Matapeli 400 wa nyumba wabainika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matapeli 400 wa nyumba wabainika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jul 7, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,774
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Matapeli 400 wa nyumba wabainika
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dodoma; Tarehe: 6th July 2010


  JUMLA ya wapangaji 376 wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wamebainika kupangisha nyumba kwa wasio walengwa bila idhini ya shirika hilo, imeelezwa.

  Hatua hiyo imebainika wakati wa uhakiki wa wapangaji wa shirika hilo ulioanza kutekelezwa nchini kote kuanzia Machi mwaka huu.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, akiwasilisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa 2010/11 bungeni jana, alisema wapangaji hao haramu wamebainika katika kipindi hicho kifupi.

  Aidha, Chiligati alisema wapangaji 28 wamepangisha nyumba kwa watu wengine baada ya kupewa vibali na shirika hilo.

  Alisema katika mwaka huu wa fedha, NHC itaendelea na mchakato wa kufuta upangaji wa wapangishaji na kuhalalisha upangaji kwa watumiaji wa sasa.

  “Hatua kali za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya watumishi wa shirika watakaobainika kushiriki njama hizi za kujinufaisha binafsi na kupitia upangishaji haramu,” alisema Chiligati.

  Katika maoni yake, Kambi ya Upinzani iliipongeza NHC kwa hatua hiyo ya kubaini wapangaji haramu, ikisema unyonyaji huo ulikuwa hauinufaishi NHC wala Taifa, bali watu binafsi.

  “Kutokana na juhudi za uongozi mpya, suala hilo litafikia tamati na Serikali itapata stahiki yake. Kwa hiyo ni vyema tukapongeza kwa hatua hiyo," alisema Msemaji wa Kambi hiyo, Ali Said Salim.

  “Kambi ya Upinzani inataka Serikali na waheshimiwa wabunge wote kuliangalia suala hili, hivyo basi, biashara hii katika nyumba za umma haipaswi kuendelea, kwani ni unyonyaji na dhuluma kwa Watanzania wengine na isitoshe imekuwa ikiipotezea Serikali mapato kwa kuwa ni mfumo wa siri unaokwepa kodi halali,” ilieleza hotuba ya Salim iliyosomwa na Mbunge wa Micheweni, Shoka Khamis Juma (CUF).

  Kuhusu azma ya NHC kuuza baadhi ya nyumba zake ambazo gharama za kuziendesha ni kubwa kuliko mapato, Waziri Chiligati alisema kazi hiyo inahitaji maandalizi makubwa.

  Alisema maandalizi hayo yanahusu kuwatambua wapangaji wa nyumba hizo na uwezo wao wa kulipia ununuzi, kutafuta benki zitakazowakopesha fedha za kununua nyumba (flats) na pia kuwaelimisha wahusika taratibu za umilikishwaji chini ya sheria ya umilikishaji wa sehemu ya jengo.

  “Maandalizi haya yakikamilika, ndipo uuzwaji wa nyumba hizi utaanza kutekelezwa. Napenda kurudia kwamba NHC watauza sehemu tu ya nyumba zao zinazowapa hasara kuziendesha na si nyumba zote,” alieleza.

  Alisema kwa mujibu wa mpango mkakati wa NHC wa miaka mitano (2010/11 – 2014/15), katika mwaka huu wa fedha, itaanza ujenzi wa nyumba 1,000 kwenye maeneo yenye uhaba hasa katika Jiji la Dar es Salaam.

  Aidha, alisema shirika hilo litaanza ujenzi wa majengo ya vitega uchumi na nyumba za makazi katika mikoa mbalimbali nchini.

  Alisema kwa mujibu wa mpango huo wa miaka mitano, shirika litakuwa limejenga wastani wa nyumba 3,000 kila mwaka na mikoa yote itahusishwa katika ujenzi huo.

  Kuhusu mikopo ya nyumba, alisema tangu kupitishwa kwa Sheria ya Mikopo ya Nyumba ya mwaka 2008 iliyoanza kutumika Mei mwaka jana, benki tano zimeanza kutoa mikopo ya kujenga na kununua nyumba.

  Alizitaja benki hizo kuwa ni Azania, Commercial Bank of Africa Ltd, International Commercial Bank, Stanbic na United Bank of Africa.

  Alisema ni matarajio kwamba benki nyingine tano nazo zitaanza kutoa mikopo ya aina hiyo baada ya Serikali kuunda kampuni inayojulikana kama Tanzania Mortage Refinancing Company (TMRC).

  “Kampuni hii binafsi inamilikiwa na benki za nchini, itakuwa inatoa mikopo ya muda mrefu kwa benki, ili benki hizo ziweze kukopesha wateja wao mikopo ya nyumba ya muda mrefu (miaka 20-25 au zaidi) na yenye riba nafuu,” alifafanua Chiligati.


   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nchi hii issue si kubaini matapeli bali kuwachukulia hatua. Matapeli huwa wanafahamika haraka sana lakini inapokuja suala la kuwachukulia hatua kunakuwa na kigugumizi cha ajabu. Kwa mfano matapeli wa Rada, Richmond, EPA, Meremeta nk wote wanajulikana lakini mpaka leo hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa zaidi ya kuambiwa "uchunguzi bado unaendelea".

  SItaki kuwasifu NHC katika hili mpaka nitakapoona matapeli hawa wamechukuliwa hatua muafaka
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mbona hiyo siyo siri! tena tunatozwa kodi kubwa zaidi ya ile ya shirika!
   
Loading...