain. The damage to the hearing system can result from a number of different sources, such as; noise exposure, age-related changes in the inner ear, certain medications, head injuries, wax, etc. If you experience ongoing tinnitus contact our clinic to schedule an appointment for a complete audiological assessment. Be sure to indicate that you are booking the test because of your tinnitus.
Wapi mlipo ndg niwatembelee?
 
Wanabodi nawasalimu kila mmoja kutokana na umri wake,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 nilizaliwa nikiwa mzima bila ulemavu wowote mpaka naingia kidato cha nne ndipo nikapata tatizo la kutosikia vizuri,tatizo hili limenitesa sana mpaka leo nimeishi maisha ya chuo kwa shida sana hasa kipindi cha darasani mpaka nikae mbele ndo nasikia,lakini kwa uaminifu wa Mungu nilimaliza chuo bila tatizo wala suprimentary yoyote ile! Nimetumia dawa za kila aina hasa dawa asili,nimetibiwa hospital ya rufaa morogoro mpaka na ear syringe bila mafanikio yoyote yale,Wameniandikia rufaa kwenda Muhimbili ili nikapewe kitu kinaitwa earphone lakini kuna doctor ameniambia kuwa pia hicho kifaa kinamadhara,!
Kuhusu ulemevu ni kwamba nasikia mda wote vitu vinaunguruma maskioni hivyo mtu akiongea nashindwa kuyanasa Maneno husika!
Ndugu kaka na dada ningependa kupata msaada wa mawazo kutoka kwenu na Mungu awabariki!
Huugui mafua mara kwa mara?
 
Ndugu kaka na dada ningependa kupata msaada wa mawazo kutoka kwenu na Mungu awabariki!
Pole sana mkuu. Nenda pale kwenye hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani, Dar Es Salaam wakufanyie uchunguzi. Wanaweza pia wakakusaidia upate usikivu mzuri kama hapo zamani...
 
Hapana siugui mafua mara kwa mara! Ila napata maumivu ya Kichwa mara kwa mara,
Nilidhani tatizo linafanana na alilowahi kuwa nalo mwanangu,yeye alikua anapata mafua mara kwa mara ghafla uwezo wa kusikia ukawa unafifia Doc kumchunguza akasema ni maji yameingia kwenye ngoma ya sikio,ambayo yamesababishwa na huo unyevu wa masikio,hivyo ili kutibu tatizo la masikio tukomeshe mafua kwanza,tukapima allergy ikagundulika ni vumbi na majani,tukamuweka mbali na hali hiyo akapona mafua,akatupa dawa ya kukausha hayi maji masikioni kweli uwezo wake wa kusikia ukarejea kabisa!hadi leo amepona kabisa.Sasa yako ni different case!
 
Nashukuru sana kwa msaada wako! Nilishauliwa niende muhimbili ndo wanapima kwa hospital ya morogoro walishindwa maana sikio haliumi wala kutoka uchafu wowote hivyo wakasema inahitajika uchunguzi zaidi,ningependa kujua huyo docta kama yupo mikoa ya karibu nimtafute
 
Tafuta specialist yeyote wa ENT atakusaidia,mie huyu yuko Mwanza anaitwa Doc Buname,ila pia kuwa makini sana,maana mie kwa mtoto nilionana na maspecialist wawili kila mmoja majibu yake yakawa yanakinzana na mwenzie,nikajaribu kureason mwenyewe nkaamua kustick na mmoja ambaye alimponyesha wakati mwenzake alidai mtoto afanyiwe upasuaji wa koo!!
 
Dah! Asante sana, Mungu akubariki ndg!
 
Pole xana kijana. Kuna daktar wa magonjwa yote hata yaliyoshindika. Naye ni YESU KRISTO.Mtumainie yeye ktk kila jambo hakika utaona ukuu wake.
Nikweli kaka siku zote naamini yupo yeye Mungu atangazae mwisho tangu mwanzo kwake nitasimama daima! Asante
 
Yes. Jambo la msingi ni kwamba unapaswa kuwa na bidii ya kuomba. (psalm 50:15, then call on me when you are in trouble, and i will rescue you, and you will give me glory). Pia jifunze kuisemesha nafsi yako juu ya hilo tatzo lako (psalm 42:11, the scripture say; why am i discouraged? Why is my heart so sad? I will put my hope in God! I will praise him again my savior and my God!
 
Wanabodi nawasalimu kila mmoja kutokana na umri wake,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 nilizaliwa nikiwa mzima bila ulemavu wowote mpaka naingia kidato cha nne ndipo nikapata tatizo la kutosikia vizuri,tatizo hili limenitesa sana mpaka leo nimeishi maisha ya chuo kwa shida sana hasa kipindi cha darasani mpaka nikae mbele ndo nasikia,lakini kwa uaminifu wa Mungu nilimaliza chuo bila tatizo wala suprimentary yoyote ile! Nimetumia dawa za kila aina hasa dawa asili,nimetibiwa hospital ya rufaa morogoro mpaka na ear syringe bila mafanikio yoyote yale,Wameniandikia rufaa kwenda Muhimbili ili nikapewe kitu kinaitwa earphone lakini kuna doctor ameniambia kuwa pia hicho kifaa kinamadhara,!
Kuhusu ulemevu ni kwamba nasikia mda wote vitu vinaunguruma maskioni hivyo mtu akiongea nashindwa kuyanasa Maneno husika!
Ndugu kaka na dada ningependa kupata msaada wa mawazo kutoka kwenu na Mungu awabariki!
Helo mkuu pole sana una ugonjwa wa tinnitus unasikio sauti ya Muungurumo kama vile kengele au mvumo fulani wa sauti. Mimi ninayo dawa yake ukihitaji nitafute kwa wakati wako.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.

Similar Discussions

Back
Top Bottom