Maswali ya msingi kwa tume ya warioba

Maswali ya msingi kwa tume ya warioba

von Meshak

Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
12
Reaction score
3
1. Ikiwa Rasimu ya pili iliyoandikwa na TUME
YA WARIOBA ndio maoni ya wananchi na
iliandikwa kwa ustadi mkubwa na wataalamu
wa masuala ya uandishi wa katiba na wenye
uzoefu ilipelekwa bungeni kufanya nini?

2. Ikiwa muundo wa Serikali 3 ni
mapendekezo ya wananchi japo idadi ya
waliotoa maoni hayo haikuwa kubwa
ukilinganisha na waliotaka mahakama ya
KADHI kwanini uliuweka muundo huo na
mhakama ya KADHI hamkuiweka au
hayakuwa maoni ya wananchi, na ikiwa
mliona yanaweza kuleta mtafaruku kidini,
kwanini mliweka muundo wa serikali 3 ikiwa
nao mlijua utaleta mtafaruku? Au yale maoni
yaliyotolewa ya kuwepo mahakama ya kadhi
yalikuwa sio ya wanchi? Na yawananchi ni
yale ya muundo wa serikali 3?

3. Wapo ambao hawakutaja muundo wa
serikali ila mkasema eti kwa namna
walivyokuwa wakitoa maoni yao mliona
kabisa muelekeo wao ni waserikali 3, hivi
mlikuwa na kipaji gani cha kujua kilicho
kichwani kwa mtu aidha serikali 3 au 4 nk?

4. Kwanini mnalazimisha wananchi waipende
rasimu mliyoiwasilisha ninyi, na utashi wa
kweli ni upi kwa mwananchi, ni juu ya rasimu
mliyoitoa nyinyi au iliyorekebiswa na BUNGE,
na kama ni hivyo nani mwenye uhalali wa
kusema hii ndiyo ya wananchi ikiwa
wananchi wenyewe ni sisi, na mwananchi
yupi ambaye huesabika huyu ndie
mwananchi halali wa kuipitisha katiba na
wale watakao ikubali sio wananchi, na kama
sio wananchi wanaruhusiwa kupiga kura ya
maoni hayo?

5. Kwanini unapinga uwepo wa baraza la
vijana inamaana hupendi vijana wawe na
baraza? Ulitaka wawe na kaibara kamoja
kama ...............

6. MWISHO tambua wapo wanaoamini na
kuiona RASIMU ya WARIOBA ndio nzuri kwao
na wapo wanaiona KATIBA
INAYOPENDEKEZWA ya CHENGE ndio nzuri
kwao. Kamwe wanaadamu hawawezi kuwa
na muono wa aina moja.
 
JK katuletea janga kwa kuvamia Ilani ya watu sasa tunatoana macho......mpk Hao jamaa watoke huko dodoma tutasikia mengi.
 
hivi wewe jiulize ile tume ilissheeni magwiji mbalimbali wa sheria, tena mpaka wa taalamu wa katiba, wakatoa na kitu ambacho kilikuwa na tija kwa taifa, wewe unakuja kukaa siku 2 mezani na kutuandikia rasimu eti kamati maalumu ya uandishi. hayo maswali yako kawaulize watoto wanaosoma uraia darasa la 3 watakujibu lakini si tume kujisumbua kukujibu.
 
Warioba mwache aende barabarani akapate aibu waliyopata mawakala wake wa CHADEMA
 
hivi wewe jiulize ile tume ilissheeni magwiji mbalimbali wa sheria, tena mpaka wa taalamu wa katiba, wakatoa na kitu ambacho kilikuwa na tija kwa taifa, wewe unakuja kukaa siku 2 mezani na kutuandikia rasimu eti kamati maalumu ya uandishi. hayo maswali yako kawaulize watoto wanaosoma uraia darasa la 3 watakujibu lakini si tume kujisumbua kukujibu.
Ni ujinga kufikiri kuwa katiba inatungwa na wataalam wa sheria. Katiba inatungwa na wananchi moja kwa moja ama kwa kutumia wawakilishi kama hawa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba japo UKAWA walisusa
 
... Hata Umpake Vip Matope Warioba, Wananchi Tuko Nyuma Yake, Nyie Kaeni Na Hiyo Toilet Pepa Yenu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Warioba anawatoa jasho hasa, uzi huu una harufu ya jasho hilo!!!!
 
von Meshak,

kwa heshima na taadhima naomba nimsaidie Mzee Warioba kujiba maswali yako. mimi ni miongoni mwa wale ambao tunaunga mkono rasimu iliyowasilishwa na Tume ya Katiba.

1. rasimu imepelekwa bunge maalum la katiba kwasababu sheria ya uandishi wa katiba mpya imeelekeza hivyo. sheria pia imeelekeza kwamba maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na tume ya katiba ni lazima yaheshimiwe. pia bunge la katiba halina mamlaka ya kubadili msingi wa rasimu iliyowasilishwa na bunge.

2. Tume ilielekeza suala la kadhi lishughulikiwe wakati wa uandishi wa katiba ya Tanganyika. Nadhani tume ilielekeza hivyo kwasababu suala hilo siyo la muungano. Zanzibar tayari wana mahakama yao ya Kadhi bila kuhusisha serikali ya muungano.

3. Kwanza Tume ilielekezwa kwamba lazima udumishe MUUNGANO. Sasa ktk mazingira hayo ikitokea mtoa maoni akapendekeza kuwe na Raisi wa Tanganyika, au bunge la Tanganyika, huyo moja kwa moja kwa kuzingatia hadidu rejea za Tume ya Wariona ataangukia ktk waliopendekeza muungano wa serikali 3.

4. Wajumbe wa Tume ya Warioba wana haki ya kutetea rasimu yao. Wabunge wa bunge maalum ya Katiba nao wana haki ya kutetea rasimu yao. Lakini wote wanatakiwa kutetea rasimu zao kwa weledi na lugha za kistaarabu. Hakuna mwenye haki dhidi ya mwingine. Mwamuzi wa mwisho kuhusu suala hili ni wapiga kura wa Tanzania. Lakini wapiga kura wanatakiwa kufikia maamuzi baada ya kusikiliza kwa makini hoja za pande zote.

5.Binafsi sioni mantiki ya kuwa na baraza la vijana la taifa. Sidhani kama tunahitaji baraza lolote lile la taifa kwa kuzingatia vigezo vya rika au jinsia. Kwa msingi huo siungi mkono baraza pia uwepo wa baraza la wanawake, watoto, wazee, etc etc.

6. Serikali ingezingatia ushauri wa kambi ya upinzani, kama ulivyowasilishwa na Tundu Lissu, kwamba iitishwe kura ya maoni kuhusu suala la muungano na idadi ya serikali kabla ya kuanza uandishi wa katiba, hakika tusingetumbukia ktk mkwamo huu. Kwasababu watawala walikataa ushauri huo mzuri, ndiyo maana zoezi hili limeingia "ukakasi" wa malumbano kati ya wajumbe wa Tume ya Warioba, na wajumbe wa bunge la Katiba.
 
Last edited by a moderator:

Heko sana mkuu..haya majibu ni zaidi ya hata atakayopata kwenye tume
 
Kamwe Tume (WAJUMBE 30) haiwezi kuwa juu ya BMK... (WAJUMBE 630: naundwa na Bunge la JMT, baraza la wawakilishi + 201 kutoka Makundi Maalamu ya jamii)...This will never happen on earth!!!
 
Katiba ni maridhiano ndugu yangu ! Ukiondoa hicho, matokeo yake ndiyo haya !

Hata kwenye tume nako baada ya kuyakusanya maoni na kuyachambua ilibidi kwa baadhi ya issues waridhiane ! Na katika maridhiano hayo ya tume, pamoja na kwamba kulikuwa na waislam wengi kwenye tume hiyo walipendekeza swala la mahakama ya kadhi liachwe kwenye nchi washirika !

Na kama kwenye BMK kungekuwa na maridhiano, wangeenda vizuri tu, pamoja na mambo mengine, wangeweza wakatafuta namna ya ku-accomodate concerns za waislam na za dini nyingine vile vile - kama walivyofanya tume !

Sasa kwa sababu ya upuuzi wa CCM wa kutokukubali maridhiano, ndio tumefika hapa - tuna Rasimu mbili !

Na kama ulivyosema kwenye point yako ya sita, kuna wanaikubali ya Sitta na wengine ya Warioba !....Sasa kwa sababu, sasa hivi imekuwa mashindano, hivyo inabidi hizo mbili zishindane kwa wananchi na wananchi wataamua ipi ni ya kwao !

Sisi tunayoikubali ya Warioba tutaipinga ya Sitta (kwa sababu kwa mujibu wa sheria ndio itaenda kwa wananchi) na wale wanaikubali wataipigia kura ya Ndio na hapo ndio wote tutajua ni ipi hasa ni rasimu ya wananchi.....

-----------
6. MWISHO tambua wapo wanaoamini na
kuiona RASIMU ya WARIOBA ndio nzuri kwao
na wapo wanaiona KATIBA
INAYOPENDEKEZWA ya CHENGE ndio nzuri
kwao. Kamwe wanaadamu hawawezi kuwa
na muono wa aina moja.
 
Kamwe Tume (WAJUMBE 30) haiwezi kuwa juu ya BMK... (WAJUMBE 630: naundwa na Bunge la JMT, baraza la wawakilishi + 201 kutoka Makundi Maalamu ya jamii)...This will never happen on earth!!!

usitokwe na povu pitia sheria ya mabadiliko ya katiba iliyoweka vyombo hivi viwili na mipaka yake
 
Ni ujinga kufikiri kuwa katiba inatungwa na wataalam wa sheria. Katiba inatungwa na wananchi moja kwa moja ama kwa kutumia wawakilishi kama hawa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba japo UKAWA walisusa

kwa hiyo tume ilikuwa ya nini? jaribu kushirikisha ubongo wako katika kuandika
 
usitokwe na povu pitia sheria ya mabadiliko ya katiba iliyoweka vyombo hivi viwili na mipaka yake

Unasema kweli...

BMK iko Juu ya TUME,

WANANCHI wako JUU ya BMK

Ndio maana wa Mwisho Ana-Approve the long written document ni MWANANCHI...
 
Na ndio maana Warioba amewaambia wajumbe wa BMK waje watetee hoja zao kwa wananchi na yeye pamoja na wajumbe wengine wa tume wataendelea kutetea za kwao kwa sababu ndizo wanaamini ni za wananchi and then wananchi wataamua ni nani aliye-represent interests zao !

Mbona ni utaratibu rahisi na fair sana !

Unasema kweli...

BMK iko Juu ya TUME,

WANANCHI wako JUU ya BMK

Ndio maana wa Mwisho Ana-Approve the long written document ni MWANANCHI...
 
kwa hiyo tume ilikuwa ya nini? jaribu kushirikisha ubongo wako katika kuandika
Product ya Tume ya Katiba =-Constitution Draft 2 (Rasimu ya Warioba). Kazi ya BMK iliyotumika kuandaa Katiba inayopendekezwa- Proposed Constituion !

Kama ulikuwa hujui Kazi ya Tume ili fanyika na ndio ilifikisha hapa tulipo!
 
Back
Top Bottom