Jamani nilipokuwa mdogo hii ndo ilikuwa hobby yangu maana kwa umbo langu dogo sikuweza kupigana ila ukinikosea kidogo..nitakupa neno utakaa kimya mwenyewe!
Najikumbushia tu...(usinichukie...)
Unataka matani..
Nyani Ngabu, una bichwa kubwa mpaka shuleni ulikuwa unaitwa Headboy! twende twende..
Fidel80, wewe umekonda mpaka ukisimama kwenye ukuta unakaa kama crack...
Mzee Mwanakijiji demu wako amekonda mpaka akivaa t-shirt ya bluu anafanana na sim card ya tiGO..
Asprin unamashavu kama mimba ya panya..
Na wewe TUKUTUKU uso kama shamba la matuta...
Unataka unataka..
Mwangalie kwanza, wewe Bigirita yaani wewe ni mbaya mpaka hutumia lotion inayoitwa 'why bother!'..teh teh..
Zak wewe ni mweusi mpaka ukirushiwa jiwe linarudi kuomba tochi...
watu8 wewe ni mshamba hadi mara ya kwanza kupanda daladala ulianza kutandika vitambaa kwenye siti.
PS: On a light touch...
hehehe wivuuu! Paw ni handsome hujapata kuona. chezeiya chotara wewe
Hanini....nawewe umepotea njia mwone...macho ka umepachikwa.
Hahaha 😱
Dah mkuu upo?
Mwangalie macho kama unalala nayo.
Wewe ni mchafu mpaka maji yana...scratch ukioga.
Mwone kwanza, ninyi kwenu ni maskini hadi geti la nyumba mnafunga kwa pini!
Kwenda huko, nyie kuku wenu ni malaya hadi wao hufanyaga abortion ya mayai!!!
Mwone kwanza, ninyi kwenu ni maskini hadi geti la nyumba mnafunga kwa pini!
Kwenda huko, nyie kuku wenu ni malaya hadi wao hufanyaga abortion ya mayai!!!
Piere. Fm umefulia hadi ukiweka mkono mfukoni kunatoka mwangwi!muone ulivyo na bichwa kubwa mpaka unashndwa kusikitika.
muone vile kichwa kama tofali
Nafikiri tunajaribu kuondoa stress za uchaguzi eeehh, haya bwana taratibu tu usijemtukana mkweo, naskia mpaka vidingi vimo humu JF!!! Sijajua JK na PINDA wanatumia nickname gani bt i think ni moja kati ya ulizotaja hapo juu, Makamba yeye anatumia nickname ya Malaria sugu au ZUBEDA