Philip Dominick FDF ni Football Development Fund.Huu ni mfuko maalum uliobuniwa na TFF ili uwe kiungo kati ya TFF na wadau katika kukusanya rasilimali za kuendesha program za mpira wa watoto,vijana na wanawake.Mfuko huu uanzishwaji wake umesimamiwa na Mwenyekiti mwanzilishi Leodegar Tenga,Katibu Henry Tandau na wajumbe Epbraim Mafuru,Mh Zarina Madabida,Mh Tarimba Abbas na Mwenyekiti mstaafu wa klabu ya Simba Mzee Ayoub Chamshama.
Mfuko huu utahamasisha wadau mbali mbali kuchangia maendeleo ya mpira wa vijana,wadau hawa ni pamoja na Serikali,Halmashauri,makampuni binafsi na ya umma,taasisi za dini nk
Kumbuka as it stands today timu yetu ya Twiga stars inayoondoka weekend kwenda Zambia haina support zaidi ya TFF,program za vijana kwa ajili ya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 na 2019 hazina support yoyote,hivyo kuna haja ya ku mobilise resources kwa ajili ya mipango endelevu kama hii.