mzalendo-wa-tz
JF-Expert Member
- Dec 15, 2014
- 404
- 187
Maswali 14 yaliyoibuliwa na tafiti ya Twaweza
1. Kwa mara ya kwanza Twaweza walisoma ripoti ya utafiti na kuonyeshwa moja kwa moja na TV. Nani alidhamini utafiti, matangazo hayo na kwa madhumuni gani?
2. Kwa nini waliamua kutoa matokeo ya utafiti wao katikati ya kampeni zenye ushindani mkali na mhemko mkubwa wa kisiasa?
3. Je, ni jinsi gani watu waliohojiwa walichaguliwa?
4. Je, watu waliohojiwa ni wa kutoka maeneo gani, makundi gani ya watu, ukiacha jinsia?
5. Je, waliohojiwa wamejiandikisha kupiga kura, mashabiki tu au mchanganyiko?
6. Twaweza wanajua kwamba kampeni za wagombea urais huanza baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuidhinisha wagombea waliopendekezwa na vyama. Kwa nini shirika hilo lilianza kufanya utafiti siku mbili kabla ya hapo?
7. Twaweza wanasema wahojiwa hawakupatiwa orodha ya majibu ya kuchagua. Je, ni kweli hawakuwa wanawajua wagombea wengine waliotajwa zaidi ya Dk John Magufuli na Edward Lowassa wakabaki kusema "mwingine?"
8. Katika nafasi ya ubunge na udiwani, wahojiwa wameonyesha kuwajua na kuwapigia kura wagombea wa ACT-Wazalendo. Inakuwaje watu hao hao washindwe kumtaja mgombea urais wa chama hicho badala yake Twaweza ikamweka katika kundi la "mwingine?"
9. Takwimu zote asilimia huwa ni 100 iliwezekanaje mgawanyo wa takwimu katika ripoti ya Twaweza katika baadhi ya maeneo asilimia zilizidi na au kupungua 100?
10. Tafiti zilizopita za Twaweza zilikuwa zinajumuisha watu wengi na zilikuwa zinaonyesha mtu aliyeshika nafasi ya kwanza pengine hadi 10. Kwa nini katika utafiti huu waliwalenga wawili tu Lowassa na Magufuli?
11. Ripoti inasema kwamba dodoso la utafiti huu liliandaliwa kabla ya uteuzi wa wagombea urais wa vyama vingine (nje ya mseto wa Ukawa), kikiwamo ACT-Wazalendo. Je, dodoso hilo lilikuwa na maelekezo gani kiasi kwamba ikawa vigumu kuwaingiza wagombea wengine?
12. Kwanini matokeo ya utafiti na kinachoonekana nje ni picha mbili tofauti?
13. Matokeo ya awali ya Twaweza yalionyesha Lowassa alipokuwa CCM aliongoza kwa ushawishi, iweje ndani ya wiki mbili baada ya kuhamia upande wa pili aporomoke hivyo?
14. Kwanini Twaweza hawakushirikisha Zanzibar katika utafiti wakati urais ni wa Muungano?
From Mwananchi Tanzania