Mlalahoi,
Mi naona we ndo umemiss point yangu ambayo ni kuwa habari ya mwanzo kama ilivyotolewa na Daily News inaungwa mkono pia na THISDAY! Sina shaka na THISDAY na nawajua waandishi kadhaa wanaofanya hapo, pamoja na Mhariri wao ambaye aliwahi kuwa Afisa wa juu pale Maelezo.
Ninachosema ni kuwa tuwafuatilie kina Richmond na hao Songas wao ambao mitambo inaharibika kila siku!
By the way, mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa hao jamaa waliotaka kujenga bomba la mafuta, alikuwa akiitwa Athumani Mfutakamba(?), si ndiye huyo huyo aliyegombea ubunge wa Afrika Mashariki akakosa, na pia alichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM (2005), akachujwa? Je, ndiye huyo sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo huko Iringa? Wazee leteni data!