Maswali yangu kwa rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali yangu kwa rais Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpayukaji, Dec 2, 2011.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Pesa imemwagwa ausiri za Jakaya zimefichuka kiasi cha CCM kuamua kuyamaliza kifisadi. Kimsingi,tumenufaika kujua kuwa kumbe Richmond ni wawili yaani Lowassa na Jakaya Kikwetewanaomtumia mwarabu wao wa Igunga. Hata siri ya kutotaka Samuel Sitta aendeleekuwa spika imefichuka. Maana kama siyo hili ngigi lao bunge lingekaa nakujadili mambo yafuatayo:
  1. Nani alikuwanyuma ya Richmond? Je ni wote yaani Kikwete na Lowassa au mmojawapo ambayealitaka kumtumia mwenzake bila kujua?
  2. Kwanini Kikwetealimzuia Lowassa kuvunja mkataba wa Richmond kama hakuwa na maslahi binafsi?
  3. Kwanini rais nawaziri wake mkuu walilidanganya bunge na taifa kama hawakuwa na lolote bayanyuma ya kadhia hii?
  4. Kwanini wawilihawa wasichukuliwe hatua haraka hasa ikichukuliwa kuwa nchi imeishaathirikasana tokana na miradi yao hii?
  5. Je baada yaukweli kubainika Kikwete anatoa utetezi gani unaoingia akilini?
  6. Baada ya ukwelikujulikana, katiba na watanzania wanasemaje?
  7. Kama raisanaweza kudanganya umma na kupinda sheria kwa maslahi binafsi anafaa kuendeleakuwa rais.
  8. Kwaniniserikali ya Kikwete imekuwa nyepesi kulipa Dowans ambayo ni Richmond badala yakuwachukulia hatua walioigiza kampuni la Richmond kinyume cha sheria kama kwelirais ahusiki?
  9. Je kunamgongano wa kimaslahi na uvunjaji wa katiba?
  10. Je suala laufisadi na uchafu wa Kikwete na Lowassa ni suala la CCM au taifa?
  11. Je ni vizurikuanza hatua za kumu-impeach Kikwete ili kuepuka miaka minne iliyobakia kuzidikuizamisha nchi kwenye umaskini usio na sababu?
  12. Je Kikweteatalimalizaje hivi na abaki salama?
  13. Je taifa namamlaka ya urais viko salama mikononi mwa mtu kama huyu anayetia kila aina yashaka?
  14. Urafiki wakweli si wa barabarani kama ambavyo Lowassa amekuwa akitaka tuamini?
  15. Je kama kweliurafiki wa Kikwete na Lowassa si wa barabarani ni kwanini Lowassa hakupata mudawa kumueleza Kikwete alichokuwa akipanga kusema juu yake hadi amstue hivyo?
  16. Je urafiki waKikwete na Lowassa sasa umefikia mwisho?
  18. Je wawili hawawalisuka hili zengwe ili kuokoana wakijua wazi kuwa mmoja yaani Kikwete ahitajikugombea tena wakati mwingine Lowassa akitaka sana urais?
  19. Je kweli badoLowassa ana udhu wa kuweza kuwa rais wa taifa hili asizidi kulipelekea kuzimunikama rafiki yake?
  20. Je ni rahisiwatanzania kusahau kiza alichowaweka Lowassa na rafiki yake kutokana na“biashara” yao ya Richmond na Dowans ukiachia mbali mazabe mengine?
  21. Je Kikweteamejifunza kuwa kushiriki au kulinda ufisadi si mbinu salama kwa mhusika maanawanapozidiwa, watuhumiwa watakutaja tu?
  22. Je kwa mazabena mauzauza haya wahusika nao wamejiridhisha kuwa wametatua tatizo auwameliahirisha ili siku nchi ikipata utawala makini wajikute korokoroni?
  23. Je maneno yaLowassa yalilenga kumtisha rais Kikwete ili amlinde?
  24. Kama lengolilikuwa ni kumtisha rais, je rais atachukua hatua zaidi au kunywea?
  25. Kama raisatanywea, haoni kuwa atazidi kujidhalilisha ukiachia mbali kujenga dhana kuwayeye ndiye mhusika mkuu wa uchafu wa Richmond?
  26. Je raisanayeweza kutishwa na watu binafsi tena wenye tuhuma za wazi anafaa kuendeleakuongoza taifa linalokabiliwa na maadui wengine wengi wenye nguvu kama vilewawekezaji wanaosaidiwa na mataifa yao?
   
Loading...