Maswali tatanishi kuhusu nchi huru ya Tanzania

Nfumu

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
610
698
Moja kati ya vitu ambavyo jamii kubwa ya viongozi na wasomi wa Tanzania wameshindwa kuvitolea ufafanuzi kuanzia mwalimu Nyerere ambaye alikuwa muasisi wa taifa hili la Tanzania mpaka viongozi wa sasa nakubakia kuwa vitu tatanishi, nimeamua kuyaleta forum ili tufanye discusion mambo yafutayo;

1.Je ni kwanini bendera na katiba ya Tanzania na Zanzibar ni tofauti wakati Zanzibar ipo ndani ya Tanzania? je muungano una maana gani?

2.Kwanini makao makuu ya nchi huru ya Tanzania yapo DAR ES SALAM ikiwa pamoja na Ikulu takatifu ya rais na isiwe katika mji mkuu wa Tanzania DODOMA, je bunge tu ndio makao makuu ya Tanzania?

3.Je ni kwanini tunaazimisha Tanzania kama nchi huru tarehe 9 /12 kila mwaka na wakati Tanzania ni muunganiko wa nchi huru mbili ambazo zilipata Uhuru siku tofauti, Je ni Tanganyika au Tanzania ilipata Uhuru vipi kuhusu Zanzibar?

Vipi Kuhusu sherehe za muuangano na jina la Tanzania.

4.Ni kwanini Tanzania tunatumia kingereza kama lugha ya kufundishia wakati watoto wakirudi nyumbani wanatumia kiswahili kama lugha kuu ya mawasilino?

5.Kwanini ofisi na ngazi zote za kiserikali wanaandika ripoti kwa kingereza na sio kwa kiswahili.
-je umuhimu wa lugha ya kiswahili uko wapi?

6.Kwanini vijana wengi wanaomaliza elimu ya chuo kikuu hawawezi kujiajiri pindi wanapokosa ajira, je mfumo wa elimu ndio mbovu
ama walimu ndio wabovu.

Wakuu tufanyeni discussion with opinion to our country.
 
Mkuu ukifuatilia mambo ya nchi hii utakuwa mwehu.
MUHIMU
Zingatia ugali wako kwa kutumia busara za kimishionari:)
 
Bunge linaendeshwa kwa kiswahili huku miswaada inaandikwa kwa kiingereza
shangaa hilo
Na huyu ndio King wa nini sijui. Anaweza kuwa mbunge wakati wowote wenye chama chao wakiamua.

14583262_1631430723818087_5764764495498969088_n-jpg.464065
 
Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na maajabu ya kisiasa uyu jamaa akiwa member of Parliament.
 
Sawa-sawa!!!

Ujanja-Ujanja ulianza toka Enzi hizo!!

Ukitafakari vizuri utagundua ni Ujanja-Ujanja!!!
Nchi imekaa ki Ujanja-Ujanja!
 
Tanzania haijawahi kupata uhuru, huu muungano ni koti tu la kuitawala nchi ya zanzibar.
 
Achana na hayo mambo mkuu....

Njaa ipo njiani inakuja umejiandaa vp?!
 
Back
Top Bottom