Maswali ya Watanzania kwa Mzee Lowassa

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,609
Baada ya kufuatilia hotuba yako ya ufunguzi wa kampeni za UKAWA jangwani kwa umakini mkubwa, naomba Mzee Edward Ngoyai Lowassa unisaidie mimi na wananchi wenzangu wa TANZANIA kujibu maswali haya;



  1. WANAMABADILIKO;
Watanzania wamechoshwa na Rushwa, wanachukia UFISADI, Mzee unamkakati gani dhidiya wala rushwa na mafisadi..?



  1. MAMA NTILIE;
Kilio chetu ni juu ya mgambo kutusumbua na mazingira mabovu ya biashara,tukakulalamikia bei kubwa ya vyakula na mazao, jibu letu liko wapi..?au atakuja kutujibu Babu Seya ukishamtoa jela..?



  1. MADALADALA;
Mzee tulikubeba kutoka Masaki mpaka Gongo la mboto, njia nzima tukikueleza kero zetu, Hatujakusikia ukisema kitu kuhusu usumbufu wa Traffic na kutunyang'anya leseni zetu..?



  1. WAKAZI WA DAR;
Mzee tumekupa mapokezi ya kufa mtu, lakini unajua kuwa tumeamka saa kumina moja alfajir ili kuwahi mkutano wako wa saa tisa Jangwani, Tatizo la foleni na shida ya Usafiri haujazungumzia kabisa...Mzee umetusahau..?



  1. WANAFUNZI;
Elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, sawa ila Mzee kwa mapato gani..? Au ndio muendelezo wa maigizo..?



  1. WACHUMI;
Sarafu yetu imeendelea kushuka kwa kasi ya ajabu, imetoka kuwa hela ya madafu imekuwa hela ya pipi, Mzee na hili nalo umelisahau..?



  1. WANASHERIA:
Nini maana ya utawala wa sheria unaouzungumzia..? ipi haki ya watoto waliolawitiwa kinyume na maumbile na Babu Seya na Wanawe, au Mzee unaujua Ukweli ambao hautaki kutuambia..?





  1. WAZANZIBARI;
Ni upi msimamo wako na maoni yako juu ya Katiba inayopendekezwa..kuwa Muwazi..?
MZEE hauoni tofauti ya maisha ya Wazanzibari kabla na baada ya kufungwa kwa Farid na Kundi lake..? Mzee amani imerudi Zanzibar au tuambie mahusiano yako na UAMSHO..?



  1. WAGONJWA;
MZEE watanzania wenzako tunaumwa Mzee..,Nini Hatma ya Afya za Watanzaniaau WEWE mwenzetu sio mgonjwa..?



  1. WANAMABADILIKO;
MZEE tuliahidiwa SLAA atahudhuria jangwani na kuipa nguvu mpya kasi ya mabadiliko, Mzee mlimsahau au ilikuwa ni Changa la macho..?



  1. VIJANA;
MZEE ulisema tatizo la ajira ni bomu, ila hatujakuelewa, ina maana umetuacha tulipuke au mkakati wetu uko kwa Balal..?



  1. WANAKIJIJI;
MZEE umetukomoa au umefanya kwa bahati mbaya kutuwekea hotuba yako kwenye Intaneti, haujui zaidi ya watanzania asilimi 80 hawajui kitu kinaitwa Intaneti..?



  1. WATUMISHI;
MZEE, mishahara yetu haikidhi mahitaji, gharama za maisha ni ghali mno..mbona hatujakusikia ukitutaja, au sisi ni mpango wa kando..?



  1. WACHUMI;
MZEE, nini hatma ya mchumi mwenzetu Prof Lipumba katika genge la wanamabadiliko, au umemchukua TAMBWE Hizza Mhitimu wa darasa la saba kuwa mbadala..?
 

😀😀😀😀😀😀 unaandika lakini....au ndo certified LOFA
 

Nianze kama ulivyomaliza..kwa kujibu salamu yako iliyotukuka ya Chama kitakatifu cha CCM, Kidumu Chama Tawala.

Kwanza nikukumbushe jambo, hakuna sehemu imetajwa wala kuzungumziwa UKAWA kwenye thread yangu, labda haujaisoma ama haujaielewa, lakini thread hii imemtaja na kumzungumzia MZEE LOWASSA na ni Mzee LOWASSA pekee..

USHAURI:
Kabla ya kuandika comment yeyote, hakikisha umesoma na kuelewa kile unachotaka kukichangia.
 
YAANI CCM MNAHANGAIKA NA LOWASSA NA UKAWA HADI MNAMSAHAU MAGUFULI WENU,hahaha...Lowassa anawanyima usingizi,poleni sana
 

Haunijui na haitatokea ukanijua..mimi sijulikani na MALOFA..

Unajua umeanza kinafiki uka-comment kama mwanaCCM, kumbe kimsingi we ni lofa unayejifananisha na watu wema wa zama hizi (wanaCCM)

UKAWA ndio LOWASSA na LOWASSA ndio UKAWA...Hii ni ajabu Kuu, natamani nipate fursa ya kumuuliza Mzee LOWASSA swali la nyongeza baada ya Maswali hayo ya watanzania hapo juu..

Nikipata fursa nitamuuliza Mzee, MAANA YA UKAWA ni nini..? naamini MZEE atachemka hilo swali..
 
YAANI CCM MNAHANGAIKA NA LOWASSA NA UKAWA HADI MNAMSAHAU MAGUFULI WENU,hahaha...Lowassa anawanyima usingizi,poleni sana
Magufuli alikuwa NJOMBE jana anazungumza na Watanzania wenzake wasiojua kutumia WEBUSAITI, nyie mlikuwa jangwani na MAWEBUSAITI yenu...

Kwa kuwa na mimi nilikuwa jangwani pia kumsikiliza Mzee, nikaona niwaulize maswali hayo ambayo nimeyasikia pia kwa Watanzania wenzangu wakitaka kufahamu..
 
 unaandika lakini....au ndo certified LOFA

Hope wewe ndio bingwa la lofa nyanya kabisa usie tiwa ndimu ukanona
kipi wewe unachoona sio sahihi hapo? mda mwingine sio unapinga tu bila kushirikisha ubongo nini wewe lowasa alichokufanya mpaka ukamwamini atakuletea mabadiiko ama ndio wafata mkumbo tu.
Mda mwingine tuwe tunashirikisha ubongo kama mabadiriko unayataka nenda kongo ama burundi sisi hapa tunataka maendeleo ya Dr Magufuli
 

mwanadamu amepewa utashi wa akili wenye vionjo vya hisia kupenda na kujiskia sehemu ya kitu fulani wewe sio jiwe uweke wazi kuwa wewe ni lofa na pumbavu tu unayeshinda kuelewa msulupwete ulioung'ang'ania utakuvuka muda na wakati wowote !
 

Naomba nianza na wewe na wasiwasi na elimu yako kwanza kama umeipata tanzania mana asilimia 90 ya waliopata elimu tanzania sio mbulura kama wewe huwez sema eti umekichoka tu chama unataka ubadilishe unazani nchi ni kama nguo kwamba utabadilisha kila mda? hiyo sio fact ya kuongea mbele ya jukwaa hili maana wanakuona chizi tu toa sababu za wewe kutaka kubadilisha chama akam huna nenda kakojoe usubili chai.
 

Inasikitisha ninapoona watu munataka mabadiliko lakini mukiulizwa mabadiliko gani munataka eti CCM itoke madarakani basi mumemaliza…!!! Sasa mbona kama hamjui mnachotaka…!!! Kuondoka CCM madarakani ndio kumepunguza maisha magumu mwa watanzania? Ndio kumeondoa kero za muungano, ndio wananchi wamepata maisha bora? Ebu tujitafakhari walau kidogo basi.
 
YAANI CCM MNAHANGAIKA NA LOWASSA NA UKAWA HADI MNAMSAHAU MAGUFULI WENU,hahaha...Lowassa anawanyima usingizi,poleni sana

Hakuna mtu anaehangaika na lowasa_fisadi ila shauku yetu ni kutaka watanzania watambue lowasa_feki ni kidudu mtu anaetaka kujifanya kondoo msafi wakati ni mkaaa mweusi
ata maandiko ya vitabu vya dini vinasema ukimwona mtu anapotea na ukamwacha usimwambie iliyo kweli basi hata wewe umetenda dhambi
 

Na je Mzee wa ESCROW, NGELEJA,TIBAIJUKA NA CHENGE?
 
kama ameshindwa kusiamama na kutoa sera.....na kujibu maswali hapo juu yaliotajwa....katika mikutanio mikubwa kama ya UN atafanya nini.....aibu itakua ni ya tanzania nzima sio.....ukawa wala CCM...akili kumkichwa
 
Jamani huyo binti yupo? Wamemtupa sasa, anasema maswali ya watanzania au sijamuelewa? Watanzania wapi wamtume huyo kuwaulizia maswali? Aseme maswali yako kwa Lowasa sio wtz acha kutujumlisha kwenye .......wako.
 
Babu Seya wakati analawiti ulikuwepo, name unajua ushahidi gani ulipelekwa mahakamani, unajidhalilisha.
 
Umoja wa Katiba ya Wananchi. Labda na wewe ulikuwa hujui.
 


Kwani aliyetoa post ni mwana CCM au mwananchi wa kawaida? Kwa upande wangu haya ni maswali ya msingi kujua majibu yake, jana ndugu EL alisoma hotuba lakini sikuielewa yampasa afafanue kiundani zaidi, tunataka mabadiliko lakini ni mabadiliko yapi?
 
hawezi kujibu hayo maswali anchoweza kusema ni kumrudisha Balali, kuwatoa mashekh, kumtoa babu Seya.Kweli ametuona malofa na wapumbavu, lakini nakubali anayohaki yakutuona hivyo kwasababu tulishangilia.
 
YAANI CCM MNAHANGAIKA NA LOWASSA NA UKAWA HADI MNAMSAHAU MAGUFULI WENU,hahaha...Lowassa anawanyima usingizi,poleni sana

Mimi nadhani kuna haja ya kuzipima akili zetu, maan tunaona lakini hatufahamu. Tunaacha kuyafikiria mambo ya msingi na kupata majibu ya maswali haya, tunaleta ushabiki. K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…