Kwani Kamanda Sirro si alisema atatoa taarifa jumanne,sasa hii haraka imetokea wapi? Mwandishi wa Mtanzania anataka kuuaminisha umma kuwa kuna kisasi. Labda ajue kuwa marehemu Thomas huko Mirerani hakuwa anaongoza kikosi cha kupambana na uhalifu,bali alikuwa mkuu wa kituo OCS wa Mirerani hapo,binafsi nimemfahamu akiwa Mkaguzi (Inspector) na tayari akiwa ni mkuu wa hicho kituo. Mali za marehemu zote alizopata,alizipata kwa kuzama na kuchimba Madini kama Mwana Apolo yeyote hapo mgodini na sio kwa upolisi wake. Hawa waandishi wanahitaji kuandika habari zenye kuzua hisia wajiridhishe kwanza na vyanzo vyao vya habari. Maziko yake yatafanyika kwao kwa taratibu za kijeshi ikiwemo kupiga risasi na risala na rambi rambi huko kwao