Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Katika taifa letu siku za hivi karibuni, watu wamekuwa wakiongelea kuhusu mabadiliko.
Mabadiliko ndilo limekuwa neno ambalo liko katika vinywa na mioyo yao. Watu wamekuwa wakiliongelea kwenye vijiwe na katika mitandao ya kijamii, lakini pia vyama vya siasa vimekuwa vikiongelea neno hili.
Lakini mabadiliko ni nini? Na ni nini mahitaji ya mabadiliko? Ni vitu gani tunahitaji kubadili? Ni watu gani wanapaswa kubadilika na kwasababu gani?
Je Kubadili serikali peke yake kunaweza kuleta mabadiliko ambayo watu wana hamu nayo? Ni nini nafasi ya wananchi kwenye mabadiliko je hawapaswi kubadilika?
Watu wanaongelea kuhusu mabadiliko lakini ukiwasikiliza kwa karibu hawajui haswa kipi wanachohitaji na matakwa ya mabadiliko.
Mimi mwenyewe nahitaji kujibadilisha kwanza tabia yangu inahitaji kubadilika. Kisha nitakuwa na haki ya kusimama na kudai mabadiliko ikiwa nafsi yangu haina tone ya wizi na ufisadi au tabia nyingine haribifu kwa jamii. Kuna mahitaji pia ya kufuata sheria za nchi na kuzitii ni wangapi tunazifuata?
Kitu cha msingi ambacho wengi hawakijui huwezi kutoa usichokuwa nacho.
Na mahitaji ya kutenda haki katika nchi yeyote ile yanamhitaji mtu aliyeonyesha matendo yasiyo shaka katika kusimamia na kutoa haki na usawa kwa wote. Mtu asiyetenda haki na mlafi atawezaje kutoa haki ambayo hana katika nafsi yake na maisha yake yameonyesha hivyo kwa kudhulumu, kudanganya na kuibia watu? Kwa kupendelea jamii yake na familia yake? kwa kujilimbikizia mali?
Matakwa ya mabadiliko yanakuhitaji wewe kwanza ubadilike. Jiulize kwanza wewe ni raia mwema ? na una timiza wajibu wako kikamilifu kama raia? Unafanya kilicho sahihi na sawa kwa nchi yako na kwa raia wenzako?
Ukweli ni kwamba kama wewe unaiba katika ofisi yako ndogo uliyopo sasa hivi, ukipewa ofisi kubwa utaiba . Na hivyo wewe hufai kuwepo miongoni mwa watu wanaodai mabadiliko. Unapaswa kubadilika wewe kwanza. Na ndipo unyanyue sauti na kusema nahitaji mabadiliko!
Kama sisi ni wa kweli kabisa tunapaswa kuchunguza tabia zetu kama ni zenye faida kwa taifa kisha tubadilike. Mabadiliko yako binafsi hayahitaji serikali kuondolewa madarakani. Ni jukumu lako kuchukua hatua kama unalipenda taifa hili.
Tuanze kubadilika sisi kwanza katika sehemu tunazofanya kazi, katika familia zetu na katika jamii zinazotuzunguka. Tusijidanganye kwamba hatuhitaji mabadiliko hayo. Mabadiliko ya kweli yanaanza na mtu binafsi huwezi kubadilisha taifa kama wewe hujabadilika. Huo ndio ukweli.
Mwizi anayedai mabadiliko kwa kuhitaji kwenda ikulu anataka kwenda kuiba tu. Kwahiyo kuna umuhimu wa kuangalia tabia za watu wanaosema wanahitaji mabadiliko. Ukweli ni kwamba wengi wao hawana nia ya dhati. Wanataka kwenda ikulu kwa faida zao binafsi, wanataka ubunge kwa faida binafsi. Wanafanya kila wawezalo wapate vyeo.Hakuna ukweli ndani yao.
Kubadilika kwa watu wanavyofikiri na kutenda ndio mabadiliko ya kweli. Tumekuwa tukitenda na kufikiri vile vile hakuna kilichobadilika kwenye tabia zetu kwa miaka sasa. Na hatuwezi kubadilika kwa fikra na matendo yale yale. Ni lazima na muhimu kubadilisha njia na kufuata njia nyingine. Na hii inahitaji mabadiliko ya fikra kwa watu walioko serikalini na kwa wananchi.
Kama hatuendelei katika kasi inayotakiwa ingawaje tuna kila kitu ambacho kinaweza kutuwezesha kuendelea tuna matatizo kwenye fikra zetu. Tunapaswa kujiuliza kwanini? Tuna watu zaidi ya millioni arobaini na tano na tuna ardhi na maliasili kibao.Tunapaswa kujua kuna kitu ambacho tunapaswa kubadili. Lakini pia tunaweza kujiuliza kujitolea kwetu kwa taifa hili ni kwa kiwango gani ili tuweze kuongeza juhudi zaidi.
Kuna mambo mengi ya kimsingi ya kujadili kama tunataka kulibadili taifa hili. Hasa kujenga uaminifu wa watu wetu kwa taifa lao. Kwasababu pasipo uaminifu taifa hili haliwezi kusimama. Ni lazima tuwajengee kujitambua na kuwa na raia wenye dira na malengo kwa taifa lao. Hatuwezi kuendelea kama tutakuwa na raia wasiokuwa na dira kwa taifa lao. Wananchi wetu ni lazima wawe na dira. Wajue kwanini wanaishi na kwanini wako katika taifa hili la Tanzania. Ya kwamba wana kitu wanapaswa kujenga na wana mission wanapaswa kuitimiza.
Na hili jambo sio kwamba haliwezekani, linawezekana tuna uwezo wa kuwa taifa kubwa kama taifa lingine lolote. Lakini kuna mahitaji ya kuwa taifa kubwa.
Taifa kubwa haliji hivi hivi. Taifa kubwa halishuki kutoka angani. Tunapaswa kujitolea na tunapaswa kuamini kwamba tunaweza kuwa taifa kubwa.
Tunapaswa kuwa na malengo na kujua kwamba jukumu la kujenga taifa hili sio la kizazi hiki tu hivyo kuwatayarishia misingi kizazi kinachokuja. Na tujue kwamba siasa za tumbo na za ulaghai haziwezi kujenga taifa hili bali zitaliuza taifa hili. Siasa za namna hii hujenga wasaliti na mapandikizi na watu wasioaminika na mandumila kuwili. Ambao hakuna kilichowapeleka kwenye siasa bali matumbo yao. Wao wasio na mission wala malengo ya juu.