Matatani Uganda kwa kuchapisha kibonzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatani Uganda kwa kuchapisha kibonzo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waandishi Habari wawili waliokuwa wamekamatwa nchini Uganda kutokana na kibonzo kilichochapishwa katika jarida lao wameachiliwa kwa dhamana, lakini wameamriwa kuripoti katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi, CID, ili kujieleza.

  Walifika huko siku ya Alhamisi lakini wamesema hakuna walichoambiwa bali kuamriwa kurudi tena siku ya Ijumaa.

  Mhariri wa jarida la kila mwezi Summit Business Review, Mustapha Mugisa pamoja na mchapishaji wake Dk Samuel Sejjaka, inadaiwa walikuwa na nia ya kumkejeli kiongozi wa taifa.

  Walikamatwa mapema wiki hii, na wakili wao, Murungi Godwin, alisema wateja wake wamekuwa wakiripoti katika kituo cha polisi, pasipo kuchelewa, na kilichofanyika Alhamisi, ni kama kuwaongezea dhamana.

  "Waliachiliwa kwa dhamana, na kutakikana kuripoti jana, na tulipofika hapo, afisa aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, alitueleza turipoti tena leo", alielezea Murungi.

  Mhariri wa jarida hilo ambalo huchapishwa kwa Kiingereza, Mustapha Mugisa, alisema askari wapatao kumi waliingia afisini mwake, na kumuuliza ikiwa yeye ndiye mhariri wa jarida hilo, na alipothibitisha hayo, walimuelezea lilikuwa na kibonzo, na ilielekea jarida lilikuwa na nia mbaya ya kisiasa, na hivyo wakamkamata.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Vi nchi vyetu na udikteta. M7 ni baba la madikteta wa afrika mashariki na kati
   
Loading...