Matatizo ya Umeme yataisha lini Tanzania?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,110
Wakuu nawaulizeni je Nchi yetu itakuwa na hayo matatizo ya umeme mpaka lini? mimi nipo ughaibuni nazungumza kwenye chat sasa hivi chat ya yahoo na mwanangu yupo mjini

Tanga ananiambia baba huku umeme hakuna natumia charge iliyopo ndani ya Betri yangu ya laptop wakati wowote ule kuanzia sasa itakwisha nashangaa kusikia tatizo la umeme bado

lipo haswa Mijini? Na nilivyo muuliza umeme umekatika Tangu saa ngapi ananijibu Mwanangu ananiambia baba tangu saa tano usiku nimezidi kushangaa mpaka hii sasa saa saba usiku kwa

huko kwenu huku kwangu ni saa sita usiku bado umeme haujarudi Jamani kulikoni huko kwetu Tanzania kuna Viongozi wa kweli jamani?Au Uchakachuaji umekuwa mwingi hata

kwenye matatizo ya umeme? Tatizo la Umeme mimi ninakumbuka tangu mwaka 1992 nilipoondoka hapo Tanzania bado lipo jamani mpaka leo? Hiyo Nchi kweli imeoza jamani.

Huku nilipo umeme hata kama utakatika hauwezi kuchukuwa zaidi ya dakika 20 utarudi tena mtaombwa samahani katika Redio na TV lakini huku kwetu Tanzania ni matatizo tu

kila siku. Nawaombeni munifahamishe kuhusu umeme wa Jua gharama zake ili niweze kutatuwa matatizo ya umeme kwa mwanangu asanteni kwa ushauri wenu.
 
Back
Top Bottom