Matapeli wa Ukweli Kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matapeli wa Ukweli Kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Jul 5, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Source: Yahoo friends


  Mimi sijui kama hapa ndio mahali pake, lakini nadhani bora ujumbe. Nimeweka na anuani ya source halisi kwa sababu yeye mwenyewe kaweka na labda ukitaka wasiliana naye, kwa kuwa kaguswa kuielimisha jamii kwa namna hii. Shule zingine zinapatikana katika mazingira magumu sana.

  Wapendwa katika Bwana,


  Za siku nyingi kwa waliowengi wenu. Mungu azidi kuwabariki na kuwatunza. Nimepata kisa hiki kilichojirudia hivi karibuni baada ya kupotea kwa takribani miezi mitatu minne hivi....kama unapenda pesa za chapchap bila kufuata mpango wa Mungu...ni rahisi sana kwako kutumbukia. Soma uone. 1. wizi mpya umeibuka...kaa chonjo

  Ndugu wapendwa,

  Story ifuatayo ni ya kweli. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri.

  Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangu sikuwa na shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

  TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
  Mimi: Nzuri
  Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
  Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
  Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
  Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana , after all alikuwa hajasema anachotaka)

  Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo madawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery!

  NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya successfully.

  Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

  Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.

  Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.

  Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details.

  Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on in my head!

  Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:

  MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?
  MIMI: YES
  MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution; we are looking for 50 pairs?
  MIMI: Yes I have sufficeint stock
  Mzungu: what is your price per pair?
  Mimi:$1700
  Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid in dollars or TZS
  MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)
  Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cash or by cheque?
  Mimi:Cash
  Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier we need this liquid urgently possibly today, and since you have said you have enough
  stock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, please arrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pair of the sample with you.
  Mimi: No problem at all I have been in this business for quite sometime now you can be sure everthing will be fine.

  Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija. Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwa saa nane.

  Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (Kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).

  Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last week.

  Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na makabila mengine.

  So guys thats my story

  Dismas Shekalaghe,
  National Team Leader,
  LIFE Ministry (T),
  P.O.Box 7962, Dar Es Salaam,
  Tel. (Office) +255-22-2461965; Fax: +255-22-2462014;
  Mobile: +255-713-270164; +255-762-413132;
  Email: Office: admin@lifeministrytz.org
  Personal Emails: dismas.shekalaghe@lifeministrytz.org; dishekalaghe@gmail.com
  Website:
  www.lifeministrytz.org; Blog: http://changeyourdestinytz.blogspot.com
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,690
  Likes Received: 1,127
  Trophy Points: 280
  Ni ndefu sana,nimeiba muda wa ofisi kuchungulia hapa janvini,....anyway ntasoma home jion
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,517
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana, hii mewaliza watu siku nyingi tangu mwaka juzi watu wanalizwa same story same actions .
  Kwakweli ni kalil
  Hebu tuwekee simu zao hapa ili tuweze kuwa makini.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 0
  Hii bona ni ya MWAKA JANA mkuu?!!!!!! Kweli ulipitwa.
   
 5. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,973
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Masikini mtaani akikuomba msaada unatoa jelo tena cheni-chenji! Umeonaee...! Pole Mkuu bai ze wei.
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hii ilitokea toka mwaka juzi watu wanaijua
   
Loading...