Maswali ya Awali

Maswali ya Awali

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Pongezi kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh.Dr.Shukuru Kawambwa kwa kutekeleza maagizo ya 'Kiti cha Spika' wa Bunge la JMT kuwasilisha Mitaala ya Elimu Tanzania kwa wakati.Imewasilishwa Mitaala ya aina tatu: ya hule za Chekechea,Shule za Msingi na Shule za Sekondari.Lakini,ya Vyuo vya Ufundi Stadi sijaisikia.Sijui kwanini.Amewasilisha tarehe 6/2/2013 kama ilivyoagizwa. Kamati ya Bunge imepewa wajibu wa kuichunguza na kujiridhisha juu ya uhalali wake na uimara(labda!).Vyema sana.

Sasa maswali:

1. Mitaala hii ilikuwepo?

2. Walimu na wanafunzi nchini wanaijua?

3. Ilikuwa inatumika ipasavyo?

4. Mh.Mbatia alifanya utafiti wa kutosha?

Kwa mwana-JF yeyote anayejua jibu au majibu ya swali/maswali haya anisaidie. Karibuni!
 
Back
Top Bottom