Maswali muhimu kwa Rais Kikwete

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,305
Ningepata kukaa na Rais Kikwete ningekuwa
mkarimu na mpole na kisha ningeanza maswali
yangu kama ifuatavyo. • 1: Ningemuuliza kuhusu MIAKA MINANE
  anayotimiza akiwa madarakani na kama
  anadhani ametimiza asilimia 80 ya ilani yake
  ya uchaguzi (Si mnajua miaka minne kati ya
  mitano ni 80%?)

 • 2: Ningemuuliza kama ana IMANI NA
  VIONGOZI wake wasaidizi, na kama ndio basi
  kwa asilimia ngapi. Na kama hana anafikiri ni
  kwanini anaendelea kuwa nao na anakabiliana
  vipi na hilo?


 • 3: Ningemuuliza ameweza KUTEMBELEA
  MIKOA MINGAPI (ukilinganisha na ile
  aliyotembelea wakati wa kampeni na
  anayopanga kutembelea kwenye kampeni
  zijazo) na ameweza kutambua matatizo
  makubwa mangapi ambayo hakuyajua kabla?
  Na baada ya kuyatambua anadhani ana
  suluhisho kiasi gani?


 • 4: Ningemuuliza anapata na kuhakiki vipi
  taarifa za utendaji wa mikoani.


 • 5: Ningemuuliza ni MABADILIKO gani
  amefanya ama kupanga kufanya baada ya
  kuona hali halisi ya JELA alizozitembelea na
  kunukuliwa akisikitishwa na hali ya huko.


 • 6: Ningemuuliza juu ya TAKWIMU halisi za
  maendelea ya ELIMU (sio majengo
  "yanayoota" kila kata)na pia Takwimu za
  AFYA (sio zahabati zisizo na dawa wala
  wauguzi) Ningemuuliza namna anavyoamini
  Serikali inawajali wale waliojitoa mhanga
  kuitumikia kama wafanyakazi wa Jumuia ya
  Afrika Mashariki, Walimu na wengine.


 • 7: Ningemuuliza kama bado anaamini kuwa
  KILIMO NI UTI WA MGONGO WA UCHUMI WETU
  na kama kuna mipango yoyote ya
  kukiboresha. Hapa ningemkumbusha kuhusu
  AHADI aliyoitoa Waziri Mkuu kuwa
  wasingenunua Mashangingi na badala yake
  wangenunua matrekta kwani shangingi moja
  ni sawa na gharama za matrekta 20.
  (Jikumbushe Hapa)


 • 8: Ningemuuliza juu ya MIUNDOMBINU na
  MAWASILIANO na kama anajua kuwa kuna
  mazao yanayooza mikoani kwa kukosa
  usafiri wa kuyaleta "sokoni" wakati kuna
  wanaokosa chakula upande wa pili wa nchi.
  Ningemuuliza kama tunatumia rasilimali kama
  mvua, mito na jua kwa manufaa ya jamii
  nzima.


 • 9: Ningemuuliza kuhusu RUSHWA na
  MATUMIZI MABAYA yanayosemwa kwa
  serikali na watendaji wakuu wake na kama
  kuna hatua zinazochukuliwa juu ya hilo.
  Labda ningemgusia kuhusu "msururu" wa
  watu wanaoongozana kwenye mikutano
  mbalimbali ambayo nchi nyingine zawakilishwa
  na watu wachache (kama ilivyonukuliwa
  HAPA ) • 10: Ningemuuliza juu ya ZIARA zake za nchi
  za nje na kama anawaelimisha wananchi jinsi
  ambavyo ziara hizo zinaisaidia Tanzania.
  Hapa sina shaka kuwa kuna manufaa kwa
  nchi, lakini yeye kama MWAJIRIWA WA
  WANANCHI ANALAZIMIKA KUWAELEZA
  WANANCHI MANUFAA YA ZIARA ZAKE na
  ningeuliza kama anajua kuwa Tovuti hii
  mfu Ya Ikulu na Blogu ya Mawasiliano
  Ikulu ni kati ya zile zenye habari chache
  kuhusu utendaji wake kuliko blogu zetu kina
  "@Gambas"?
  Labda ningemuuliza kama HABARI ZA
  MAENDELEO YA UTENDAJI WAKE NI HAKI
  AMA ANASA KWA WANANCHI WA Tanzania?
  Sina hakina na muda kama ungetosha lakini
  ningepata wa ziada ningeuliza kuhusu
  maendeleo ya Ripoti za Richmond na nyingine
  ambazo ninaamini "wanazifanyia kazi", ila
  hawajatujulisha walipofikia.
  Najua angekuwa (kwa hakika ANASTAHILI)
  kuwa na majibu maana "anatenda kazi
  yake".
 
Watanzania hebu tujaribu kufikiri kidogo swala hili, wanaojiita watetezi wa wananchi hapa wanasemaje mbona wanaouza nchi ni ccm?Kigamboni mpo kwa nani!
 
Back
Top Bottom