kisugujira
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 774
- 200
WanaJF,
Ni lini tutaondokana na hali hii ngumu ya upatikanaji wa ajira? Kwa wale wasio na ajira kama mimi nawashauri kuwa makini sana na baadhi ya matangazo ya kazi yanayowekwa mitandaoni.
Kutokana na ugumu wa ajira, matapeli wameamua kutumia mwanya huo kwa kuweka matangazo feki ya kazi mitandaoni na kuwaibia wale wote wanaomba kazi hizo! Kuna tangazo la nafasi za kazi toka kampuni inayojiita HD CO Ltd liliwekwa katika mtandao wa zoomtanzania.com siku kadhaa zilizopita kwa lengo lililofanikiwa kwa kuwaibia walengwa.
Kuna mtu anayejiita HR DIRECTOR wa kampuni hiyo kwa jina la ERICK URASA aliweza kumwibia kila mtu aliyepata walaka wa elektroniki (email) unaomtaarifu kuwa anatakiwa kuhudhuria mafunzo ya kazi kama sehemu ya usaili kabla ya kuchaguliwa na kupangiwa sehemu ya kwenda na kuanza kazi.
Watu waliopata walaka au ujumbe huo walitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000/-) kwa kutuma kwa njia ya MPESA namba +255764660443 na kupangiwa sehemu za kuhudhuria mafunzo hayo ya awali kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini. Kwa mfano hapa Dar ES salaam kuna watu walielekezwa kwenda TANZANITE EXECUTIVE SUITE lakini watu walipofika pale hakukuwa na mafunzo wala semina yoyote zaidi ya kuambiwa wametapeliwa!
Namba hiyo ya simu (+255764660443) ikipigwa haipatikani na imesajiliwa kwa jina la ERICK SAMSON URASA! Hawa watu ni hatari sana katika soko la ajira kama walivyo baadhi ya mawakala wa kazi toka nchi jirani wenye upendeleo na ubaguzi kwa wasiotoka nao sehemu moja na hivyo kuchochea uwakaji wa utambi wa bomu la ukosefu wa ajira na kusababisha siku moja likalipuka na kuleta madhara kwa Taifa.