mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Kwa mara ya kwanza nimguswa na maswali magumu ya Mh Zitto kuhusu hamahama ya Wanasiasa, kama yalivyonukuliwa kwenye gazeti la Nipashe, Jumapili Desemba 17, 2012.
Nayaweka hapa chini:
1) Je, hakuna sababu za ndani sisi wenyewe zinazokimbiza wanachama wetu? Kama zipo ni zipi?
2) Je, ni sababu ambazo tunaweza kuzirekebisha na kukiimarisha chama?
3) Kama ni sababu zilizo nje ya uwezo wetu tunafanya nini ili kuzikabili?
4) Je, bado sisi tunaamini katika misingi ya chama kwa mujibu wa Azimio la Tabora?
5) Tulikuwa kundi tu tulioumizwa na vyama tulivyokuwamo na tukaamua kuunda chama kupoza hasira zetu tu na sasa hasira zimeisha, hakuna sababu ya chama kuwapo?[/B.
Hongera Mh Zitto kwa kuwa mkweli. Mawazo hayo yanakuingiza kwenye kundi la wanasiasa waliokomaa.
Kwangu mimi sababu kubwa ya kuhamahama ni kubadilika kwa mitazamo, imani na itikadi ya viongozi wa juu wa vyama vya siasa tofauti na msingi ya vyama vyenyewe. Hii ikichangiwa na nguvu wanayokuwa nayo viongozi, ufinyu wa demokrasia ndani ya chama, na uchu wa madaraka, wanachama/viongozi wasio na uvumilivu, au wanaojitambua huamua kuhama.
Maswali ya Mh Zitto yanahitaji mjadala wa kina.
cc: Mwanahabari Huru, tindo, swissme, Daudi Mchambuzi, kisu cha ngariba, francis12, barafuyamoto, Retired, Erythrocyte, Paskali, jingalao, Nyani Ngabu, MM, Petro E. Mselewa, nk