upo sawa kabsa hamna kuongopa hapa!nimeona mifano ya watu weng ambao yamewashnda..haswaa kwenye foreverWadau wa Forever, Tianshi, GNLD, SwissGuard, n.k. Mnasemaje au ninaongopa ?
Kweli mkuu usemayo, elimu / ufahamu kwa kila unachokifanya ni muhimu.., sasa jukumu la kuwaelewesha hao watu si wale wanaofanya kazi hii tayari ? Sasa badala ya watu kusema ukweli na ugumu wa kazi wanapowapa watu false hope kwanza ni rahisi tu na kila mtu anaweza kufanya (hata wale wasiopenda kuuza) huoni kwamba wanaongeza tatizo badala ya kutibu tatizo ? Sababu ni kwamba kinachotokea mamia ya watu wanajiunga na mamia ya watu wanaondoka kila siku.Keysersoze umeelezea vizuri, kwa upande wangu nitasema hayo yote yanatokea kwa sababu moja kubwa ukosefu wa elimu ya biashara kwa wafanyao biashara na wale wapya.
Watu wakijifunza misingi ya biashara na hata misingi ya Marketing na wakajifunza pia namna Network Marketing inavyofanywa kwa usahihi kutoka kwa wale waliofanikiwa (si lazima Tanzania, hata sehemu nyingine duniani). Basi watafurahia matunda yake. Tofauti ya hapo ni hayo uyasemayo.
Nashukuru kwa aliye posti hii topic nadhani kuna mambo yapo sawa lakini mengine sio sawa na hii naweza kusema inatokana na kukosa elimu ya biashara hii. Hii ni biashara mpya huku kwetu, Ulaya na marekani ilianza miaka ya 50 na 60 kwa hiyo unaweza kuona tofauti yake. Ukisoma historia ya biashara hii utaona huko ilikoanza ilipingwa sana mwanzoni, wengi walikuwa na mawazo yanoyojitokeza hapa lakini baada ya muda yalibadilika.
Kuna vitabu, mafunzo, makala, na vifaa vingi vinafundisha jinsi ya kufanya biasha hii na namna ya kuchagua kampuni ya kufanya nayo biashara ya mtandao.Tatizo kubwa kwetu ni kuwa wengi hatupendi kusoma vitabu na makala ili kujua biashara hii na mbinu zake. Ukweli ni kuwa pamoja na magumu ya biashara hii watabiri wa mifumo ya biashara dunia na tafiti zinasema kuwa ndiyo biashara ya karne ya 21(Soma kwa mtandao the business of the 21st century), na itatengeza mamilionea wengi duniani, mfano USA peke yake watu zaidi ya 3500 huwa mamilione kila mwaka na hapa Tanzania nimefanya utafiti hilo limeanza kutokea pamoja na magumu na changamoto zake.
Tatizo linguine la watu wengi nchi zetu ni kama alivyoandika mmoja hapo juu wengi hatukufindishwa elimu ya biashara (business education) mashuleni tuliotoka. wengi tuna ujuzi hatujui namna ya kuuza na hivyo hata ukiwa na bidhaa zako hatujui kuziuza pia. mimi nimekuwa nikifanya kazi na wajasiliamali wengi wa bara hili na TZ pia wengi hatujui kabisa masula ya kutafuta masoko na namna ya kuuza. watafiti pia wanasema the most succesfull people in this world are good salers hapa selling ina maana pana hata mawasiliano (communication) ya faida na kuileza bidhaa au ujuzi wako.
Changamoto nyingine ya biashara hii ni kuwa watu wengi tumezoea kusukumwa sukumwa au kusimamiwa ili mamabo yaende. hii biashara waliofanikiwa ni watu wachapakazi,wanaofanya kazi bila kusimamiwa, wabunifu, wanopenda kujifunza, wanaopenda mabadiliko na wanaopenda kubadilisha maisha yao (wenye ndoto-dream). Ushauri wangu kwa wanaoifanya na wanaotaka kufanya biashara hii ni kwamba wafanye tafiti, wasome vitabu na kuhuduria mafunzo ya namna ya kufanya biashara hii na washikamane na waliofanikiwa nao watafanikiwa na wasiogope kudhubutu.
Kweli mkuu usemayo, elimu / ufahamu kwa kila unachokifanya ni muhimu.., sasa jukumu la kuwaelewesha hao watu si wale wanaofanya kazi hii tayari ? Sasa badala ya watu kusema ukweli na ugumu wa kazi wanapowapa watu false hope kwanza ni rahisi tu na kila mtu anaweza kufanya (hata wale wasiopenda kuuza) huoni kwamba wanaongeza tatizo badala ya kutibu tatizo ? Sababu ni kwamba kinachotokea mamia ya watu wanajiunga na mamia ya watu wanaondoka kila siku.
Pili watu wanasahau kwamba kuna product / bidhaa ambayo inabidi kutumiwa kwahio kabla ya kurukia kupata watu ili wapate wengine ni bora kuhakikisha hao watu unaowapata ni wale watuamiaji wa product. Ni bora wakafahamu Product ndio inayoendesha biashara na Watu peke yake bila Product haina tofauti na Ponzi Scheme na watu wanafaidika kwa entrance /membership fee.
entrance /membership fee ni ada ya aina gani kwa mm ninayetaka kufanya biashara ya networking ?
nifahamishe ili nipate kufahamu vyema au waweza kunitumi tips za somo hilo?
Dr. Said
Ni kweli umeeleza vizuri na kuwapa watu nyenzo za kuweza kunuifa pamoja na kuweka vitabu vinavyoweza kusaidia watu hata kama sio kwenye hii biashara na pia kuwapa motivation.., ila nadhani utakubaliana na mimi bado issue ya gharama ya hizi bidhaa ni kikwazo kikubwa..., sababu hizi suppliments kwa wabongo wingi wa waganga inaonyesha kwamba wateja wapo na watu wanajali afya, tatizo its just affordability.
Alafu issue nyingine ni kwamba wajanja hata huko ulaya mtu akishatengeneza downline yake anatumia hiyo fursa na yeye kutengeneza products zake, mfano info-products, vitabu, cds as well as kufanya seminars na hizi hazitoi bure anakuwa anaziuza, hence anatumia downline yake kujiongezea kipato sio kutegemea tu kampuni husika kutoa commissions. Kwahio people never stop working.
Pia nadhani utakubaliana na mimi kwenye hizi MLM Spill Over Matrix ni bora kuliko matrix nyingine sababu watu wanafanya kazi kama team na kusaidiana hata wale wavivu wanapata faida ya wachapa kazi...., ingawa wale ambao matrix zao hazipo hivi watakwambia hii matrix ni mbaya sababu wavivu wanafaidika kwa kazi ya wachapa kazi.
Kuhusu gharama za bidhaa ni kitu ambacho ni subjective (kila mmoja ana muono wake). Kuna msemo maarufu wa mwanafalsafa na mfanyabiashara maarufu Jim Rohn, anasema "Don't say it's expensive. Say I can't afford it"
Ingawa mara nyingi tunahisi tunanunua bidhaa, lakini ukweli kitu tunachokinunua ni faida (value) inayopatikana kutokana na bidhaa hiyo. Kama mimi ningekuwa nina uzito wa kilo 200 na nikaamua kununua vidonge vya kupunguza uzito. Na vidonge hivyo vikafanya niweze kupunguza kilo 50 ndani ya mwezi, hata kama ile bidhaa ingekuwa inauzwa 300,000/- nisingesema ni ghali kutokana na faida itokanayo na hivyo vidonge.
Kuhusu viongozi kutengeza information products kuwasaidia downlines wake kufanikiwa haina tofauti na mwalimu mzoefu kuanzisha tution nje ya saa zake za kazi. Kama yale mafunzo yatazaa matunda kwa wanafunzi wale, basi ni bora afanye hivyo kwani wengi unaowaona waliotengeneza mamillioni katika hii biashara ni aidha wamenunua vitabu, wameshiriki katika semina nchi tofauti duniani au wanasikiliza trainings zao kwa njia ya sauti (audio).
Kaka gharama ni gharama tu, mtu unaangalia na kipato cha watu husika katika nchi husika na buying power ya watu.., ndio maana hata nikikupa mfano wa Kampuni kama Epson za Printer huwa wanatoa matoleo kulingana na nchi husika, wakitoa kwa Africa wanaweza wakaipa mashine jina tofauti ingawa ipo sawa na mashine ya nchi nyingine lakini bei ya huku inakuwa nafuu kulingana na buying power ya watu.
Sasa kwa Kampuni zinazotoa kwamba ni Health and Wealth..., alafu unajua kabisa mtu hata mkate wake wa siku ni kashehe inakuwa tabu kwa yule mtu kutumia.., alafu hizi suppliments nyingine na za kula kama chakula sio unakula kama dawa (its an everyday thing) Labda ungeniambia njia bora kama baadhi ya hizi kampuni wameshatengeneza pesa za kutosha wanaweza wakaweka baadhi ya viwanda vyao nchini (kukuza ajira as well as kupunguza cost ya importation), lakini kinachofanyika sasa is like Selling Ice to Eskimos.., kuna mtu unajua kabisa hizi suppliments zitamsaidia ila kumwambia atoe 95% ya kipato chake ili kuongeza virutubisho unaona kabisa haumsaidii bali unamuangamiza.
Kuna tofauti ya mimi kununua Ferrari yangu binafsi na mimi kufungua duka la kuuza Ferrari katika nchi ambayo matajiri ni watu wa kuhesabika, au kufungua duka la high end products Kariakoo badala ya kwenda Mlimani City. Kumbuka hapa siongelei kwamba mimi taweza au wewe uliweza, bali katika biashara hii inayotegemea leverage na nguvu za downlines kufanya kazi ana kwa ana inafikia wakati ambapo pool ya watu (wanunuzi) inabidi iwe kubwa sasa ndio hapo majority ya watu mitaani they can't afford the pricesNi kweli kuwa watu wengine watashindwa kununua hizo bidhaa. Lakini haimanishi kuwa hizo bidhaa ni 'expensive'. Kuna tofauti kubwa kati ya kitu kuwa ghali na kutokuwa na uwezo nacho. Nanukuu tena msemo wa Jim Rohn, "don't say it's expensive, say I can't afford it."
Kama mtu uwezo wake ni baisikeli hatakiwi kulalamika kuwa gari ni ghali. Ughali wa kitu unatokana na faida ya kile kitu ukilinganisha na kiasi ulichokitoa.
Investment ya mtu its not only monetary, hata mtu investment ya nguvu zake nayo ni investment tosha.., sasa kuna watu anaangaika kwa udi na uvumba hadi kuwatolea membership fee watu ili nao wajiunge, lakini changamoto zinazowakuta watu wa chini, ambao wengi company yao ni watu wa chini wanajikuta wanakata tamaa sababu kazi yao inakuwa ngumu.Ikisha kitu chengine cha kuzingatia ni kuwa, "je unataka kuwa mnunuzi tu au unataka kufanya biashara?". Kama una nia ya kufanya biashara, ukizingatia mtaji wa kufanya biashara ya Network Marketing ni mdogo sana (kupita kiasi) ukifananisha na biashara yoyote ya kawaida. Hata biashara ya kiosk itakugharimu hela nyingi zaidi (kwa makampuni mengi ya Network Marketing) na potential ya faida yake ni ndogo sana ukifananisha na biashara ya Network Marketing.
Mkuu alafu mimi siongelei sana membership fees au investment fees..., bali naongelea wateja, people we sell products to, je majority of them tena wengi wagonjwa na wanaziitaji, wanaweza waka-afford ?, au ni a chosen few ? and if that's the case unakuta salespeople ni wengi kuliko hata wateja.Mimi nilivyoanza biashara hii ya mtandao nilikuwa mwanafunzi. Nilikuwa nimechacha, sina hela. Hohehahe. Badala ya kulalamika kuwa kianzio ni kikubwa nilikuwa sana naangali ROI (return on investment). Nilivyoina kuwa kurudisha pesa inawezekana, nilikopa hela nikaanza bila ya kusita. Baada ya miezi michache nikawa nimerudisha mtaji wangu na mpaka leo nafanya hii biashara bila matatizo yoyote.
Again siongelei membership fee kwa sana, bali kile kinachouzwa.., mfano kama Kikombe cha Babu kingekuwa bado kina-hit kama kipindi kile alafu akasema hata kujiunga mtu utoe milioni mbili, ingekuwa ina-make a lot of sense sababu tunajua fika demand ya kile kikombe and with no time ile pesa itarudi, hata kama 50% ya watanzania wote wangekuwa wanauza hiki kikombe bado pool ya wanunuzi ingekuwa ya kutosha.Tukija kwenye uweza wa watu kushiriki katika biashara ya mtandao lazima tuelewe kuwa kila kampuna inakuwa inalenga watu wa kundi maalum (Class ya chini, kati na kati na upper class) ingawa makampuni mengi sana (zaidi ya 80%) inalenga middle class. Kuna makampuni yenye vianzio vya $25 na makampuni yenye vianzio vya $20,000. Sasa itategemea wewe upo wapi na ungependa kujenga biashara yako kwa kulenga kundi lipi?
Ndio pale pale nikasema kama nauza Ferrari peke yangu Tanzania huenda ikawa biashara nzuri sababu hata wale matajiri kumi wakinunua tu huenda ikawa ni faida tosha kwa mwaka mzima, ila kama tayari kuna watu wanne wanauza hizo Ferrari alafu na mimi nikawa watano nadhani utaona competition iliyopo..., It is Better to Sale a Lot to a Few People than to Sell Less to a Lot of People, Huo ndio ukweli lakini kwenye hii biashara ya Network people are also a product, kwahio ni lazima uangalie hio product yako (watu/salespeople) je kazi yao ni ngumu au rahisi kiasi gani. Na kwenye nchi ya wengi wenye kipato cha chini utaona kwamba hii ni challenge.Kwa upande wa faida ya kibiashara, makampuni yanayouzi products ghali (High Ticket Direct Selling Companies), zinaingiza faida kubwa na uhakika wa kuingiza faida ni mkubwa zaidi kuliko makampuni yanayo promote promote product za bei ya chini.
Mfano wako kwenye hii case ni very misleading.., moja kwanza lazima ufahamu kwamba kwenye hizi products nyingi commission inayopatikana kwenye every sale of every product sio nyingi kivile, mbili utaona kwamba Network inavyokuwa saturated hence competition inaongezeka na ugumu wa kumpata yule mteja mmoja inavyozidi kuwa ngumu. Tatu angalia culture ya Mtanzania ni price conscious kwahio anything ikishakuwa na bei kubwa inakuwa tatizo. Nne hapa tunaongelea product ya mtu kutumia continuously kila mwezi (kitu consumable) which means mtu anayekinunua sio mara moja kwa mwezi bali ni mara kwa mara.Kuna misconception kubwa ya watu wengi kuwa biashara nzuri ni ile ambayo utapata kuwauzia watu wengi.
Imeonakana kuwa ni rahisi zaidi kumpata mnunuzi 1 atakayenunua bidhaa itakayokuingizia $5000 (high ticket sales) kuliko wanunuzi 200 ambao watanunua bidhaa ya $25. Ni rahisi zaidi kumpata huyo mnunuzi 1 kuliko 200.(unless kama una sales and marketing strategies za bakhressa).
Sababu kubwa kwanini makampuni mengi yanalenga middle class ni kwa kuwa class ya kati ndio wameonekana ni wachapa kazi kuliko class ya chini na hata mara nyengine ya juu.
Na hao wanaotozwa 95% ya kipato kufanya biashara hii wanamiliki magari? How come waweze kumiliki magari na wasiweze kuwekeze katika biashara?
Hayo ni maoni yangu. I hope it's clear.
Thanks for the nice discussion KeyserSoze
Wow! This is getting more interesting. 😉
Kutokana na majibu yako ya mwisho, napata hisia kuwa
- Focus yako ipo katika makampuni ya wellness (kama forever living, tianchi, GNLD, Oriflame na wengineo) kampuni ambazo unanunua wholesale na unauza retail. na unatafuta wateja na watu wa kuwa recruit kwenye biashara. Na hujazingatia makampuni yenye mfumo tofauti.
- Vile vile unaongelea makampuni yanayohitaji wewe kuuza products zenye volume kubwa kwenye market na kuhitaji kujenga network kubwa ili ufanikiwe.
Ofcourse it goes without saying lets say mfano wa Forever au GNLD ilipoingia Tanzania, mwanzoni watu walikuwa hawatambui ni nini even recruitment was easier as the time goes more and more people join recruitment becomes harder na watu inabidi waende mpaka vijijini na ndani ndani kabisa kupata watu zaidi. Now don't get me wrong ili sio tatizo iwapo product zitakuwa zinamove kwa wingi.., ila utakuta kwamba sababu ya prices kuwa juu products zinamove slower due to the fact that the products can only be afforded by a certain class of people. Therefore even if the commission was 80% or 95% kama products ni za wachache (or few can buy) obviously ni wachache watakaofaidika. Pia am not saying all the MLM companies products zao ni expensive (nimeongelea kutokana na kipato cha mtanzania) sababu America, UK na hata South kuna kampuni ya Avon ambayo products zake ni very cheap even comparing with retail shops na quality yake ipo juu vilevile, and what is expensive for Tanzanians Citizens might be very cheap for an American market.
- Una assumption kuwa this is a ZERO SUM game kuwa watu wengi wakijiunga kwenye market itakuwa saturated na itakuwa ngumu watu kujiunga.
- Nahisi kuwa hujua kuwa kuna makampuni ya Network Marketing (direct sales) wanaolipa commision kubwa (zaidi ya 70%) kwa wanachama wake kwa kila mauzo ya bidha zao.
Elewe kuwa
- Makampuni yapo aina nyingi na sio yote yanayofata mfumo huo wa kununua na kuuza na kutafuta wateja. Hata hivyo, bidhaa zao zina market segment fulani na wapo watu wanaopenda hizo products, wanaonufaika nazo na wanazinunua kila mwezi, japokuwa sio wote watafanya hivyo (but the same case is for all products in every industry). 20% ya wananuzi watanunua 80% ya bidhaa. Hiyo ni law ya economics (Pareto's principle) ambayo hatuwezi kuiepuka. Wanachama wa Network Marketing wanatakiwa kujifunza skills za ku target hao 20% na sio 80%. Marketing is all about targeting.
Ofcourse inategemea na buying power ya watu, alafu unaongelea hao watu kumi ambao wewe umewapata ila practically wale kumi watakaowapata kumi watakaowapata kumi baada ya muda kupatikana hao kumi inakuwa ngumu.., ila hili sio tatizo kama products zinauzija sana na ku-move kwa wingi.., ila kama haziuziki (kutokana na bei kubwa kwa available customers) kupata hizo pesa kunakuwa easier said than doneKuna makampuni yanayofuata mifumo tofauti. Mfuma ambao hata kwa Network ya watu kumi unaweza kuingiza zaidi ya $1000 kila mwezi. Huhitaji kujenga Network kubwa kama makampuni mengi.
Ofcourse Amway ipo mpaka leo na baada ya conquering America imekwenda mpaka China na nchi nyingi na Forever and GNLD zitaendelea kuwepo maisha.., that's not a dispute..., Saturation yangu ni kwamba within a given area (kumbuka hapa tunaongelea recruitment) baada ya muda recruitment becames harder as more and more people join hio ndio ninayomaanisha ya saturation, na hapo umeongelea suala zuri la demand.., ndio maana nikasema demand sio kubwa sababu ya bei (ni wachache ambao wana-afford the given products) sio kwamba hawaitaji/hawapendi products hizo. Hata hivyo kuna kipindi kilifika Amway ikawa saturated America ndio maana wakaanza ku-move kwenye nchi na sehemu nyingine. Ili kupata more sales representatives.Tukija kwenye issue ya saturation, it's usually an illusion. Kwenye karatasi saturation inaonekana inaweza kutokea. Lakini in reality sijaona kampuni ambayo imefikia saturation. Ingekuwepo basi Amway (kampuni ya 1959) ingekuwa ishakuwa saturated. Biashara zote zinafata law of demand and supply. As long as hizo product zitakuwa kwenye demand watu watanunua tu hata miaka 100 zijasho.
Kwa ufupi ni kwamba yaani ubishi wangu mimi na wewe ni kwenye Point kwamba Suala la Bei ya Bidhaa kuwa kubwa kuliko uwezo wa wananchi wengi ni kikwazo kikubwa sana kwa hizi kampuni hapa Tanzania...., Hapo Tuuuu