Matajiri wanalipa kodi ndogo

Matajiri wanalipa kodi ndogo

researcher12

Senior Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
160
Reaction score
164
Watu wenye utajiri wa kupindukia ndio wanaolipa ushuru wa chini zaidi duniani, ripoti iliyotolewa na shirika la Oxfam imesema.
“Idadi ya mabilionea imeongezeka licha ya mfumuko wa bei huku mapato yao yakipanda kwa dola bilioni 2.5 kwa kila siku. Licha ya hiyo, mabwenyenye na mashirika tajiri wamelipa kiwango cha chini zaidi ya kodi katika kipindi cha miaka kumi zilizopita,” ripoti hiyo imesema.
“Katika mataifa tajiri, kodi inayotozwa mapato ya kibinafsi ilipungua hadi 30% mwaka wa 2013 kutoka 62% mwaka wa 1970. Katika mataifa yanayoendelea, kodi ya mapato ya kibinafsi ni 28% kwa wastani,” shirika hilo limesema. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utajiri wa dunia unamilikiwa na mabilionea 26 ambao thamani yao inalinganishwa na thamani ya watu maskini bilioni 3.8 kwa pamoja kwote duniani. Hii ni licha ya watu bilioni 3.4 ambao wangali wanaishi chini ya dola 5.5 kwa siku.
Source; China Xinhua News
 
Sio kwamba wanalipa ela ndogo, anajua mianya ya mifumo ya kodi na wanaitumia katika kuhakikisha either wanakwepa au wanalipa kidogo..

Siku zote mfanyabiashara makini ni yule anayejua jinsi ya kukwepa kodi bila kuvunja sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko Tanzania au wapi ndugu?
Tafuta mtu kueleweshe maana ya VAT value added tax analipa nani?
Pay as you earn analipa Nani?
Investors wana tax exemption nyingi Sana na wameajiri makonsultant wa kodi hivyo pambana uwe tajiri ujitoe kwenye hicho kifungo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So ukiishi chini ya $5.5 wewe ni maskini?

nadhani Tz nzima 75% ya wananchi ni maskini sasa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom