Matatizo ya Mfumo, Mizigo Yapungua Bandari DSM

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
24,825
28,738
MADA MOTO Kupungua kwa Mizigo Bandarini Nani alaumiwe? 08.04.2016

Source: Channel Ten youtube

  • Hakuna Marketing ya Bandari ya Dar Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia , Congo DRC . Bandari Salama (DSM) inadhani bila ''promo'' mambo yatakuwa sawa kwa vile nchi zingine kama Zambia, Burundi, Rwanda, Mashariki ya Congo DRC, Zimbabwe ''hawana jinsi watakuja tu Dsm wanasahau kuna Bandari za Beira, Walvis Bay, Durban n.k
  • Wadau mbalimbali wa Bandari wanawekwa mbali na Mamlaka ya Bandari wadau hao ni TAZARA, RELI ya Kati, Wasafirishaji, Shipping agents, Mkemia wa serikali
  • Mombasa wanapakuwa tani million 9 kwa mwaka wakati Dar-es-Salaam wanapakuwa tani 1.5 Milioni (on-transit/mizigo kwenda nchi jirani) kwa mwaka pia.
  • Mzigo unatolewa ndani ya siku tatu toka kupakuliwa kwenye meli Mombasa wakati Bandari ya Dar-es-Salaam inachukuwa siku 9 mpaka 12 mzigo kutoka geti la bandari ya Dsm
  • Bandari kavu Lubumbashi na Kapiri Mposhi zifunguliwe kwa serikali ya Tanzania na Zambia. DRC Congo kukubaliana. Mbona Burundi walikuwa na gati maalum Bnadari ya DSM toka mkoloni lakini baadaye serikali ya Tanzania ikaondoa kivutio hicho kwa Burundi? Soma zaidi: Belgium Burundi/ Congo special preference Dsm Port Guido Fallentheyn
  • sikiliza mwenyewe matatizo lukuki ya bandari ktk video clip
 
Kwa urasimu wao na ughali Wa gharama mbalimbali zisizo rafiki wa mfanyaviashara wamebakia KUNADI MZIGO YA WANAOSHINDWA KULIPA.
*MTU ANAPOSHINDWA KULIPA KWA SABABU YA GHARAMA KUBWA SI JAMBO LA AFYA KWA BANDARI NA MAMLAKA YA MAPATO HATA KIDOGO.
"lazima itaathiri taifa katika kipindi kisicho kirefu"jamani tuwe na long attractive and friendly plan for users.
 
Mimi Nadhani tusiangalie tu kupungua wingi wa mazigo, pia tuangalie upande wa mapato. Kama mapato hayajapungua basi ongezeko lililokuwepo hapo kabla Lilikuwa halitusaidii zaidi ya kuifanya bandari yetu busy (busy for nothing). Wachache tu walikuwa wanufaika na huenda ndo wanapiga kelele.

Hata hivyo tujipange kuboresha huduma.
 
Mapungufu ya mizigo bandarini ni Kwa sababu wale wakwepa kodi hawaleti mizigo tena.Na kina Masamaki Na wale vilaza wa TRA wako KEKO.
Afadhali tupate kodi zote Kwa mizigo michache kuliko tupate mizigo mingi kodi ndogo.
 
Mkuu,
Wasikilize vizuri wadau wakubwa wanaofanya biashara na Bandari ya Dsm, Angelina Ngalula (Mwenyekiti wasafirishaji wa Malori) na Elias Lukumay (Makamu Mwenyekiti TATO) sababu za mizigo kwenda kushushwa Mombasa, Beira Port of Beira, Mozambique , Durban, Walvis Bay Namibian Port Authority - Namport - Port of Walvis na Lobito Angolahttp://www.fallentheyn.be/EN/Guido_Belbases.html .
 
magufuli anaiharibu Tanzanaia.

swissme

Kuna ka-ukweli maana bila kurekebisha mfumo/mifumo hata ukifukuza kazi watu au kufuta leseni za mawakala lengo la kuongeza ufanisi, tani za mizigo na mapato bandarini halitafikiwa.

Upakuaji kwa mwaka Mombasa tani million 6 , DSM milioni 1.5 nini sababu ya tofauti kubwa wakati kijiografia bandari ya Dsm ingekuwa ina vutia wengi.
 
Mkuu,
Wasikilize vizuri wadau wakubwa wanaofanya biashara na Bandari ya Dsm, Angelina Ngalula (Mwenyekiti wasafirishaji wa Malori) na Elias Lukumay (Makamu Mwenyekiti TATO) sababu za mizigo kwenda kushushwa Mombasa, Beira Port of Beira, Mozambique , Durban, Walvis Bay Namibian Port Authority - Namport - Port of Walvis na Lobito Angolahttp://www.fallentheyn.be/EN/Guido_Belbases.html .
Bwagamoyo nimekuelewa mkuu.Ila tatizo la KODI liko pale pale.Kweli miaka ya nyuma mizigo ni mingi sana iliyokuwa inaletwa kupitia Dar.
Karibu nusu ya hiyo mizigo ilikuwa ni Dili za mletaji Na Masamaki.Serikali haipati KODI Ila kina Masamaki Na wale Mafisadi wanatajirika.
Bandari iajiri maofisa wa masoko nakutembelea nchi zinazo tumia Bandari yetu Na serikali ikapunguza kodi.
 
Hivi mnatenga muda na kuangalia hali ya Uchumi Duniani ilivyo hali ni mbaya si ya kufurahisha sana.Ukilifahamu hili Upungufu wa mizigo umechangiwa na hilo.Acheni hayo mnayoyasema kila siku ooh Waziri Mkuu oohWaziri Mbarawa mlitaka kila siku kutuibia Angalieni na pande nyingine kulikoni.Tusiwe kama Chura katika kidimbwi cha maji kumbe kuna bahari Na bahari
 
Kama mizigo imepungua lakini pato la serikali linapanda,ni dalili kuwa kilichofanywa na kusababisha mizigo ipungue ni sahihi kwa sababu ilipokuwa mingi huku pato la Serikali likiwa chini,ni dalili kuwa hiyo mizigo mingi haikuwa ikitusaidia wala kuwa na faida kwetu na kuna uwezekano kuwa ilikuwa mingi kwa sababu ilikuwa rahisi kukwepa kodi,kutoa rushwa na magumashi mengi hapo bandarini kwetu. Pia pato la serikali kupanda ni dalili kuwa ile mianya ya magumashi na upuuzi mwingine imefungwa na inayopitia hapo kwa sasa ni ile inayotunufaisha,na ya wafanyabiashara au wasafirishaji halali.
Point ya msingi hapa na uliyoigusia pia,ni kuboost zaidi flow ya mizigo kwa kuangalia njia za kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi na wasafirishaji kuitumia bandari yetu ili pato lizidi kuongezeka. Kampuni za magumashi ziendelee kukaa kwenye dustbins na zile halali zipewe motisha ili zivutike kuendelea kuitumia bandari yetu na hata mpya pia ziweze kuvutika kuja kwetu.
 
Hiyo ndiyo Point tuangalie ni kwa jinsi gani tutapat wateja wengi Na siyo wale Magumashi wanaojaza Bandari yetu na kutumia huduma zetu pale Bandari kisha Wanatutoa kapa (Serikali) wao wanaendelea kutajirika .Jitahada Zifanyike waongezeke hata hao wachache wanaozingatia sheria na za kutii.Wafanyabiashara kuona ufalme wa mbinguni ni sawa na Ngamia kupita katika Tundu la sindano
 
  • Mombasa wanapakuwa tani million 9 kwa mwaka wakati Dar-es-Salaam wanapakuwa tani 1.5 Milioni kwa mwaka pia.
Hizo takwimu zipo sahihi kweli?

Mizigo lazima ipungue maana yule tapeli aliyefuta kampuni yake kabla ya Magufuli kuingia madarakani alikuwa halipi kodi serikalini. Yeye ndiyo alikuwa serikali akichukua kodi kwa wafanyabiashara hasa wa Kariakoo maarufu kwa kuleta bidhaa feki.
 
Bandarini kunahitajika marekebisho ya kina kuhusu uongozi mzima na watendaji zaidi ya 50% hawako competent, usishangae manager wa bandari (wharf) hajui maana na aina ya misamaa ya kodi? this is a shame!!! meneja haelewi anasababisha ucheleweshaji wa mizigo kwa uzembe halafu tunasema tuna watu hapo? kama meneja haelewi unategemea watendaji wengine watakusaidia nini, Tanzania kazi ipo! bandarini kumeoza, maofisa ukaguzi wa TRA (bandarini) wengi vishoka wanasumbua wateja kwa kuwaongezea thamani za mizigo, sasa hapo unategemea nini? mhhhh!!!
 
  • Mombasa wanapakuwa tani million 9 kwa mwaka wakati Dar-es-Salaam wanapakuwa tani 1.5 Milioni kwa mwaka pia.
Hizo takwimu zipo sahihi kweli?

Mizigo lazima ipungue maana yule tapeli aliyefuta kampuni yake kabla ya Magufuli kuingia madarakani alikuwa halipi kodi serikalini. Yeye ndiyo alikuwa serikali akichukua kodi kwa wafanyabiashara hasa wa Kariakoo maarufu kwa kuleta bidhaa feki.

Ufafanuzi. Umewasikia wadau ktk video clip wanatuambia takwimu zinazotolewa na TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) ni za ''kupikwa'' ukweli ni tani hizo unaazosikia ktk video clip 1.5 Millioni za kwenda nchi jirani (on-transit) na ndiyo maana wanataka kiwango hicho kizidi maradufu. Mizigo ya wateja-wa-ndani haina namna lazima kupakuliwa ktk bandari ya Dsm lakini mizigo ya kwenda nchi jirani wana nafasi ya kutumia bandari zingine zaidi ya Dsm.
 
Sina uhakika hiyo video clip ni ya lini.
Report ya TPA ya mwaka 2013/14 inaonyesha tani million 15. Ndiyo, tani million 15!
Report ipo hiyo ya mwaka 2013/14 hadi sasa ipo kwenye website yao ukurasa wa 22.
Hizo tani 1.9 million ilikuwa miaka ya nyuma zaidi.
Fuatilia hizo takwimu huko.
 
Nimetazama video wanasema takwimu hizo ni za 2014 na kuwa matatizo ya mizigo kupungua ni kutokana na serikali kutochukua hatua mapendekezo ya wadau miaka miwili iliyopita na sasa ndiyo Tanzania na serikali ya awamu ya tano inakumbushwa changamoto hii.
 
April 14, 2016

Kamati ya bunge imesema bandari ya DSM haimo katika kundi la bandari 7 zinazofanya vizuri.

Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu imesema bandari ya Dar es Salaam haimo katika kundi la bandari saba zinazofanya vizuri katika ukanda wa Afrika licha ya kuwa katika mazingira mazuri kijiografia ya kufanya biashara zaidi ya nyingine.

Source: ITV Tanzania youtube
 
Back
Top Bottom