Matatizo ya Afya ya Akili

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,118
Hizi ni dalili za mtu mwenye ugonjwa wa afya ya akili ujulikanao kama Sonona (Depression).

Kumbuka: Usijitafakari kwa kuona dalili mojawapo na kuhitimisha kuwa unalo tatizo la afya ya akili, jaribu kujiona inaweza kuwa ni tabia yako umezaliwa nayo. Dalili zaidi ya mbili kutokea mfululizo zaidi ya wiki 2 ni tatizo tayari.
  • Mfadhaiko/kukosa amani kabisa.
  • Hasira za haraka isivyo kawaida.
  • Kupoteza hamu ya ulivyo vipenda.
  • Kujitenga au kutojumuika na watu.
  • Kupoteza sana kumbukumbu.
  • Kulala sana au kukosa usingizi.
  • Kuhisi huna thamani/kujidharau.
  • Hali ya simanzi na kulia lia.
  • Kukosa hamu ya kula.
  • Wengine hula sana kupita kiasi.
  • Kutojijali, uchafu kupitiliza.
  • Uchovu na uvivu wa mda mrefu.
  • Kuduwaa.
  • Hofu na wasiwasi.
  • Wasiwasi.
  • Lugha za kukata tamaa.
  • Kupoteza hisia za mapenzi.
  • Maumivu ya shigo, mabega, kichwa na mgongo bila kufanya kazi ngumu na nyinginezo.

Kama ni hali mpya katika maisha yako na imeanza baada ya wewe kupata changamoto za maisha na inakuchukiza ila huna jinsi ya kujinasua wasiliana na mtaalamu wa Afya ya Akili.

KUMBUKA: Wewe mwenyewe ndiye unafahamu kama unapitia matatizo kadhaa, na unajua kama yanakusumbua au hayakusumbui. Hivyo dalili hizo hapo juu hazimuhusu mtu ambaye anaona kabisa hana changamoto, na kama ana dalili hizo yawezekana ikawa ni tatizo lingine.
 
daaaah kwenye i think i have 7
 
Back
Top Bottom