Matamshi yanayowashinda wengi

Nyamanoro

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
651
518
Mimi napenda sana kujifunza Lugha yetu hii ya Kiswahili. Leo ningependa kuwashirikisha juu ya changamoto inayowakabili watu wengi sana katika kutamka baadhi ya maneno ya Kiswahili. Kuna maneno mawili ambayo watu wengi yanawashinda kutamka, ningependa kufahamu nini hasa sababu ya wengi kukosea

1. Tazama: Neno hili watu wengi sana wanakosea kulitamka, wengi utamka "Tizama" kwa nini?
2. Thibitisha: Neno hili watu wengine utamka "dhibitisha" sababu nini?
 
Sababu ni kuathiliwa na lugha mama ya kienyeji mtu aliyezaliwa nayo.
Kazi.....kasi
Ramani....lamazi
Dhiki....ziki
 
Iko shida kwenye matumizi ya R na L, sehemu ya R inawekwa L.

Arusha- Alusha
Morogoro- Mologolo
 
Back
Top Bottom