Matatizo ya Uongozi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya Uongozi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by donasheri, Apr 24, 2012.

 1. d

  donasheri Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Matukio mengi serikalini yanadhihirisha waziwazi udhaifu mkubwa wa uongozi wa JK. Nitajaribu kuelezea kidogo:
  Kwanza uongozi wa nchi ni kama kitambaa cheupe ukutani. Wananchi wanakiangalia wakati wote ili kuwa na imani nacho. Kinapokuwa cheupe wakati wote wananchi huwa na imani kubwa nacho.

  Lakini kitambaa kikijaa madoa meusi kila mahali imani hiyo huondoka kabisa. Ndivyo ilivyo kwenye uongozi wa JK. Alitakiwa kukisafisha kila mara ili kuondoa madoa yanayoingia.

  Pili kiongozi mkuu ana vyombo vyake vingi vinavyomsaidia kazi. Taarifa za wasaidizi wake kama hazitumii ipasavyo unatarajia nini? Kama anazidharau taarifa hizo ajue kuwa hata wale wanaomsaidia kumpelekea hizo taarifa hawatafanya hivyo kwa uaminifu na ufanisi mkubwa. Kwa kutozifanyia kazi huzaa majanga ndani ya mfumo wake.

  Nadhani hali ndiyo hiyo. Kiongozi msikivu huvuna mazuri mengi kutoka kwa wasaidizi wake. Matokeo yake ni ubora wa uongozi wake. Lakini sivyo hivyo kwa JK.

  Tatu kiongozi yeyote anayetuhumiwa anapoteza heshima yake mbele ya umma. Mponda hana sifa na heshima hadharani. Nkya pia. Na wale wote wanaotuhumiwa. JK anapowalazimisha waendelee na nyadhifa zao anawapa shida kubwa mbele ya umma.

  Nne JK ni kitambaa cheupe kilichojaa madoa meusi hata kama yeye ni mtu msafi. La yeye kuwa usafi au mchafu mimi sijui. Kutokana na kitambaa chake kuwa na madoa meusi heshima yake mbele ya umma imepotea. Sasa kazi iliyopo ni kukifanyia usafi wa hali ya juu. Hii ni kazi kubwa sana. Kwa nini tumefika hapo? Kwa sababu ya mwanzo mbaya.
  Tano ili kujiweka sawa inafaa tuangalie hivi. Kwa mfano mtu unaingia ofisini mwako. Pengine umetoka safari. Unakuta meza yako imejaa makabrusha mengi yanayohitaji attention yako wewe mwenyewe. Hali hii inaweza kukuchanganya kabisa. Bali unahitaji kutulia. Tumia hata wasaidizi wako. Pango kila kabrusha kulingana na umuhimu wake. Ndipo sasa anza kulitendea kazi kabrusha moja moja. Kwa hakika utamaliza hata kama itakuchukua muda mrefu.
  Tulipofikia ni pagumu mno. Kwa sababu tunavna kile tulichokipanda. Gabbage in gabbage out!
  Ndugu zangu wana JF nimeliangalia hili kiuongozi na si vinginevyo.
   
Loading...