Maswali magumu: Viko wapi visu vya Mahita?

Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.

Ukitaka kujua mchumia tumbo ni yupi kati ya alieandika makala na wewe chukua kioo na angalia utamuona!
 
hakuna anayejua nyumbani kwa mahita?tanzania kuna vituko sana,yani lile jambawazi nalo lilikuwa IGP!
Huwa wanayaweka majambazi makusudi ili kulinda maslahi yao. Mahita yupo Morogoro anapiga jaramba agombee ubunge 2015 kwa chama chao cha majizi.

Eti Said Mwema naye amepata tuzo ya utumishi uliotukuka,,, what a shame.
 
makala n nzuri na iko wazi,cha msing 2naenda mashinani na vijiwen kujidhatiti kwa sana tu.
 
"Serikali ya ccm imevaa miwani ya mbao" by muona mbali DEO FILIKUJOMBE(mbunge wa ccm ludewa) swali: hata masikio na yenyewe wameka pamba? Maana kila jambo walishaambia ila wameamua kujifanya sikio la kufa!!!!!!!!!!
 

Hilo container la visu limehifadhiwa ikulu ya Kikwete, 2015 atamkabidhi IGP Mwema ili vifanye kazi!!
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.


na wewe pia unaweza kutoa majibu ya hayo maswali aliyoyauliza mwandishi wa huu uzi

nahisi wewe utakuwa hujatahiriwa kiakili#
 
Udini ni maneno aliyojinadi nayo mgombea wa chama chenu. yamemshinda kuyabeba anahaha kuita viongozi wa dini magogoni. mi ningekuwa wao nisingeenda alafu.
 
Kuonesha mapanga na kusema CUF ni chama cha waislam ni CCM kuuzalilisha uislam. Nashangaa waislam wanaoshabikia CCM

Unadhani msemaji wa waislamu Tanzania ni nani? Ulishawahi kuuliza huyo msemaji (shekh mkuu) yuko chini ya chombo gani (Baraza)? analipwa na nani?. Je waislamu baadhi yao kama kina ponda ambao leo wana kesi za jinai uliwasikia wanaungana na hicho chombo?. Kwa sasa taifa liko katika sekeseke la mambo ya udini, Ulishamsikia kiongozi gani wa Waislamu akiongelea hilo?. Ukishapata majibu ya baadhi ya hayo maswali ndio utajua kuwa waislamu Tanzania wana viongozi wa kusema au hakuna na kama wapo wako chini ya nini mpaka wasiongee chochote.
 


Uwezo wako wa kufikiri ndio umeishia hapo, pole sana!
 
HUo ni unafiq mbona hamkuwasaidia wakati wanachafuliwa kipindi kile na mahita?.kwahiyo mliwasaliti?kwanini?

Mkuu! Hatukuwa na mdomo mpana wa kusemea kama jinsi tunavyo yasema leo, hata hivyo kwa kuwa tulishindwa kuyasema kipindi kile haituzui kuyasema leo maana bado yanahusiana na medani ya za kisiasa tena kwa kufuata mkondo ule ule.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tanzania bila ya CCM nchi itayumba -Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere 1995 kwenye Mkutano mkuu Chimwaga
 
Udini ni maneno aliyojinadi nayo mgombea wa chama chenu. yamemshinda kuyabeba anahaha kuita viongozi wa dini magogoni. mi ningekuwa wao nisingeenda alafu.

eti ungekuwa wewe usingeenda!! Ndio maana Huwezi kuwa wewe labda uanzishe dini yako wewe na mumeo chumbani wewe kiongoz yeye mfuasi halaf ndo ujisifie kugomea Mwaliko wa Mh.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete!
 
Mwandishi wa hii makala atakuwa ni mchumia tumbo.

Anauliza swali halafu anajijibu yeye mwenyewe.
Hayo ndiyo maoni yako. Naona unajua nani mchumia tumbo wa kweli kati yako na mwandishi wa makala hiyo lakini ili wewe na watoto waende choo na umudu 'kavocha' ka kutumia huo, mtumba wako wa BB inabidi uandike kila anachokueleza mwajiri wako!
 
 
Mchumia tumbo ni wewe uliyecoment uharo kwenye thread ya mwenzako ili ulambe buku saba

hakuna anayejua nyumbani kwa mahita?tanzania kuna vituko sana,yani lile jambawazi nalo lilikuwa IGP!

tatizo wanazani wale wadanganyika wa 2005 wanaendelea kuwa na influence katika jamii ya kizazi hiki?

Asante ngurumo. Makala yako inafikirisha sana.

Mkuu, kwa kum quote kwako huyo Kinaja umemuongezea Bonus leo Lumumba

Kuonesha mapanga na kusema CUF ni chama cha waislam ni CCM kuuzalilisha uislam. Nashangaa waislam wanaoshabikia CCM
Baada ya miaka kadhaa kupita leo wameupgrade wameibuka na remix yake.

 
KWANINI serikali inahangaika kupandikiza hisia za udini na ugaidi katika siasa? Mwaka 2005 ilikitangaza Chama cha Wananchi (CUF) kuwa cha kidini na kigaidi. Sasa hivi inasema vitu viwili.

Kwanza, inasema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kidini, kikabila na kigaidi. Pili, inawatumia makada wake kutamka kwamba chama hicho kitakufa.

Tunajua kuwa inafanya hivyo kunusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lakini kwa tabia hii, tutaiita serikali au genge la wapika propaganda za kigaidi?

Hebu tuulizane. Watawala wanaotumia na kupandikiza hisia za udini na ukabila kama mbinu ya kuwashinda wapinzani wao wanastahili kuaminiwa tena? Wanaweza kuzungumzia amani na utulivu?

Watawala wanaoingiza Jeshi la Polisi katika misukosuko ya kiitikadi, wanadhani wanapanda mbegu ya amani na ustahamilivu? Chama cha siasa kinachotegemea nguvu za dola kama njia ya kupata ushindi kina haki ya kuendelea kuaminiwa?

Tukumbushane. Mwaka 2005, katikati ya joto kali la Uchaguzi Mkuu, baada ya kubanwa na CUF, serikali ilimtumia Mkuu wa Jeshi la Polisi wa wakati ule, Inspekta Jenerali Omar Mahita, kutisha wapiga kura.

Mahita akajidhalilisha, akaibukia kwenye TV akiwa na visu vilivyopakwa rangi za bendera ya CUF, akisema jeshi lake limekamata kontena la visu ambavyo chama hicho kilikuwa kinakusudia kufanyia ugaidi.

Hadi leo hawajatueleza visu hivyo vilipelekwa wapi. Hatujaambiwa kontena hilo liliishia wapi. Hatujasikia mtu yeyote au kiongozi wa CUF amekamatwa kwa ugaidi. Wala hakuna kesi yoyote mahakamani dhidi ya viongozi au wanachama wa CUF kutokana na tukio hilo.

Ni dhahiri lilikuwa tukio la kupika na kuidhalilisha CUF mbele ya umma. Ilikuwa mbinu ya ushindi mchafu. Na kwa kuwa iliwasaidia kuipiku CUF na kuidhoofisha, sasa wamedhani mbinu ile ile itakuwa msaada kwao kuimaliza CHADEMA.

Ndiyo maana na tambo zao eti CHADEMA kitakufa kabla ya 2015. Ndiyo sababu ya kauli za kidini, kikabila ka kigaidi dhidi ya CHADEMA. Wanapanda mbegu chafu katika siasa za Tanzania, kwa hofu tu ya kuondoka madarakani!

Halafu wanathubutu kusimama majukwaani kutamka kwamba wapinzani wana uchu wa madaraka. Yapi? Nani anangangania madaraka kati ya wale waliokaa madarakani kwa miaka 50 na wale wanaotaka kuingia madarakani kwa mara ya kwanza?

Mbinu chafu za kutumia vyombo vya dola, udini, ukabila na ugaidi hazioneshi uzoefu, weledi, wala umakini katika kutawala. Kwa maana nyingine, tunaweza kusema miaka 50 ya kukaa madarakani haijawasaidia watawala wetu. Bado wanabahatisha!

Zaidi ya hayo, wanatujengea Jeshi la Polisi lisilo adilifu, lililo tayari kuingizwa kwenye michezo michafu ya kihuni na kihalifu kwa ajili ya kutukuza watawala.

Kama leo tungeulizana, upo wapi uadilifu wa Mahita? Tunakuwa na uhakika gani na uadilifu wa viongozi wa Jeshi la Polisi baada ya Mahita?

Kwanini serikali inataka kulifikisha Jeshi la Polisi mahali ambapo halitaheshimika wala kuaminika? Kwanini inatumia vyombo vya dola kukandamiza haki na kulinda uovu?

Na baada ya yote yaliyotokea katika nchi za wenzetu Syria, Tunisia, Misri, Libya, Kenya,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…