Jamal Malinzi
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 710
- 650
- Thread starter
-
- #561
Mr President Malinzi
Nimesoma kwa masikitiko makubwa saana jinsi swala la Yanga kupeleka timu ya vijana lilivyokuwa handled na TFF baada ya maagizo ya katibu wa CECAFA, Mr MUSOKE.
1) Mashindano yamepangwa katika wakati mgumu, kwa timu washiriki
2) Kama nia na lengo ni kuibua wachezaji, sasa kosa la Ynga ni lipi?
3) Inamuhusu nini MUSOKE kusema haiwezekani Yanga ije na kocha mwingine?
Rejea yote haya, ni fedheha kubwa jinsi TFF ilivyolishughulikia hili swala.
Afisa wa TFF, aliyeshiriki kutoa uamuzi na kuwapeleka AZAM, anastahili kusimamishwa kazi au Ajiuzulu, haiwezekani ifike Musoke aanze kuamua jinsi ya uendeshaji na ujenzi wa soka katika taifa letu.
Hii ni aibu kwa nchi, wewe kama Rais wa TFF, onyesha kutokubali kuingiliwa katika masuala ambayo hayana sheria.
Ni udhaifu pia wa uongozi wa TFF. 'Mtu akikuambia jambo la kipumbavu, nawe ukalikubali, anakudharau' (J. K.Nyerere, n.d.). CECAFA wamewaambia jambo la kipumbavu TFF kuwa Yanga hawana sifa ya kushiriki mashindano eti kwa sababu wanapeleka kikosi B huku TFF wakijua fika kuwa wale ni wachezaji halali wa Yanga. Kwa kitendo cha TFF kukubali upumbavu ule, CECAFA imewadharau kana kwamba TFF haina viongozi ndiyo maana CECAFA iliwataka TFF wawaandikie barua Yanga na wao kukaa pembeni nje ya tatizo. Nashangaa ni kwa nini viongozi wa TFF hawajaomba radhi hadi sasa kwa kukubali upumbavu ule. CC. Jamal Malinzi (Mkuu una utetezi gani katika hili?).
Baada ya Yanga kukataliwa Tanzania hatukuwa tayari kupoteza uwakilishi.
Kipaji Halisi hili la Yanga na cecafa siai kama federation we tried our best kuokoa situation na hili Yanga wanajua,walichoamua cecafa ndo hicho.
Malinzi
Naomba nitoe ushauri wangu kwa ajili ya kukuza mpira wa Tanzania
1. Kwanza idadi ya timu za premier ziongezeke ili wachezaji wacheze mechi nyingi zaidi
2. Kuanzishwe ligi nyingine ya timu za vijana za vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza na ligi hiyo iende sambamba na ligi kuu
3. Uongozi wa TFF utafute wadhamini na kuwe na makato ya asilimia flani katika mechi zote za premier ili kuendesha ligi ya vijana
4. Kuwe na mkakati maalumu wa kupandisha vijana kwenye premier kila mwaka kwenye usajili wa vilabu hii itatuwezesha kupata timu bora ya taifa na yenye uzalendo.
Naomba niambie kati ya haya lipi linawezekana na lipi haliwezekani na kwa sababu zipi mkuu?
Hapa kuna walakini inakuaje cecafa ikatae wachezaji walio na leseni zilizotolewa na chama cha soka cha husika na chama hicho hicho kishindwe kuitetea klabu husika!
ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
Anzisheni ligi za shule, kuanzia primary, kwa wilaya hadi taifa na mzi-fund team na waalim wa soka shuleni.
Vipaji vianze kuibuliwa kuanzia mtu anapoanza darasa la kwanza.
Bila hivyo, hata miaka 100 ijayo hamtafika fainali za Afrika wacha za Dunia.
Kinachotakiwa muwe na plan, iliyojaa uwazi na mapato na matumizi yanayoonekana wazi, na muweke board ya soka kila shule kutokana na hao hao wazazi na si watu kutoka TFF. TFF wawe wasimamizi tu wa hiyo plan na kutoa technical know how. Nakuhakikishia hakuna mtu ambae atakataa kusaidia team ya shule ya mwanawe.
Aaah, nione mjukuu wangu kavaa jezi ya shuleni kwao, halafu nisiwe fan wa hiyo shule? Na hapo ndipo mtakapotuona akina mama tukijazana viwanjani kuwa support watoto / wajukuu zetu. Fikiri.
Achaneni na haya mavilabu, yameshakuwa vituo vua ulaji na kujitafutia umaarufu na matajiri watashindana kuyaendesha, nyinyi mnatakiwa focus yote iwe primary schools.
Simple and achievable plan.
Nimebaki na maswali lukuki baada ya kusoma jibu hili toka kwa Rais wa TFF.Makoye Matale politics za mpira ukanda wetu ni zaidi ya uzijuavyo.
Mh kijiografi na kihistori tuna nafasi ya kuwa wanachama wa chama cha soka kusini mwa afrika COSAFA,na mara nyingi jamaa washatuinvite ktk mashindano lkn kwa interest za uongozi uliopita walikuwa wakikataa kushiriki,mh kama una nia ya dhati ya kukuza mpira wa nchi yetu ungekaa na wizara husika ili tujitoe cecafa na kujiunga COSAFA,hii nafasi iwapo km wangekuwa nayo kenya siku nyingi wasingekuwepo cecafa km walivyojitoa zambia na malawi,yote kwa yote mh itendee haki nchi yetu kwa kujitoa cecafa
Nimebaki na maswali lukuki baada ya kusoma jibu hili toka kwa Rais wa TFF.
Nimebaki na maswali lukuki baada ya kusoma jibu hili toka kwa Rais wa TFF.
FaizaFoxy ahsante kwa wazo jema,we are also thinking along those lines.Nchini mwetu tuna shule za msingi yapata 19600,our plan ni kuandaa mtaala wa kufundisha mpira nchini ili kila shule ifundishe mpira unaofanana na tuhakikishe kupitia TAMISEMI kila shule inakuwa na mwalimu wa mpira/michezo pamoja na kupata mipira ya size stahili (size 3 na 4).Pia ni muhimu kuwa na tournament za uhakika za mpira wa watoto na vijana.Yote kwa yote huwezi kutenga vilabu kwa sababu baada ya kuvuka umri wa miaka 17 lazima vijana hawa wapate vilabu vya kuchezea.
Nakukubali kitu kimoja tu kuwa active JF, hadi mimi wa Mlooo Mbeya nakusoma ila maswala ya Mengine ya soka wewe ni walewale tu.ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
uanachama wetu cecafa ni wa kisiasa na kihistoria kuanzia enzi za Gossage tukipigania uhuru.Mwaka huu tuliwaomba cosafa watualike nafasi ikawa ngumu (wamealika Ghana ).Hata hivyo usidhanie kote ni shwari,changamoto za uongozi ziko kila mahali,ni kukabiliana nazo tu.
Mheshimiwa mbona unarahizisha sana, hivi TFF haina kura ya Veto kushinikiza jambo fulani ndani ya CECAFA.?maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
tatizo hawajui hasira za wadau mitaani.Hayo ndio yanawafanya msikosoleke, sasa kama ya kijinga nisikwambie ya kijinga? staha katika ukweli? ndio maana mpaka leo ni kichwa cha mwendawazimu.
Usipoukubali ukweli hutaendelea hata siku moja. Ujinga ni ujinga tu hauna jina lingine.
ndugu yangu hapa tutakesha,naomba ukubali tu kuwa maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
Kifupi Tanzania ya sasa uzalendo ni zilo kwa Kila idara.