Matapeli wa ajira

Kuziwa

JF-Expert Member
May 23, 2011
248
212
habari wanajamii!
napenda kushare yalionikuta kama wiki mbili zilizopita, nilitumiwa email na mtu mmoja aliyejitambulisha kua anafanya kazi STMICO katika mgodi wa tulawaka. akanieleza kuna post mpya za administration zimetoka na bado hazijatangazwa, kwa kua nilikua na connection naye kupitia mtandao wa linkedin, aliona anishirikishe ili kama nakubaliana naye nianze kufanya mchakato wa application.
nilikulikubali na akaniambia nimtumie cv yangu kwa email yake ili anisaidie kuisubmit kwa HRO, nilifanya hivyo na tukawasiliana baada ya kuipata. baada ya muda mfupi alinipigia kua pia MEDICAL EXAMINATION INAHITAJIKA, aliniuliza kama ninayo fasta fasta. kwa kua sikua nayo, aliniambia kua kuna doctor yupo bugando ni mshkaji wake anaweza kuiforge fasta ili itumwe, so akaniambia kua nitume elfu kumi ili jamaa anisaidie. sikuona kua ishu, nikamtumia 10000 kwa mpesa. baada ya hapo alinipa aliniambia kua atanipa feedback siku ya pili.
kweli siku ya pili alinipigia simu kua ameshasubmit kila kitu so tutaendelea kuwasiliana, siku hiyo ya pili mchana akanipigia simu kua kama nina chochote nimtumie yule HRO ili afanye mambo faster faster na ikibidi aniweke kwenye batch ya kwanza, mmhh! nikaanza kustuka na nikaanza kuchunguza, nikafuatilia details za huyu jamaa, nikaona kweli kila details zake zinaonyesha kua yeye ni mfanyakazi katika mgodi huo wa tulawaka. ila nikawaza zaidi kwa nini haombi hela nyingi? nikagundua kua huyu jamaa utapeli ndio kazi yake na itakua anatapeli vihela vidogo vidogo tu kwa watu wengi ili wasimstukie na inawezekana kweli anafanya kazi huko, au alishawahi kufanya kazi huko.
anachokifanya ni kujiunga na mitandao mbalimbali, hasa ile ambayo ni kwa proffessionals kama linkedin, then anacheki profile yako, akiona inalipa kwa job flan, anakutafuta na kukuomba uwe rafiki yake, soon anakuunganishia job kama vile yeye ni kijana mmoja msamaria sana.
 
Nimeshawah kukutana na mtu kama huyo linked in lakin alifua dafu mi mwenyew mtoto wa mjini ataanzaje kuniingiza mjini labda
 
ni mawazo yako kaka! nilistuka mapema! kala elfu kumi yangu tu, alikua ananiengeneer ili nimpe nyingine
 
Back
Top Bottom