Mfukutuzi
JF-Expert Member
- Feb 15, 2015
- 239
- 175
MASWALI 5 YA MSINGI UVAMIZI WA NDG. HUMPHREY POLEPOLE
Hatukatai moja kwa moja kwamba alivamiwa ila ni vyema akatusaidia kujibu haya machache;
1. Anasema aliwasikia Majambazi wanavunja uzio kisha akapiga simu kwa rafiki yake Mwanahabari ndiye akamtolea taarifa Polisi, na baadae Polisi ndipo wakaja eneo hilo na kuwafanya majambazi wakimbie, hivi ni kweli inawezekana muda wote huo uliotumika kufanya mawasiliano mpaka amri ya Polisi itoke tena usiku wa manane vile na mtiririko huo wa utoaji taarifa Majambazi walikuwa bado wanahangaika na uzio tu?
2. Au la Nyumba ya Polepole iko Nyuma tu ya kituo cha Polisi kiasi cha kuchukua sekunde chache vile kufika kwake?
3. Taarifa yake inasema hakuna madhara yaliyoripotiwa lakini mbona mwanzo anasema alisikia Majambazi wakivunja uzio au uzio siyo sehemu ya hayo madhara?
4. Hata kama ni kweli alivamiwa kipi hasa kilimfanya atambue kuwa ni Majambazi na si vibaka pengine?
5. Kama kavamiwa, kwa nini taarifa hii ianzie Gazetini na si Polisi? Iko wapi taarifa ya kipolisi?
USHAURI WANGU: "Tujifunze kutunza heshima tunazopata baada ya kufanya kazi za heshima"