Matatizo kwa mjamzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo kwa mjamzito

Discussion in 'JF Doctor' started by Amoeba, Nov 17, 2009.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Wakuu Mke wangu ana mimba ya miezi mitatu, amekuwa akilalamika mara kwa mara maumivu kwenye kitovu, pia moyo kubana. Tumeenda Hospitali mara mbili, majibu tunayopata ni kwamba, hiyo ni hali ya kawaida kwa miba ya miezi miwili mpaka mitatu! lakini hali hii naona haikomi!!! Kama kuna mtaalamu wa magonjwa ya wanawake na watoto atusaidie ushauri tafadhali, kwani nampenda sana mke wangu, akilalamika tu naona anateseka.

  Natanguliza shukrani zangu
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa Ushauri wangu kama Doctor amesema kuwa hali hiyo ni ya kawaida inategemea huyo Mke wako kama ndio Mimba yake ya kwanza basi hayo matatizo yatakwisha itakapo kuwa hiyo mimba imefikisha miezi 4 au mwezi wa 5 ondosha wasiwasi au kama wewe ni mkristo nenda kwa Mchungaji akamuombee au kama wewe ni muislam nenda kwa shekhe akamuombee kwa Mwenyeezi Mungu kama ni shekhe mwambie Achukue maji katika Glasi Ayasomee hayo Maji ndani ya glasi baadhi ya sura za Qur'ani Ampe Anywe hayo maji na mengine anywe maji na kidogo umwagie katika kichwa na huyo Shekhe ayasomee maji mengine katika Glasi achanganye katika maji mengi uyatumie kila siku kutwa mara tatu kabla ya kula kitu Mwenyeezi Mungu Atamsaidia matatizo hayo yatakwisha Onyo Usiende kwa Mganga wa kienyeji tafadhali
   
 3. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri mpate second opinion, kuna magonjwa common wakati wa ujauzito hasa miezi 3 ya mwanzo mfano maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kutapika etc. Magonjwa mengine yanayojitokeza ni pamoja na kisukari, blood pressure na magonjwa ya moyo, haya yanahitaji ufuatiliaji wa karibu wa daktari.

  Kuna issue nyingine incompetent cervix ambayo inamsababishia mama kuingia premature labor. Kuepuka hili kama mama ana maumivu chini ya kitovu, cramping au kama anaspot amuone daktari mara moja. Kwa hili tatizo madaktari aidha watafunga njia ya kizazi au watamuweka mama kwenye complete bed rest.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ujauzito unaambatana na mabadiliko kadhaa ya kimwili/kimaumbile. Pamoja na vipimo na matibabu, ni vema pia nyote wawili mkajianda kisaikolojia hususani kama ni ujauzito wa kwanza kuzielewa na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoletwa na mabadiliko yanayotokana na ujauzito.

  Mara nyingine, maumivu ni 'perception' zaidi kuliko ukweli. Utafiti unaonesha wanawake 'wanaosumbuliwa' na ujauzito wengi wamo kwenye ndoa ama uhusiano ulio rasmi. Hii inaashiria mchango mkubwa wa kisaikolojia katika ujauzito.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu pole, kama uko Dar kamuone dokta mmoja anaitwa Kapona yuko muhimbili au Tumaini... yeye hutoa msaada kwa wote wawili, kama uko nje sijui umuone nani ila siku hizi kuna lots of reference mateirals kwenye mitandao na vitabu ambavyo vinapatika. Nunua au download them usome sana, huu ndio wakati wako wa kujua afya ya mama na mtoto kiundani zaidi,

  msaidie mpenzi wako
   
Loading...