Matatizo ya Engine za Toyota IST na suluhisho lake

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,662
2,745
Wanajamvi,
Kama tujuavyo IST ndio Gari zilizo nyingi kwa sasa mtaani na zote zikiwa na Engine model 1NZ-Fe (CC1490) na 2NZ-Fe (CC 1290)

Engine za 1NZ na 2NZ zote kwa pamoja hukumbwa na matatizo yanayo fanana kama ifuatvyo;

1. Engine kula sana Oil.
-Hizi engine zikifika kuanzia km 120,000-150,000 huanza tatizo la kula sana oil, suluhisho ni kubadili Piston ring (kama gari inatoa moshi mweupe) na Valve stem seals.

2. Rough idle.
-Badili Throttle body na idle control valve

3. Engine kupiga mluzi
-Cheki na badili alternator belt

4. Engine high vibration
-Cheki Fuel Filter/ weka mpya
-Safisha injectors
-Cheki engine mounts plus interior one

5. Kama engine yake imefikisha km 100,000-150,000 unashauriwa kuicheki Chain Tensioner mara kwa mara au weka Timing Chain mpya ili kuondokana na tatizo la motor tapping

6. Hakikisha unatumia engine oil iliyopendekezwa na Toyota kwa ajiri ya engine za 1NZ na 2NZ ambazo ni 5W-30 na 10W-30. Kwa ulinzi wa Gari lako hakikisha unatumia Full Synthetic Oil. Hii itakusaidia kuepukana na tatizo la oil pressure sensor na rear crankshaft oil seal leakage.

Asanteni, na karibuni Kwenye chama cha wenye IST.
 
Natumia ist ya pili sasa sijawahi juta. Mwanzoni nilikuwa na polo (my first car), nikaona miyeyusho kwenye spare na matengenezo....

Nikakauza na kununua ist kwa dem mmoja hivi, akatokea dem mwingine akakapenda, nikapiga bei ya maana.
Nika ongeza 1m nikaagiza kingine.

Niliuza ist nika agiza ist.

Ist itabaki kuwa Juu (in Makonda Voice )
 
Hizo changamoto ulizotaja huenda zikawa kwenye injini tofauti tofauti za Toyota. Ninatumia gari yenye injini ya 1ZZ-FE (1794cc), hizo changamoto zote nimekutana nazo.

Ilikuja imetembea roughly 160,000km, hapa nimeitumia miaka 5 kasoro miezi 2, changamoto za kula oil nilikutana nayo, bahati mbaya it was worse, hivyo overhaul ilifanyika. Tukabadili oil seals, piston rings na cones. Imeacha kula oil. Oil ilikuwa inavuja inaingia kwenye throttle body.

Nilibadili idle control valve, engine mounts pia baada ya kuwa na mtikisiko mkubwa wa injini hadi ndani unauhisi.

Hivi karibuni nimebadili fuel pump baada ya gari kuwa inakosa nguvu pale ninapopanda kilima au ninapobeba mzigo na watu.

Kwa mujibu wa mtandao fulani, injini nyingi za Toyota, life span ni 200,000km. Ikigonga hapo, changamoto kama hizo zinakuwa za kawaida. Muhimu kuzifanyia kazi na maisha kuendelea.
 
Shukran sana mkuu. Yapo ya kujifunza hapo, yangu ina km 120000 lkn naona tayari imeanza kula oil japo ni kidogo sana lakini inakula, haina tatizo lolote nadhani ni valve seal zimeanza kuisha.
 
Hapo mi naona ni kuzeeka kwa baadhi ya parts hasa kwenye gari zenye engine ndogondogo kama ist zikishafika kuanzia 120,000 km....... cha msingi ni matunzo tu na kuipa gari kitu inataka
 
Hapo mi naona ni kuzeeka kwa baadhi ya parts hasa kwenye gari zenye engine ndogondogo kama ist zikishafika kuanzia 120,000 km....... cha msingi ni matunzo tu na kuipa gari kitu inataka
Yes, that's the reality. Kwa engine ndogo hizi km 120000 uzee unakuwa umeanza kuingia kwenye engine kwa baadhi ya parts. Kinachotakiwa ni kuifungua yote na kununua baadhi ya parts kama valve na seals zake, piston ring na baadhi ya vitu vidogo vidogo. Ukiweka genuine parts utaenda kilometa 120000 zingine bila shida
 
Natumia ist ya pili sasa.....
Sijawahi jutaa.....
Mwanzoni nilikuwa na polo (my first car), nikaona miyeyusho kwenye spare na matengenezo.
Haleluya! Haleluya! Haleluya! That's the car buana watu waache madharau! We are very comfortable and its a very reliable car
 
Habari za majukumu wadau gari yangu ni passo ilikuwa inaleta taa ya check engine baadae ikajaleta taa nyekundu gari likazima mafundi wakasema engine imekufa tukanunua engine ileile wakafunga haina hata wiki bado inaandika check engine hapo tatizo ni nini?
 
Habari za majukumu wadau gari yangu ni passo ilikuwa inaleta taa ya check engine baadae ikajaleta taa nyekundu gari likazima mafundi wakasema engine imekufa tukanunua engine ileile wakafunga haina hata wiki bado inaandika check engine hapo tatizo ni nini?
Utakufa na Pressure uza hii gari nunua nyingine.
 
Habari za majukumu wadau gari yangu ni passo ilikuwa inaleta taa ya check engine baadae ikajaleta taa nyekundu gari likazima mafundi wakasema engine imekufa tukanunua engine ileile wakafunga haina hata wiki bado inaandika check engine hapo tatizo ni nini?

Yani engine na vifaa vyake vyote hivo unaambiwa tu imekufa unakubali?....

Mfano spika haina vitu vingi just a coil ndo chanzo cha sauti spika ukiambiwa imekufa kwel yaweza kuwa i ekufa labda imechoma coil ...lkn sio mtu kukwambia radio au tv imekufa zenyewe zina vitu vingi vinavofanya kazi pamoja huenda kifaa kimoja kilikufa kinahitaj replacement lkn sio kusema eti engine yote imekufa na ww ukubali tu
 
Back
Top Bottom