Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 588
- 1,698
Je, Kassim Majaliwa ni Waziri Mkuu? Jibu ni HAPANA
Waziri Mkuu, mawaziri na naibu mawaziri leo wamefikia kikomo cha uwaziri wao. Asubuhi ya leo waliamka wakiwa mawaziri, lakini kabla ya mchana wakawa si mawaziri tena. Kikatiba leo Baraza la Mawaziri limevunjika automatically. Si mawaziri tena. Uwaziri unakoma ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais, yaani kuapishwa. (Ibara 57(1)(f)). Kwa hiyo viti vyao viko wazi kuanzia leo.
Je, Job Ndugai ni Spika wa Bunge? Jibu ni NDIYO
Job Ndugai bado ni Spika wa Bunge ingawa bunge jingine halijaanza baada ya kuvunjwa kwa lile lililomaliza muda wake. Ingawa Majaliwa amekoma kuwa waziri, Ndugai bado anaendelea kuwa Spika wa Bunge pamoja na kwamba Bunge lilishavunjwa zaidi ya miezi minne iliyopita. Kwanini?
Kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Ndugai anaendelea kuwa Spika wa Bunge hadi Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanywa baada ya Bunge kuvunjwa (Ibara ya 84(7)(c)). Kwa hiyo Ndugai bado ni Spika hata baada ya Rais mteule kuapishwa.
Kwa maneno mengine, Ndugai atakoma kuwa Spika wa Bunge siku ile Bunge linakutana kwa mara ya kwanza baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu.
Leo Rais atamteua mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria, na huyo atatajwa tu kwa kifupi kama "Mwanasheria Mkuu". Tutatajiwa jina. Kabla ya Novemba 19 tutakuwa tumeshatajiwa jina la Waziri Mkuu. Je, atakuwa ni Kassim Majaliwa? Jibu langu lolote kwa swali hili ni la kubahatisha.