Mabasi ya mikoani kwenye barabara ile kweli njia mbili? Mnasubiri janga lipi mtambue zile hatari za Kimara zinahamia Bunju?Kwa ufupi,
Sijui mipango ya hii miji inapangwa vipi. Kipindi serikali inafanya juhudi kutanua Morogoro road moja ya sababu kuu ilikuwa ni kuzidiwa kwa wingi wa magari.
Hivi nani aliamua mabasi sasa yaanze kupita Bagamoyo road na huku Morogoro imetanuliwa na bila upanuzi wa Bagamoyo road? Hivi mnaona yanayoendelea kwenye hiyo barabara? Hayo maeneo ndio premium kwa nchi kwasasa na magari ni mengi ila barabara finyu.
Mabasi ya mikoani kwenye barabara ile kweli njia mbili? Mnasubiri janga lipi mtambue zile hatari za Kimara zinahamia Bunju?
Anyway, hizi barabara tunatumia wote! Ila hatari haichagui. Mnawapa mizigo trafiki isiyo na ulazima.
Juzi mmeona yaliyotokea! Wote tunaona yanakuja mengi zaidi. Chukueni hatua!
Kwahiyo tatizo ni uendeshaji mbaya wa madereva wa mabasi sio?Sasa hivi hiyo barabara ajali kila kukicha! Imagine mashule yaliyojaa huko na school buses achilia mbali watumia njia wengine. Mabasi yanatanua kwa kasi bila kujali kabisa.
Mwezi wa 4 hiyo barabara kulitokea ajali 3 mfululizo
Cc Mbaga JrMabasi ya mikoani kwenye barabara ile kweli njia mbili? Mnasubiri janga lipi mtambue zile hatari za Kimara zinahamia Bunju?View attachment 3587644
Nimetumia sana njia hio nuda wa jioni madereva wa huko ukiachilia mbali wa mabasi wanaendesha hovyo sana. Hio hio njia nyembamba maderva wanalazimisha njia tatu hadi nne unategemea nini?Barabara nyembamba sana unategemea nini kwa mabasi ya mikoani na malori? Ni hatari sana
Huyu mzee bhana 😂