Matatizo yasiyosemwa katika Industry ya ajira na Taasisi za elimu Tz

mwanaNjilo

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
277
195
Leo nilikua napita-pita kwenye site moja ya ajira (Ntahifadhi jina la site)...nikakutana na job vacancy ya Senior Transport Officer ilitangazwa na Jhpiego (Tz)!

Kabla cjaendelea na hi thread, naomba niseme maoni yangu juu ya taaluma hii ya Transport management japo kwa muhtasari, mana hii ni taaluma yangu...I majored in Logistics and Transport Management.

Transport Mgt, ni miongoni mwa courses za social science. Ni set moja na watu wa Procurement, Education, uchumi, BA...taja wengine!
Hawa ni watu wa operations! Transport officer(TO), Procurement officer, etc ni watu wa operations. Sio watu technical katka kampuni. TO sio Technician wa magari. TO sio technician wa umeme! (Tofaut ya Techinical staff wa kampuni na operational staff wa kampuni!)

Naendelea...
Ni kwanini mwajir anahitaji mtu wa operations katka kampuni yake kwa vigezo vya technical staff??! Au kwann mwajiri avifanye vigezo vya technical staff kua kipaumbele cha kumwajiri mtu wa operation (mwenye nafac yake!) na kufanya qualifications za mtu wa operations kua ni additional qualification?? (nimeeleweka??)
...kama cjaeleweka, naomba nafac nyingine hapa ya kujielezea...
Pale National Institute of Transport (NIT) kuna kozi inayozalisha transport officers...a complete course!! Mtu aliesoma vzur koz hii akawa competent kwenye soko la ajira, anakua Transport officer! Kwenye hii koz hawafundishwi mambo ya mechanics au automobile, unafundishwa operational aspects za magari (na fleet). Sasa kwanini mwajiri atangaze kazi ya u-TO huku qualifications zilizopewa kipaumbele cyo 'Core' katika taaluma hyo?!...core subjects za Tansport management hazisomw na watu wa automobile/mechanics, as a matter of fact, transport mgt ni social science, while mechanics/automobile ni 'Hard' science km medicine and other majors!

Mimi naona tatizo lipo kwenye Departments za Research & Developments (R&D) za taasis zetu za elimu na mamlaka zake (hapa nazungumzia...NACTE na TCU pamoja na colleges na uni!) mana hawa ndo hua wanaona demands za soko la ajira, na kubuni kozi zitakazoendana na mahitaji ya soko, sasa kwanini kunakua na mwingiliano wa kimaslahi baina ya taaluma mbili tofaut?? Au ni kwann wanashindwa ku update mtaala wa either Transport mgt au Automobile ili mmoja aweze kukidhi vgezo vya soko la ajira?? Kuliko kumfanya mtu wa transport kudhani kua yupo unfit kwny taaluma yake bila kua na basic techical knowledge ya magar!

Au shida nyingine ni uhuru wa industry yetu ya ajira. Uhuru huu unawapa mamlaka waajir kuamua ni watu gani wanahitajika kweny kaz zao, na siyo taaluma mahsusi zitolewazo vyuoni kukidh hitaj la nafasi zao za kaz...
Screenshot_20181228-155620.jpeg
Screenshot_20181228-155500.jpeg
Screenshot_20181228-155549.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom